JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatatu, 7 Julai 2025

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

....,.........

๐Ÿ“ŒApatiwa elimu juu ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa  Nishati safi ya kupikia

๐Ÿ“Œ Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa tasisi zake kutekeleza majukumu yake kikamilifu

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi leo 7 Julai, 2025 ametembelea banda la Wizara ya Nishati  kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba jijini Dar es salaam

Akiwa kwenye banda la Wizara ya Nishati Mhe Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa kitengo cha  Mawasiliano Serikalini Bi Neema Chalila Mbuja, ambapo alimweleza juu ya hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa ajenda hiyo ni utekelezaji wa azimio la Mhe Rais Samia kama kinara wa nishati safi ya kupikia.

Amesema Wizara ya Nishati kupitia taasisi zilizopo chini ya Wizara zimekuwa zikitekeleza kwa vitendo ajenda hiyo kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambae ni kinara wa nishati safi ya kupikia kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Wizara ya nishati tayari imezindua mikakati miwili ya nishati safi ya kupikia na ule wa mawasiliano ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo

 

BALOZI HAMAD AKUTANA NA RAIS WA BUNGE LA MSUMBIJI

 Mhe. Balozi Hamad Khamis Hamad amekutana na Mhe. Margarida Adamugu Talapa, Rais wa Bunge la Jamhuri ya Msumbiji kwenye Ofisi za Bunge hilo Leo Jijini Maputo   Julai 07, 2025;

Wakati wa mkutano huo, Mhe. Talapa alimpongeza Mhe. Balozi Hamad kwa kuteuliwa kuiwakilisha Tanzania nchini Msumbiji na kumhakikishia kila aina ya ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake. Aidha, alieleza kutambua ushirikiano na msaada wa Tanzania tokea wakati wa mapambano ya kutafuta Uhuru wa Msumbiji na jitihada zinazoendelea za kutafuta amani Kaskazini mwa Msumbiji.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Hamad alimshukuru Mhe. Talapa kwa kukubali kukutana naye na alimhakikishia kila aina ya ushirikiano kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidugu na historia baina ya Tanzania na Msumbiji. Aidha, alishauri kuhusu umuhimu wa Mabunge ya nchi hizi mbili kuendeleza ushirikiano hasa baada ya Tanzania kumaliza Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba, 2025.

Mwisho, alieleza kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana Serikali na Wananchi wa Msumbiji katika maeneo mbalimbali hususan utunzaji wa amani Kaskazini mwa nchi hiyo ambapo Majeshi ya Tanzania yanaendelea kusaidia kwenye mapambano dhidi ya vikundi vya kigaidi.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Maputo. 

LUHEMEJA AWATAKA WATANZANIA KUTOA UZITO NA MSISITIZO UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA


..............

WATANZANIA wamehimizwa kulipa uzito na msisitizo suala la uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini kwani ni agenda muhimu ya kimaendeleo kwa binadamu.

Hayo yamesemwa leo Jumapili (Julai 6, 2025) Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akizindua Siku ya Mazingira iliyoadhimishwa katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF).

Luhemeja amesema  Dunia inakabiliwa na changamoto za kimazingira zikiwemo ukataji miti, upotevu wa viumbehai, kupanda kwa joto, hivyo jitihada za pamoja baina ya Serikali, Asasi zisizo za Serikali, sekta binafsi na wananchi zinahitajika katika kukabiliana na hali hiyo.

”Natoa rai kwa Watanzania kudumisha utamaduni wa kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa taka na kukata miti hovyo. Aidha, tuendeleze utamaduni wa kupanda miti na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa kutumia nishati safi ya kupikia” amesema Mhandisi Luhemeja.

Ameongeza kuwa Tanzania imebarikiwa urithi mkubwa wa rasilimali asilia na vivutio vya kipekee vinavyotambulika kitaifa na kimataifa ikiwemo misitu, ukanda wa bahari, uchumi wa bahari, eneo la misitu ya mikoko, hivyo endapo mazingira yataendelea kuharibiwa rasilimali hizo hazitakuwa salama.

Mhandisi Luhemeja awataka wananchi na  wadau kupunguza matumizi ya plastiki kwa kutumia falsafa ya ”Punguza, Tumia Tena na Rejeleza” ambapo kwa mujibu wa tafiti zimebainisha kuwa taka za plastiki huchukua miaka 400 mpaka 1,000 kuoza ardhini na hivyo kuleta athari hasi kwa afya ya binadamu, mazingira na uchumi.

Ameeleza kuwa katika kukabiliana na changamoto za mazingira,  Serikali kwa kushirikiana na wadau imefanya jitihada mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kuandaa na kutekeleza Sera ya Taifa ya Mazingira, Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, Mchango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Maafa.

Ameeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya kaya nchini bado zinaendelea kutegemea kuni na mkaa kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia, hivyo Serikali imezindua Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia (2024–2034) unaolenga kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.

“Mkakati huu unaonesha dhamira ya kweli ya kumkomboa Mtanzania dhidi ya athari za nishati chafu, hasa wanawake ambao ndio wahanga wakubwa. Hili si suala la majiko au mafuta tu, bali linagusa afya, heshima, fursa na haki ya kuishi katika mazingira bora” amesema Mhandisi Luhemeja.

Awali Mkurugenzi wa Usimamizi wa Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bi. Lulu Mkudde amesema tukio la uzinduzi wa Siku ya Mazingira ni la kwanza kufanyika tangu shughuli na huduma za maenesho hayo kuanza nchini.

Amesema kuwa TANTRADE itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais katika masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini hususani kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na upandaji miti.

“Tunatambua suala la uhifadhi wa mazingira kwa sasa limekuwa ni fursa ikiwemo biashara ya kaboni ambayo imeendelea kunufaisha jamii ya Watanzania. Tutaendelea kuunga mkono juhudi hizi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya jamii yetu” amesema Mkudde.

MWISHO

  

MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI YAFANYIKA OSAKA JAPAN

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Kiswahili duniani, tarehe 7, Julai, 2025. Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika eneo la Yumeshima; jijini Osaka, nchini Japan, yamekuwa sehemu ya maonesho ya biashara ya dunia (Expo 2025, Japan) yanaondelea nchini Japan.

Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya siku ya Kiswahili kikanda (Afrika Mashariki) yanafanyika nchini Rwanda na kwa Tanzania, maadhimisho hayo yanafany9ika visiwani Zanzibar.  

OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA USHAURI KATIKA MIKATABA KWA TAASISI ZA UMMA

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kuboresha Ushauri kwa Taasisi za Umma wakati wa kuingia mikataba mbalimbali ili kuwa na Mikataba iliyobora na kutimiza malengo ya Serikali ya kuwa na mikataba inayotekelezwa vizuri na kuwanufaisha Wananchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel M. Maneno tarehe 7 Julai, 2025 katika Maonesho ya Kimataifa ya 49 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

*"Tunaendelea kuzipa ushauri Taasisi za Umma ili kuwa na ubora wa mikataba pia kuhakikisha kwamba utekelezaji wa Mikataba hiyo unafanyika kwa mujibu wa Makubaliano".* Amesema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayatumia maonesho hayo katika kutoa Ushauri wa Kisheria, Kushughulikia Malalamiko, Utatuzi wa Migogoro na Elimu ya Sheria hususani sheria zilizofanyiwa Urekebu toleo la Mwaka 2023 zilizoanza kutumika Julai 1, 2025.

*"Sheria zilizofanyiwa urekebu zimezinduliwa na zimeanza kutumika na kitu kizuri ni kuwa kati ya sheria 446 sheria 300 zinapatikana kwa lugha ya kiswahili".* Ameeleza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Katika hatua nyingine Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitembelea mabanda ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria pamoja na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, kuona shughuli zinazotekelezwa na Taasisi hizo katika maonesho hayo.

Maonesho ya Sabasaba 2025 yamezinduliwa rasmi leo tarehe 7 Julai, 2025 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambapo maonesho yanatarajiwa kumalizika tarehe 13 Julai, 2025. 

MAGAZETI YA TZ LEO JTATU JULY 7/7/2025.....karibu usome hap

Listen Mkisi Radio