JSON Variables

Wednesday, March 19, 2025

WAKOPAJI WAASWA KUTOTUMIA MALI ZA FAMILIA KAMA DHAMANA YA MIKOPO BILA RIDHAA

Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, akitoa mafunzo ya elimu ya fedha  kwa wakazi wa wilaya ya Butiama, mkoani Mara, yaliyotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CRDB, TCB, NMB na NBC.

Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akitoa elimu ya fedha kupitia vipeperushi vyenye mada mbalimbali ikiwemo akiba, uwekezaji, mikopo walizofundishwa wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha  kwa baaadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha  wilayani Butiama, mkoani Mara, yaliyotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CRDB, TCB, NMB na NBC.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji Kyankoma, Kata ya Nyamimange, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha yenye mada mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo, akiba na uwekezaji yaliyotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CRDB, TCB, NMB na NBC.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, Bw. Zakaria Wambura, akiuliza swali namna ya kuitambua Taasisi iliyosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania  (BoT), wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali mkoani Mara, ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CRDB, TCB, NMB na NBC.

Afisa Mikopo wa Benki ya CRDB, Bw. Calvin Temba,  akieleza mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo kwa wananchi walioshiriki mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali mkoani Mara, ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CRDB, TCB, NMB na NBC. 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Butiama Mara).

..................

Na. Josephine Majura, WF, Mara.

 

Wakopaji wametakiwa kutojihusisha na matumizi ya dhamana za mali za familia bila ridhaa ya familia husika ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea iwapo mali hizo zitapotezwa kutokana na kushindwa kulipa mikopo.

 

Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa wananchi wa Kijiji cha Kyankoma, Wilaya ya Butiama mkoani Mara na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki, ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC.


“Wakopaji wanatakiwa kuwa waangalifu na kuhakikisha wanaelewa masharti ya mikataba ya mikopo kabla ya kutumia mali ya familia kama dhamana ili kuhakikisha kuwa dhamana zinazotolewa hazihatarishi ustawi wa familia” alisema Bw. Myonga.


Aliongeza  kuwa Taasisi za kifedha zinatakiwa kuwa waangalifu na kufuata sheria na taratibu stahiki kabla ya kukubali mali ya familia kuwekwa kama dhamana, kwa kuhakikisha kuwa hati zote muhimu, kama vile hati za umiliki na ridhaa za maandishi za familia husika vinaambatishwa.


Akizungumzia kuhusu udhamini wa mkopo, Bw. Myonga, waliwashauri wananchi kabla ya kukubali kuwa wadhamini, wahakikishe wamejiridhisha kuwa mkopaji ana uwezo wa kulipa mkopo kwa wakati.


Alifafanua kuwa mtu akiwa mdhamini, anakuwa na wajibu wa kulipa mkopo wote endapo mkopaji atashindwa kulipa jambo ambalo linaweza kuathiri mali zake binafsi na hali yake ya kifedha.


Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Bi. Rebeca Sanga, aliwasisitiza wanavikundi wote nchini kusimamia vizuri miradi waliyonayo ili izalishe faida kwa ajili ya manufaa ya kundi na mtu mmoja mmoja.


Aliongeza kuwa miradi ya kikundi ikisimamiwa vizuri itazalisha faida ambayo inaweza kutumika kama mtaji wa kukopeshana wanakikundi na kujiepusha na mikopo yenye riba kubwa.


Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha Bw. Bryan Mkurya, aliiomba Serikali kuendelea kutoa elimu hiyo katika ngazi zote kuanzia Kitongoji hadi Kata ili kuhakikisha kila mwananachi anapata elimu ya fedha.


Aliongeza kuwa Serikali ihakikishe inatoa elimu kwa mkopaji na mkopeshaji ili wote wawe na uelewa wa pamoja ili  kupunguza migogoro inayoendelea nchini.


Bw. Mkurya aliishauri Serikali kutumia mikusanyiko mbalimbali kutoa elimu ya fedha ikiwemo nyumba za ibada na mikusanyiko mingine inayotambulika na Serikali ili iweze kuwafikia wananchi wengi kwa mara moja

 

Tuesday, March 18, 2025

TMDA YATANGAZA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI

....................

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imetangaza msimu wa Tuzo ya Waandishi wa Habari walioripoti taarifa  na kuandaa makala mbalimbali kuhusu kazi na majukumu ya TMDA katika kipindi cha mwaka 2025.

Kazi hizo ni zile zilizotoka kuanzia Julai, 2024 mpaka Machi 2025.

Taarifa ya Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne, Machi 18, 2025 imesema kuwa lengo la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa waandishi wa habari na kuleta hamasa katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya udhubiti wa Dawa na Vifaa Tiba,  Vitendanishi na bidhaa za Tumbaku kupitia vyombo vya habari ili kulinda afya ya jamii. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  kazi zitakazolengwa ni zile zilizoripotiwa kupitia Runinga, Radio, Magazeti na Mitandao ya Kijamii kwa kipindi tajwa. 

"TMDA inawaalika waandishi wote wa habari kushiriki Tuzo hizi  kwa kuwasilisha kazi zao ifikapo au kabla kabla ya Aprili 18,  2025 kupitia anuani ya barua pepe ya commpedtmda@gmail.com au kwa njia ya CD katika ofisi za  TMDA zilizopo Dodoma, Dar es Salaam,  Mwanza, Arusha,  Mbeya,  Mtwara, Tabora  na Geita.


WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA MISITU DUNIANI

 


..........................

Na Happiness Shayo-Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani itakayoenda sambamba na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa itakayofanyika Machi 21, 2025 Mkoani Njombe.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) katika kikao na Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizo chini ya Wizara kilichofanyika leo Machi 18,2025 Mtumba jijini Dodoma.

“Maadhimisho ya mwaka huu yana lengo la kuhimiza, kuelimisha na kuhamasisha Watanzania juu ya umuhimu wa kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu nchini. Kauli Mbiu ya mwaka huu ni ‘‘Ongeza Thamani ya Mazao ya Misitu kwa Uendelevu wa Rasilimali kwa Kizazi Hiki na Kijacho’’ na Mgeni Rasmi wakati wa kilele atakuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “ Mhe. Chana amesisitiza.

Mhe. Chana ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo na maono yake katika kuendeleza masuala ya misitu na uhifadhi hasa katika utalii.

“Katika uongozi wa Rais Samia tumeshuhudia sekta ya misitu ikiendelea kuimarika siku hadi siku hivyo ni wajibu wetu Watanzania kuhakikisha kwamba tunalinda misitu yetu isipate uharibifu wa aina yoyote” Mhe. Chana amesema.

Amefafanua kuwa Maadhimisho hayo yatahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo zoezi la upandaji miti katika Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe, maonesho ya bidhaa na huduma za misitu, midahalo itakayohusisha wataalam na wadau wa misitu, maonesho ya vivutio mbalimbali vya kitalii ikiwemo Wanyamapori hai kama Simba na wanyama wengine.

Maadhimisho hayo yanafanyika kwa kuzingatia maazimio yaliyotolewa na Bazara Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2012.

   

TOENI MAFUNZO YANAYOZINGATIA SOKO LA AJIRA-MAJALIWA


......................

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini watoe mafunzo yanayozingatia mahitaji halisi ya soko la ajira.


“Mahitaji ya soko la ajira tutayajua kwa kufanya tafiti za mara kwa mara kwa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, na mashirika ya kimataifa.”


Ametoa wito huo leo (Jumanne, Machi 18, 2025) katika Maadhimisho ya miaka 30 ya Uanzishwaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.


Amesema katika zama hizi zenye kasi ya maendeleo ya teknolojia, ni muhimu kwa VETA kuendelea kujiimarisha kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia duniani.


“Toeni mafunzo ya ufundi stadi yanayoendana na mabadiliko ya teknolojia, mafunzo hayo yajumuishe ujuzi wa teknolojia za kisasa zinazochochea uzalishaji wenye tija.”


Akizungumza kuhusu umuhimu wa Elimu ya Ufundi Stadi, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa takwimu za Shirika la Kazi Duniani (ILO) zinaonesha kuwa takribani asilimia 70 ya ajira zote ni ajira binafsi na kwa watu wenye elimu ya ufundi stadi hasa kwenye sekta za kilimo, ujenzi, usafirishaji, na huduma za kijamii.


“Kwa upande wa nchi yetu, takwimu za ajira zilizozalishwa kati ya mwaka 2020 na 2024 zinafikia Milioni 7 ambapo ajira binafsi katika sekta isiyo rasmi imeajiri watu milioni 6.1 sawa na asilimia 87.1 ambapo wengi wao wana elimu ya ufundi stadi, na sekta rasmi imeajiri watu 907,873 (asilimia 12.9) ambapo wengi wao ni wale wenye elimu ya juu”.


Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Wizara ya Viwanda na Biashara wahakikishe ujenzi wa vyuo 65 vya ufundi unakamilika haraka.


Waziri Mkuu amesema ukamilishwaji wa vyuo hivyo vinavyojengwa na Serikali unalenga kutimiza dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwawezesha Watanzania kiujuzi.


“Ujenzi wa vyuo hivi ukikamilika, VETA itakuwa na vyuo 145 katika ngazi ya Mikoa yote 26 na Wilaya zote nchini. Vilevile, katika vyuo 80 vilivyopo, vyuo 30 vilikamilishwa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita (6). Tuna kila sababu ya kumpongeza Rais wetu kwa kazi kubwa anayowafanyia Watanzania.”


Kadhalika Waziri Mkuu ameitaka VETA ihakikishe inatangaza fursa za mafunzo zilizopo ili vijana haswa wa vijijini waweze kuzitumia. “Inawezekana kabisa kuwa, wapo vijana katika maeneo mbalimbali nchini haswa ya vijijini ambao hawana taarifa ya fursa za mafunzo zilizopo.”



MBUNGE WA KIBAMBA MTEMVU AJINDIKISHA KUBORESHA TAARIFA ZAKE

*****

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Jimbo la Kibamba, Wilayani Ubungo, Dar es Salaam, Issa Jumanne Mtemvu amejitokeza Katika Kituo cha Kibwegere Shule, Mtaa wa Kibwegere Kata ya Kibamba mkoani Dar es Salaam kŵa ajili ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zake katika Daftari la kudumu la Mpiga kura ili aweze kupata fursa ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi

Hili linakwenda sambama na kuandikisha wapigakura wapya lakini linalenga kuboresha pia taarifa za wapiga kura wa zamani wakiwemo wale waliopoteza kadi zao .

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema uandikishwaji huo utafanyika kwa siku saba umeanza jana Machi 17 na utakamilika Machi 23, 2025.

Amesema uandikishwaji huo unawahusu waliotimiza miaka 18, pia wale waliopoteza kadi zao ama kuharibika watapatiwa nyingine.




 

UFAFANUZI KUHUSU KUPOTEA KWA GIPSON


 *****

Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa katika Mitaandao na picha mjongeo ikimwonesha mwananchi mmoja aitwae Mercy Daniel Mkazi wa Arusha ambaye ameeleza kupotea kwa mmewake aitwae David Gipson Mkazi wa Arusha huku likiweka Wazi kuwa Mtu huyo ashirikiwi na Jeshi hilo.

Akitoa taarifa hiyo leo Machi 18,2025 kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo amesema kuwa Jeshi hilo limepokea taarifa hiyo na uchunguzi wa shauri hilo unaendelea, katika ufuatiliji huku akibainisha kuwa uchunguzi wa awali ukibaini kuwa David Gipson amehusishwa na upotevu wa fedha uliotokea katika benki moja hapa jijini Arusha jina akisema jina wanalihifadhi.

SACP Masejo ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na ufuatiliaji wa shauri hilo ili kubaini mtu huyo yuko wapi na taarifa kamili itatolewa.

Akatoa wito kwa wananchi kusaidia Jeshi la Polisi kutoa taarifa za mtu huyo popote atakapoonekana. Pia kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Mkoa wetu uendelee kuwa shwari.

KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MRADI WA MAZINGIRA KATAVI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu za Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea na kukagua Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi tarehe 17 Machi, 2025. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis).

....

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imewahimiza wasimamizi wa miradi ya kuhifadhi mazingira ngazi ya Halmashauri za Wilaya kuisimamia miradi hiyo kwa ukaribu ili ilete tija kwa wananchi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi tarehe 17 Machi, 2025.

Mhe. Kiswaga ameongoza kamati hiyo kukagua miradi inayotekelezwa kupitia mradi wa SLR ambayo ni josho, banio, birika itakayosaidia kuogesha, kunyweshea na kutibu mifugo, pia mradi wa ng’ombe wa maziwa waliotolewa kwa kikundi ili kusaidia wananchi kuachana na shughuli za uharibifu wa mazingira na mradi wa shamba darasa la malisho lenye ukubwa wa ekari 2.5, miradi iliyopo katika Kijiji cha Kapanga yote ikiwa na thamani ya shilingi milioni 81.

Amesema Serikali Kuu inapeleka fedha katika halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi hivyo wasimamizi wa miradi ngazi ya chini wanapaswa kuisimamia ili ikamilike kwa wakati uliopangwa na kunufaisha wananchi sanjari na kulinda mazingira.

“Ndugu zangu miradi hii ni ya kwenu wananchi,m Ofisi ya Makamu wa Rais inahakikisha fedha za utekelezaji zinawafikia na hivyo ninyi watu wa Halmashauri hadi ngazi ya vijiji mnalo jukumu la kufuatilia utekelezaji wake kuhakikisha inaendana na thamani ya fedha zilizotengwa,“ amesisitiza Mhe. Kiswaga. 

Mhe. Kiswaga ambaye pia ni Mbunge wa Kalenga ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuratibiwa miradi ambayo inasaidia katika kuhifadhi mazingira na kusema ni muhimu elimu iendelee kutolewa kwa wananchi sanjari na uwepo wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewahimiza wasimamizi wa miradi ngazi za wilaya kukamilisha miradi kwa wakati uliopangwa ili wananchi waweze kunufaika.

Amesema malengo ya miradi hii ni kuwabadilisha wananchi kutoka kwenye shughuli za uharibifu wa mazingira hivyo wanapopelekewa miradi na kukamilishiwa kwa wakati wataachana na shughuli za uharibifu wa mazingira.

Aidha, Naibu Waziri Khamis ametoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri wa kusimamia fedha kwa ukamilifu walizopokea kutoka Serikali Kuu katika kutekeleza miradi iliyokusudiwa ili matokeo yaonekane na kuomba zingine kama kuna uhitaji.

Awali akiwasilisha taarifa za miradi iliyotembelewa na kamati, Mratibu wa Mradi wa LSR Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw. Ephraim Luhwago ameishukuru Serikali kwa kuiwezesha halmashauri kupata mradi huo ambao una manufaa makubwa kwa wananchi.

Amesema kjuwa lengo kuu la mradi ni kuimarisha usimamizi wa pamoja wa ardhi iliyoharibiwa ili kujenga uhimilivu wa mifumo ikolojia na jamii kwa ujumla.

Viongozi walioambatana na kamati katika ziara hiyo ni hiyo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme na Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mradi wa SLR wenye thamani ya sh. bilioni 25.8 unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) kupitia Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais unatekelezwa Halmashauri za wilaya za Tanganyika na Mpimbwe (Katavi), Iringa (Iringa), Mbeya, Mbarali (Mbeya) na Sumbawanga (Rukwa).

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu za Bunge ya Maji na Mazingira wakipata maelezo kuhusu mradi wa josho, banio na birika katika Kijiji cha Kapanga unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi tarehe 17 Machi, 2025.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu za Bunge ya Maji na Mazingira wakipata maelezo kuhusu mradi wa shamba darasa la malisho maziwa katika Kijiji cha Kapanga unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi tarehe 17 Machi, 2025.

DC KAEGELE AWATAKA WANANCHI WA BUTIAMA KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA FEDHA

Mkuu wa Wilaya ya Butiama,  mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akikabidhiwa kipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, chenye mada mbalimbali ikiwemo mikopo na akiba ambazo zitafundishwa kwa wananchi wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama,  mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke, akikabidhiwa kipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, chenye mada mbalimbali ikiwemo mikopo na akiba ambazo zitafundishwa kwa wananchi wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe. Moses Kaegele, akiteta jambo na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Kutoka kushoto ni Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama,  mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Kutoka kulia ni Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji Kyankoma, Kata ya Nyamimange, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, wakiangalia filamu  yenye mada mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo, akiba na uwekezaji wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mara. 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Butiama Mara)

......................

Na. Josephine Majura, WF, Butiama Mara

Serikali imewataka Wananchi wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo ya elimu ya fedha ili kujiongezea maarifa yatakayowasaidia kusimamia vizuri rasilimali zao.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambayo ipo mkoani Mara kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali.

“Kushiriki katika mafunzo haya kutawawezesha wananchi kuepuka changamoto za kifedha kama vile madeni yasiyolipika, matumizi mabaya ya fedha, na kutokuwa na akiba ya kutosha kwa dharura,”, alisema Mhe. Kaegele.

Aliongeza kuwa wananchi wakijitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo ya elimu ya fedha kutawasaidia kupata maarifa yatakayowawezesha kufanya maamuzi bora ya kifedha na kujenga maisha yenye utulivu na mafanikio.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke Makanyanga, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na elimu muhimu ya fedha ili waweze kusimamia vizuri fedha zao.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, alisema kuwa wakati wanaendelea na zoezi la utoaji elimu katika makundi mbalimbali wamekutana na malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wamekopa maeneo mbalimbali kubadilishiwa mikataba na watoa huduma wasiowaminifu. 

“Tumekutana na kesi mwananchi anasema kwenye mkataba aliosaini siku ya kwanza alikopa kiasi fulani, lakini anaporudi ofisini kutaka kuanza kufanya rejesho la kwanza anakuta mkataba mpya wenye kiwango kikubwa tofauti na alichokopa” alisema Bi. Elizabeth. 

Alifananua kuwa ni haki ya mkopaji kuomba nakala ya mkataba wa mkopo ili utumike kama ushahidi iwapo kutatokea kubadilishiwa kiwango cha mkopo, lakini nakala hiyo itamsaidia mkopaji kujua taarifa muhimu ya kiwango cha riba, kiasi cha rejesho kila mwezi na kiasi cha mkopo alichokopa.

MWSIHO.