JSON Variables

Friday, March 14, 2025

WAZIRI MKUU AZINDUA MSIKITI WA NUURIL HIKMA

*****

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 14, 2025 amezindua msikiti wa Masjid Jaami’u Nuuril Hikma uliopo mtaa wa Yombo, Temeke jijini Dar es Salaam ambao umejengwa na Taasisi ya Al-Hikma

Akizungumza baada ya kuzindua msikiti huo, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa jamii na Watanzania watakaotumia msikiti huo kuutunza kwani kufanya hivyo ni njia ya kudumisha uhusiano na Mwenyezi Mungu na inahesabika kama sadaka.

“Mtume Muhamad S.A.W anatufundisha pia kutunza nyumba za ibada, msikiti ni sehemu ya jamii na ni mahali pa ibada na umoja. Kupitia hadithi ya Bukhari, ni wajibu wa waumini kutunza msikiti, kuhakikisha kwamba ni sehemu safi, na inakidhi mahitaji ya ibada na mafunzo ya kiislamu.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa msikiti ni kituo cha kiroho, kijamii, kiutamaduni na nyumba kwa ajili ya ibada na unatoa nafasi kwa waumini kushirikiana katika ibada, kujifunza, na kujenga jamii bora kwa kutoa huduma za kijamii.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini kuliombea Taifa pamoja na kukemea vitendo vyote visivyo mpendeza Mwenyezi Mungu.

“Tunajua mnaliombea Taifa hili, ila endeleeni kufanya hivyo ili utulivu huu uendelee, tuachane na mambo yatakayoleta adha kwenye jamii, tunafurahi mnavyohubiri amani na mshikamano, Mwenyezi Mungu analipenda Taifa hili.”

Pia Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza Taasisi ya Al-Hikma kwa ujenzi wa msikiti huo. “Ujenzi wa Msikiti huu ni ishara ya juhudi za taasisi hii katika kuimarisha misingi ya imani na maadili mema katika jamii”.

Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt Abubakar Zuber Ali Mbwana amesema kuwa maendeleo sio ugomvi bali ni kufanya mambo yanayoonekana na yanayompendeza Mwenyezi Mungu ikiwemo ujenzi wa msikiti “fitna, ugomvi, fujo kwenye misikiti hatutaki, tupendane na heshima itawale.”





 

TANZANIA NA JAPAN ZASAINI MKATABA WA MSAADA WA BILIONI 27.3 KUSAIDIA SEKTA YA AFYA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Kulia), na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoichi Mikami, wakisaini Hati za Mkataba (Exhange Note) wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3), kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika hafla iliyofanyika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Kulia), na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoichi Mikami, wakibadilishana Hati za Mkataba (Exhange Note) wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3), kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika hafla iliyofanyika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Kulia), na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoichi Mikami, wakionesha Hati za Mkataba (Exhange Note) wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3) baada ya kusaini, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika hafla iliyofanyika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara, wakibadilishana Hati za Mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3) baada ya kusaini, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika hafla iliyofanyika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara, wakionesha Hati za Mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3) baada ya kusaini, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika hafla iliyofanyika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza baada ya hafla ya kusaini Hati za Mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3) kati ya Serikali ya Tanzania na Japan, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa fedha hizo zitaboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma bora za afya hususani Huduma ya Mama na Mtoto kwa kutoa vifaa-tiba vya kisasa vitakavyoongeza uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu katika Hospitali saba za Rufaa.

Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoichi Mikami, akizungumza jambo baada ya hafla ya kusaini Hati za Mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3) kati ya Serikali ya Tanzania na Japan, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa Serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuchochea maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara, akizungumza jambo baada ya hafla ya kusaini Hati za Mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3) kati ya Serikali ya Tanzania na Japan, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa JICA imekua ikishuhudia maboresho katika ufanisi, usalama, na ubora wa huduma na wanaamini kuwa hayo yote yamechangia kwa kiasi kikubwa katika kufikia Lengo la Upatikanaji wa Huduma za Afya kwa Wote (Universal Health Coverage (UHC)) nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Katikati mstari wa mbele) Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoichi Mikami (wa pili kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Bw. Ismail Rumatila (wa kwanza kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melkizedeck Mbise (wa kwanza kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, JICA na Ubalozi wa Japan nchini, baada ya hafla ya kusaini Hati za Mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi za Tanzania bilioni 27.3) kati ya Serikali ya Tanzania na Japan, kwa ajili ya ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dar es Salaam)

...................

Na. Scola Malinga na Joseph Mahumi, WF, Dar es salaam

 

Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), zimetiliana saini mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 (sawa na shilingi bilioni 27.3) kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini.

 

Mkataba huo umesainiwa katika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami na 

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara, kwa niaba ya Serikali ya Japan.

 

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto. 

 

Dkt. Mwamba alisema kuwa, ufadhili huo muhimu unaendana na Mpango wa sasa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao pamoja na masuala mengine, unalenga kutatua changamoto za ubora katika utoaji huduma za afya nchini. 

 

“Ufadhili huu unaunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta ya afya, zinazolenga kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wakati kwenye jamii,” alisema Dkt Mwamba.

 

Aliongeza kuwa mradi huo utatekelezwa na Wizara ya Afya na utaboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma bora za afya hususani Huduma ya Mama na Mtoto kwa kuwa na vifaa-tiba vya kisasa vitakavyoongeza uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu katika Hospitali saba za Rufaa ambazo ni: Dodoma, Tumbi iliyoko mkoa wa Pwani, Mount Meru iliyoko Arusha, Sekou-Toure iliyoko Mwanza, Songea iliyoko Ruvuma, Maweni iliyoko mkoani Kigoma na Hospitali ya Lumumba iliyoko Zanzibar.

 

“Msaada huu ni mwendelezo wa ushirikiano unaokua kati ya nchi zetu mbili kama inavyodhihirishwa na kuongezeka kwa idadi ya miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia misaada na mikopo nafuu”

 

Dkt Mwamba aliishukuru Japan kwa ufadhili huo na mingine ambayo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kuchochea maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi na kuboresha Maisha ya Watanzania. 

 

“Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kwa faida ya watu wetu na Serikali itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa” alisema Dkt. 

Mwamba.

 

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoichi Mikami, alisema kuwa kwa kutambua ushirikiano wa nchi hizo mbili, Japan imekuwa ikitoa misaada katika sekta ya afya ili kuchochea maendeleo ya watanzania. 

 

“Serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuchochea maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi na kuboresha Maisha ya Watanzania,” alisema Mikami.

 

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara, alisema kuwa JICA imekuwa ikitoa msaada mkubwa katika sekta ya afya ya Tanzania kwa miaka mingi, katika kuimarisha usimamizi wa hospitali na kujenga uwezo wa usimamizi wa ubora wa huduma za afya kupitia mbinu mbalimbali, katika Hospitali za Rufaa za Kanda. 

 

Bw. Hitoshi alisema kuwa, JICA wamekuwa wakishuhudia maboresho katika ufanisi, usalama, na ubora wa huduma na wanamini kuwa hayo yote yamechangia kwa kiasi kikubwa katika kufikia lengo la Mpango was Upatikanaji wa Huduma za Afya kwa Wote (Universal Health Coverage (UHC)) nchini Tanzania.

 

Aliongeza kuwa wakati viwango vya vifo vya kina mama nchini Tanzania vimeimarika kwa kiasi kikubwa, kutoka 760 kwa kila vizazi 100,000 mwaka 2000 hadi 238 mwaka 2020, pia vifo vya watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano vimepungua.

 

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Bw. Ismail Rumatila, alishukuru kwa msaada huo na alisema kuwa utasaidia kununua vifaa katika hospitali saba za rufaa vitakavyoongeza uwezo mkubwa wa uchunguzi na matibabu.


 

AFISA MWANDIKISHAJI JIJI LA DSM ASISITIZA MAMBO MATANO KWA WABORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA.

.....................

Na:Shalua Mpanda

Afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es salaam Wakili Faraja Nakua amefungua mafunzo kwa waendeshaji wa  vifaa vya Bayometriki na waandishi wasaidizi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya kata na kusisitiza mambo matano muhimu ili kufanikisha zoezi hilo.

Wakili Nakua amesema zoezi hilo la uboreshaji linalotarajiwa kuanza Machi 17,2025 ni muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Amewataka Watendaji hao kuwa na weledi, nidhamui,kujituma kazini,bidii ya kazi pamoja na kuwa na lugha nzuri na zenye staha kwa "wateja" wao ambao ni wananchi.

"Wateja wetu Wapiga kura watakaojitokeza kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura,kuboresha taarifa zao au kuondoa taarifa za wapiga kura ambao hawana sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari hilo,hivyo tunapaswa kuwa na lugha nzuri kwao na zenye staha".Alisisitiza Afisa huyo.

Aidha amewataka waandishi  na Waendesha Vifaa hao kufanya kazi kwa ushirikiano na wakala wa vyama vya Siasa katika vituo vyao na kutambua kuwa Wakala hao sio maadui bali ni wadau wanaowezesha zoezi hilo kukamilika.

Ameongeza kusema kuwa wanapaswa kuhakikisha wakala wa vyama hivyo vya Siasa hawavuki mipaka ya kazi yao.

Mafunzo haya ya  Waendesha Vifaa vya Bayometriki na waandishi wasaidizi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yanafuatia mafunzo ya awali yaliyofanyika mapema wiki hii kwa Watendaji ngazi ya Jimbo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ndugu Ramadhan Kailima.

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA UTALII ULAYA, KISHINDO CHAHAMIA MIJI YA LONDON NA MANCHESTER

 

Na Mwandishi wetu, London Uingereza.


Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake kwa uratibu taasisi ya Kili Fair inaendelea na  msafara wa kunadi vivutio vya utalii katika nchi za Ulaya Magharibi ulioanza tarehe 10- 15 machi 2025 ambapo wauzaji na wanunuzi katika sekta ya utalii wanakutana katika msafara huo wenye mawakala zaidi ya 30.


Msafara huo unaojulikana kwa jina la _"My Tanzania Roadshow 2025_ " tayari umenadi vivutio vya utalii katika miji ya Cologne Ujerumani, Antwerp Ubelgiji na Amsterdam Uholanzi ambapo kuanzia leo tarehe 13-15 Machi, 2025 msafara huo umehamia miji ya London na Manchester iliyopo nchini Uingereza kunadi vivutio vya Utalii katika soko hilo.

Akizungumzia Msafara huo, Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania Ernest Mwamwaja amesema, Wadau na wauzaji wa Mazao ya utalii ukihusisha vyama vya waendesha utalii, wamiliki wa hoteli, wenye kambi za kulala wageni, makampuni ya ndege kutoka Tanzania wanakutana  na wanunuzi wa Utalii (Buyers) wa bara la Ulaya kwa ajili ya kufanya biashara.


Mwamwaja ameeleza  kuwa Nchi za Ulaya magharibi zina idadi kubwa ya watalii wanaotembelea Tanzania ambapo takwimu za mwaka  2023  zinaonesha kuwa watalii kutoka Ujerumani ni takribani 100,000, Uingereza zaidi ya watalii 80, 000, Uholanzi watalii zaidi ya 37,000 na Ubelgiji zaidi ya watalii 17,000 wametembelea Tanzania huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka kuanzia mwaka huu.

Katika Nchi wa Uingereza Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchi humo Bw. Adam Mhagama  aliipongeza Kampuni ya Kili Fair kwa uratibu mzuri wa msafara wa kutangaza utalii katika nchi hiyo ambapo pia taasisi za Serikali zinatumia fursa hiyo kuelezea mazao mapya ya utalii yanayoibuliwa pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya utalii unaofanyika katika maeneo yenye vivutio ili kukidhi idadi kubwa ya wageni wanaoendelea kutembelea Tanzania 

Msafara huo unaoshirikisha kampuni za Sekta binafsi zaidi ya 30 unajumuisha pia taasisi za Serikali ambazo ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),  Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) na shirika za Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambazo ushiriki wao  unatoa hakikisho kwa sekta binafsi kuwa Serikali inawaunga mkono jitihada zao  kwa kuweka mazingira rafiki, kuboresha miundombinu na huduma za utalii kwa wageni wanaotembelea Tanzania.

Rais wa World Bank amshushia sifa Rais wa Tanzania Dr. SSH




Hiki hapa kinacho msibu Manila, Karibu Kusoma Kurasa za magazetini leo ijumaa 14.03.2025





























Thursday, March 13, 2025

RAIS MWINYI:WANANCHI ENDELEENI KUJIUNGA NA ZANZIBAR SUKUK

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali ametoa Rai kwa Wananchi Kuendelea kujiunga  na kuwekeza katika hatifungani ya Zanzibar SUKUK kwa ajili ya Kupata faida halali.


Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Wananchi katika Futari maalumu iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ) iliofanyika Hoteli ya Golden  Tulip Uwanja wa Ndege, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.


Aidha Rais Dkt, Mwinyi amesema kwa kufanya hivyo Serikali itapata fedha za Kuendeleza Miradi ya Maendeleo kwa kuwa na fedha za Uhakika na Wananchi Kupata faida halali.


Rais Dkt, Mwinyi amefahamisha kuwa tayari Serikali imelizingatia wazo la kuwekeza   katika Sukuk kwa Dola Hususan kwa Wazanzibar Wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) na sasa wanaweza kuwekeza  kwa  Dola.


Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza PBZ kwa Kuendelea kutoa huduma Bora za kibenki na kuifanya kuwa Benki inayoaminika na kutegemewa na  Wananchi.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ) Nd, Arafat Haji  amewahakikishia Wateja wa Benki Hiyo huduma Bora zinazokidhi Mahitaji Yao ya kibenki Ili kuendelea kuifanya Benki Hiyo kuwa kimbilio na Chaguo la Watu.

WANANCHI WA NGOMBO AMBAO BADO HAWAJALIPWA FIDIA ZAO WATAKIWA KUJITOKEZA KUCHUKUA STAHIKI ZAO



📍 TAWA yaagizwa kurejesha Hifadhi ya Kilombero katika uasili wake


Na Mwandishi wetu - Malinyi.


Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Wakili Sebastian Waryuba amewataka wananchi waliohama kwa hiyari kutoka katika Kijiji cha Ngombo ambacho awali  kilikuwa ndani ya Pori la Akiba Kilombero ambao bado hawajalipwa fidia zao wajitokeze na kufika katika Kata ya Biro kufanya uhakiki ili kulipwa stahiki zao kabla ya mwezi Juni 2025.


Akizungumza na waandishi wa habari Machi 13, 2025 wilayani humo Mhe. Wakili Sebastian Waryuba amesema Serikali ilitenga kiasi cha zaidi ya shillingi bilioni 6.9 Kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi hao huku akithibitisha kuwa zoezi la kulipa fidia hizo limekwenda vizuri    ambapo mpaka sasa Serikali imeshalipa jumla ya Kaya 998  Kati ya Kaya 1056  na kubaki Kaya 58 ambazo bado hazijalipwa, na  wanufaika wa makaburi 104 Kati ya 133  na kwa fedha zilizokwishalipwa mpaka sasa ni asilimia 97.66


"Sasa changamoto tunayoipata ni kwamba hao wanaotakiwa kulipwa hawapatikani kwa simu wala Kwa posta na hawaeleweki wako wapi. Sasa nitoe rai na wito Kwa wananchi wangu wa Ngombo ambao walistahili kulipwa fidia na hawapatikani wajitokeze waje katika Kijiji cha Biro watamkuta Mtendaji Kata atachukua takwimu na kumbukumbu zao zote ili uhakiki uendelee na waweze kulipwa, fedha za fidia za makazi na makaburi zipo, Rais Samia ameziachia zipo waje kuchukua" amesema Mhe. Sebastian.


Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewataka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kuendeleza Kasi ya kusafisha maeneo ya Pori la Akiba Kilombero hasa  kwenye maeneo waliyohama wananchi hao ili kurejesha uasilia wa Hifadhi hiyo ikiwemo kuondoa magofu/mahame yaliyoachwa hifadhini humo.


Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amewashukuru wananchi hao waliofanya maamuzi ya kuhama Kwa hiyari yao wenyewe ili kupisha shughuli za uhifadhi akitaja  kitendo hicho kuwa ni cha kizalendo kinachopaswa kupigiwa mfano.


Nao wananchi waliohamia vijiji jirani kutoka Kijiji cha Ngombo  wameishukuru Serikali Kwa kuwalipa fidia zao ambazo zimewawezesha kuanza maisha mapya na kuwahamasisha wenzao 58 ambao hawajajitokeza kuchukua fidia zao, kujitokeza ili kupata stahiki zao.


"Tumetoka Ngombo tumehamia Kijiji jirani, fidia yangu nimepata na michakato ya kuhama tumefika salama na wale wenzangu ambao hawajachukua pesa naomba waende kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Biro watapata pesa zao wasiwe na hofu" amesema Maganga Mkumba aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Ngombo ambaye sasa amehamia Kijiji cha Biro.

RC CHALAMILA AZINDUA OFISI YA MACHINGA-DSM

 

-Amshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutoa pesa zilizowezesha ujenzi wa ofisi hiyo.


-Awataka machinga na Bodaboda kuitumia ofisi hiyo kuleta matokeo chanya.


-Arudisha tabasamu la Bi Beatrice aliyekumbwa na sakata la kuuzwa nyumba yake


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 13, 2025 amezindua ofisi ya Machinga Mkoa ambayo imejengwa katika eneo la TBA, Kata ya Ndugumbi Magomeni Kota Wilaya ya Kinondoni.


Akifungua ofisi hiyo ya kisasa RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa ya ujenzi wa ofisi ya machinga na mradi mingine inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo ambapo amesema furaha ya Rais Samia ni kuona watanzania wanakuwa wanufaika chanya wa miradi hiyo ili kuwa na jamii yenye ustawi.


RC  Chalamila amesema ofisi aliyoizindua itatumiwa na machinga Mkoa pamoja na Bodaboda Mkoa ambapo ameyataka makundi hayo kuitumia ofisi hiyo vizuri ili kuweza kuleta matokeo chanya 


Naye Bi Zubeda Masoud akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Dkt Toba Nguvila amesema ujenzi wa ofisi hiyo ya machinga ni maagizo ya Rais Samia kuwa kila Mkoa uwe na ofisi ya Machinga ambapo alitoa pesa shilingi milioni 10 kupitia OR-TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo ambayo imezinduliwa leo.


Vilevile kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amemshukuru Rais Dkt Samia kwa ujenzi wa ofisi hiyo na kuahidi kama Wilaya kumalizia baadhi ya vitu vichache ikiwemo samani na kompyuta ili waweze kufanya kazi zao kisasa zaidi.


Hata hivyo viongozi wa Machinga na Bodaboda kwa nyakati  tofauti wamemshukuru Mhe Rais kwa kulitambua kundi hilo muhimu na wao wako bega kwa bega naye lakini ombi lao ofisi hizo zijengwe pia katika ngazi za Wilaya zote za Mkoa huo


Sambamba na hilo RC Chalamila amerudisha tabasamu kwa Bi Beatrice William ambaye amekumbwa na sakata la kuuzwa nyumba yake ambapo amemhakikishia ofisi yake kwa kushirikiana na TLS imeshaweka pingamizi la kimahakama hivyo nyumba hiyo haitauzwa kwa sasa pia ameongoza changizo kwa ajiri ya kumfariji mama huyo ambapo yeye binafsi ametoa milioni moja huku watu wengine wakijitokeza kwa wingi kumchangia.