JSON Variables

Monday, March 17, 2025

WAZIRI WA IRELAND AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI , ATEMBELEA DIT

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Ireland anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa, Maendeleo, na Diaspora, Mhe. Neale Richmond, amehitimisha ziara yake nchini kwa kutembelea Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT). 


Ziara hiyo imelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland katika nyanja za teknolojia na nishati endelevu.


Akiwa DIT, Mhe. Richmond alitembelea Maabara ya Ubunifu wa Ufanisi wa Nishati, inayofadhiliwa na Serikali ya Ireland kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) inayolenga kusaidia uvumbuzi wa teknolojia ya Nishati safi  ili kuchochea maendeleo endelevu na kuimarisha sekta ya nishati nchini.


Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Richmond alisifu ushirikiano uliopo na kusisitiza umuhimu wa teknolojia bunifu katika kukuza uchumi na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. 


Pia aliwatambua wanadiaspora kwa mchango wao katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia ujuzi wao wa kimataifa. 


Waziri huyo alithibitisha kuwa Ireland itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za nishati, elimu na teknolojia kwa maendeleo ya pande zote mbili.


Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alibainisha kuwa uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Ireland katika miradi ya teknolojia na nishati endelevu unatoa fursa kwa wanafunzi na watafiti wa Tanzania kupata ujuzi wa kisasa na kushiriki katika ubunifu wa suluhisho za kitaifa na kimataifa. 


Alisisitiza kuwa ushirikiano huu utaongeza tija katika sekta ya elimu na TEHAMA.


Mawaziri hao wamekubaliana kuendelea na mashauriano na kuweka mikakati madhubuti ya kuendeleza mifumo ya nishati endelevu, ambayo itachochea maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kiteknolojia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.


Waziri Richmond aliambatana na viongozi mbalimbali, akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, ambaye pia anawakilisha Ireland, Mhe. Mbelwa Kairuki, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme.


Mhe. Richmond alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku Tatu ambapo Alikutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe Balozi Mahmoud Thabit Kombo, alitembelea miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Ireland na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Dkt. Batilda Buriani na kutembelea Kitengo cha Saratani cha watoto cha Hospitali ya Taifa Muhimbili.

RAIS MWINYI:TUISHI KWA KUFUATA MISINGI YA UISLAMU


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu  Kuishi kwa kuifuata Miongozo ya  Uislamu pamoja na kufungamana na Ibada.


Rais Dkt.Mwinyi  amesema hayo alipozungumza katika Mashindano ya Tajwiid Quraan yalioandaliwa na Taasisi ya AlHikma Quraan Foundation yàliofanyika Masjid Jamiu Zenjibar Mazizini Wilaya ya Mjini.


Aidha Rais Dkt, Mwinyi amesema Kazi kubwa inayofanywa na Masheikh na Walimu wa Madarasa ya kuwasomesha Vijana na Kuwa na Uwezo wa Kuhifadhi Quraan inapaswa kuungwa Mkono na kila Mmoja .

Amewanasihi Waislamu kushughulika na Miongozo ya Dini hiyo  ili Wapate kuongoka kwani Quraan ni kitabu cha Uongofu.


Rais Dkt, Mwinyi amewahimiza Waislamu kuzidisha bidii ya  kuisoma Quraan na Kuwasimamia Watoto kuwa na Mwenendo Mzuri unaonekana  wakati wa Mwezi wa Ramadhani .

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza Wadhamini wanaoendelea  kuyafadhili Mashindano hayo kila Mwaka na  kuwaomba wengine wapya kujitokeza kuunga Mkono Juhudi hizo.

Saturday, March 15, 2025

KUELEKEA SIKU YA MISITU DUNIANI, MITI 25O YAPANDWA MAKETE.

................

Na Mwandishi Wetu - Njombe

Wananchi Wilayani Makete Mkoani Njombe, wametakiwa kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji kwa kupanda Miti rafiki kwenye maeneo yao ili iweze kuwasaidia katika Uhifadhi wa rasilimali za Misitu kwa kizazi hiki na kijacho

Wito huo imetolewa leo Machi 15, 2025 Mkoani Njombe na Bw. Agustino Ngajilo, Afisa Tarafa ya Lupalilio, katika siku ya pili ya upandaji wa miti kitaifa katika Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Njombe ambapo amesema hatua hiyo itasaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uhifadhi ya rasilimali zilizopo

"Niwasihi wananchi wenzangu kuacha tabia ya kuchoma moto hivyo misitu kwakuwa hupekeka uharibufu mkubwa wa mazingira na kupelekea hasara kwa wananchi na serikali kwa ujumla" Amesema Ngajilo

Naye, Afisa Misitu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Emmanuel Msoffe, amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Makete kwa kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi, huku akiwataka kuitunza miti ya asili kwa ajili ya uhumilivu wa mazingira.

"Nachukua fursa hii kuwapongeza wananchi kwa kuamua kuacha kazi zenu na kuungana nasi katika zoezi hili la Upandaji Miti katika Wilaya yenu, sisi kama wawakilishi wa Wizara tutaendelea kuwa na nyinyi kupitia kampeni hii ya utunzaji Miti na uhifadhi wa Misitu kwa kuwa ndio maono ya kiongozi wetu wa nchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uhifadhi wa Misitu hapa nchini"Amesema Bw. Msoffe

Kwa Upande wake, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bi. Upendo Mgaya, ametoa rai kwa wananchi wa Wilaya hiyo, kuitunza miti hiyo na kuacha kupanda miti isiyo rafiki na Mazingira kwenye vyanzo vya maji sambamba na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo

Jumla ya Miche ya parachichi 100 na miti ya mapambo 150 jumla ikiwa miti 250 imepandwa katika shule hiyo kupitia zoezi hilo likihudhuriwa na wataalamu kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

Itakumbukwa Machi 21, kila mwaka Tanzania huungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Misitu Duniani na siku ya Upandaji Miti kitaifa ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika Mkoani Njombe

 

ELIMU YA FEDHA KUWAFIKIA WANANCHI WOTE IFIKAPO MWAKA 2O26


Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizaya ya Fedha, Bw. Santley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha  kwa Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Musoma, mafunzo ya elimu ya fedha yalitolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, mkoani Mara.

Afisa Msimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mzava, akigawa kipeperushi chenye taarifa kuhusu uwekaji akiba kwa Bw. Zakayo Emmanuel, mkazi wa Busekera, mkoani Mara, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Musoma, Bi. Jacqueline Wanzagi, akimkabidhi zawadi ya fulana, Bi. Ester Tingali, baada ya kujibu swali kuhusu umuhimu wa kusoma mkataba kabla ya kusaini kuchukua mkopo, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC mkoani Mara.
Baadhi ya watumishi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) wakifuatilia mafunzo ya  elimu ya fedha yaliyotolewa kwa Wananchi mkoani Mara, na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), NMB, CRDB, NBC  na Benki hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Benki ya CRDB, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa Wananchi mkoani Mara, na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, NBC na CRDB.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakisoma vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, mkoani Mara.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji cha  Busekera, wakifuatilia elimu iliyotolewa na  Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Busekera, mkoani Mara.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Mara)
Na. Josephine Majura WF, Mara.
 
Wizara ya Fedha  inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi yote ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2930.
 
Hadi sasa Wizara ya Fedha imetoa elimu ya fedha katika mikoa 15, ikiwemo mkoa wa Kagera, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Pwani, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mtwara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mara.
 
Katika zoezi la utoaji elimu ya fedha Wizara ya Fedha, imeambatana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC.

TANZANIA YAHITIMISHA MSAFARA WA KUTANGAZA UTALII BARA LA ULAYA KWA MAFANIKIO MAKUBWA


Na Mwandishi Wetu, Manchester.


Kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii kupitia Msafara wa mawakala 30 wa utalii katika bara la Ulaya ijulikanayo kama "My Tanzania Roadshow 2025' imehitimishwa tarehe 14 Machi 2025 katika Jijini Manchester nchini Uingereza.


Kampeni hiyo iliyojumuisha  miji mitano iliyoko nchi nne za Ulaya ambayo ni Cologne (Ujerumani), Antwerp (Ubelgiji), Amsterdam (Uholanzi), London na Manchester (nchini Uingereza) imekuwa na mafanikio makubwa ambapo waandaaji wamefanikiwa kuvuka lengo la kuvutia Wakala au Wanunuzi wa Utalii kutoka Tanzania ambapo katika miji hiyo mitano  zaidi ya Mawakala 240 wa nchi za Ulaya walihudhuria mikutano ya kibiashara baina yao na Wakala wa Utalii 30 kutoka Tanzania.


Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Ernest  Mwamwaja ameeleza kuwa katika kila mji mikutano hiyo imetoa fursa kwa Wakala wa Utalii wa Ulaya kupata taarifa za kutosha toka kwa taasisi za uhifadhi zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo ni TTB, NCAA na  TANAPA.


Ushiriki wa taasisi hizi umesaidia kutoa taarifa ya vivutio vilivyopo na kuelezea uboreshaji wa miundombinu ya utalii, mikakati ya Serikali ya utangazaji utalii, mwenendo wa utalii, juhudi za Serikali kuongeza mazao ya utalii, ubora wa huduma, na fursa za uwekezaji zilipo katika sekta ya utalii.


Mawakala wa Utalii kutoka Tanzania wameeleza kuridhishwa na kiwango cha ueledi katika maandalizi ya kampeni hiyo na ubora wa Wakala wanunuzi walioalikwa kukutana na Wakala toka Tanzania na kupanua soko la kupata wateja wa bara la ulaya.


Katika hatua nyingine, Bw. Mwamwaja amezishukuru ofisi za balozi za Tanzania katika nchi ya Ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi, na Uingereza kwa kuwa chachu ya mafanikio ya Kampeni hiyo na kuwataka Wakala walioko Tanzania kuendelea kuhudhuria midafara hiyo kila mwaka kuchangamkia fursa zinazoletwa na Serikali pamoja na sekta binafsi katika kuitangaza Tanzania katika masoko ya ndani na ya kimataifa. 


Akihitimisha msafara huo Bw. Mwamwaja amemshukuru kipekee Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maono na juhudi zake binafsi za kutangaza Tanzania katika masoko ya kimkakati ya kimataifa.


Msafara kutangaza Utalii wa Tanzania My Roadshow 2025 umeratibiwa na Kampuni ya KiliFair ambapo ulianza tarehe 9- 14 Machi, 2025.

Habari kubwa za leo magazetini jumamosi 15.03.2025

Wasira aonya wanataka wanaotaka kuharibu Amani na Umoja, Simba na Yanga kazi iendelee, Mkemia aongeza ufanisi Bandarini.














 

Friday, March 14, 2025

RAIS MWINYI:TUDUMISHE AMANI KWA MAENDELEO ZAIDI.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea Nchi Amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na Viongozi Wakuu wa Nchi .



Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya Kujumuika katika Sala ya Ijumaa, Msikiti wa Ijumaa Mpapa Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 14 Machi 2025.


Amefahamisha kuwa Maendeleo yanayofikiwa hivi sasa hapa nchini yanatokana na kuwepo kwa Amani na kuahidi kuendeleza Juhudi za kuleta Maendeleo Zaidi.


Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewahakishia Wananchi wa Mpapa kuwa Serikali itazifanyia  Kazi Changamoto za Kijamii ziliomo katika kijiji  hicho .


Changamoto hizo zilizobainishwa na Wananchi ni Uchakavu wa Barabara za ndani , Ukosefu wa Uzio katika Skuli ya Mpapa na Ukosefu wa huduma za Karibu za Afya  kutokana na kutomalizika kwa Kituo cha Afya kiliopo kwa Miaka mingi ambacho kimejengwa kwa nguvu za Wananchi.


Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amewahakikishia kuwa Serikali itamaliza Changamoto hizo   alizoziielezea kuwa ni za  Muhimu.

SERIKALI: TUMIENI MIKOPO KUWEKEZA KWENYE BIASHARA ZINAZOZALISHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoan Mara, Bw. Msongela Palela, akisoma kipeperushi alichokabidhiwa na Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizaya ya Fedha Bw. Santley Kibakaya, chenye mada kuhusu uwekezaji ikiwa ni moja ya mada ambayo itafunzishwa wakati wa utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Bw. Msongela Palela, akizungumza na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha iliyofika mkoani Mara kwa lengo la kutoa elimu ya fedha katika maeneo mbalimbali mkoani humo. Kushoto ni Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mzava na kulia ni Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizaya ya Fedha Bw. Santley Kibakaya na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Bi. Angela Mollel.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Bw. Msongela Palela, akizungumza na Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani Mara.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Bi. Angela Mollel (kushoto) na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Suguti, Bw. Joel Samson, wakimkabidhi fulana mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Suguti, Alex Baraka, baada ya kujibu swali kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki  ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari  Suguti mkoani Mara.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji cha Suguti wakifuatilia elimu iliyotolewa na  Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanznaia (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Suguti, Musoma, mkoani Mara.

Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mzava, akitoa elimu ya fedha kwa wakazi wa Kijiji cha Suguti, elimu ya fedha inatolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanznaia (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Suguti, Musoma, mkoani Mara.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Mara).

............................

Na. Josephine Majura WF, Mara

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, Bw. Msongela Palela, amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutumia mikopo wanayokopa kufanya uwekezaji unaozalisha faida  ili kuepuka kushindwa kufanya marejesho ya mkopo.

 

Bw. Palela alitoa rai hiyo wakati alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Taasisi za Serikali na Binafsi ambayo ipo mkoani Mara kutoa elimu ya fedha  kwa makundi mbalimbali.

 

"Kwenye Wilaya yetu kumekuwa na changamoto kwa wananchi wetu kuchukua mikopo na hawaendi kuwekeza kwenye maeneo ambayo yatazalisha faida ili watumie faida ile kufanya marejesho”, alisema Bw. Palela.

 

Aliongeza kuwa wananchi kukopa sio jambo baya lakini alitarajia mikopo hiyo iwasaidie lakini imekua tofauti kwa sababu haiendi kutumiwa katika shughuli za uzalishaji hivyo wanashindwa kufanya marejesho.

 

Bw. Palale alifafanua kuwa elimu ya fedha ni muhimu hivyo ni vyema Wizara ya Fedha ikahakikisha inawafikia wananchi wote na elimu hiyo iwe endelevu kwakuwa ina mchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi endapo itaeleweka kwa wananchi wote.

 

Aidha, alizitaka Taasisi za Fedha zinazojihusisha na utoaji mikopo, kufuata utaratibu na Sheria zilizowekwa na Serikali ili mikopo wanayotoa kwa wananchi iwasaidie na isiwe chanzo cha kuongeza tatizo  kwa kuweka riba kubwa zisizolipika kwa urahisi.

 

"Naendelea kuwaomba watoa huduma za fedha kuwa waaminifu na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania za kuwalinda watoa huduma na wateja.

 

Vilevile, aliwataka Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kujenga utaratibu wa kutumia Taasisi rasmi zinazotambuliwa na Serikali wanapohitaji mikopo, ili kuepuka udhalilishaji unaofanywa na Taasisi ambazo haziko rasmi na hazifuati utaratibu.

 

Bw. Palela aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuendelea kuwachukulia hatua watoa huduma wanaofanya biashara kinyume na utaratibu unavyoelekeza.

 

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bw. Mbagira Kajanja, aliishukuru Serikali kwa kuwapatia elimu ya fedha ambapo alieleza kupitia elimu hiyo imewafumbua macho na kuelewa baadhi ya taratibu ikiwemo kuwa na haki ya kusoma mkataba kabla ya kuchukua mkopo na kuelewa masharti ya mkopo na kujua viwango vya riba.

 

“Naamini baada ya elimu hii, tutabadilika na kutumia Taasisi rasmi zinazotambulika na Serikal, tutasoma mkataba kwa makini na kama hatujaelewa tutaomba tuelimishwe kabla ya kusaini”, alisema Bw. Kajanja.

 

Kwa upande wake Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizaya ya Fedha Bw. Santley Kibakaya, alisema kuwa Wizara inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2930.

 

Alisema kuwa hadi sasa Wizara ya Fedha imetoa elimu ya fedha katika mikoa 15, ikiwemo mkoa wa Kagera, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Pwani, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mtwara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mara.

 

Lengo la Wizara ni kwamba hadi kufikia mwaka 2025/2026 mikoa yote 26 ya Tanzania iwe imepata elimu ya fedha.