JSON Variables

Friday, April 4, 2025

DKT. NCHIMBI ATUMIA LUGHA LAINI SANA KUJIBU ‘NO REFORM NO ELECTION’ YA CHADEMA

*Asema CCM inauwaunga mkono wakiamua kususia uchaguzi mkuu

*Asisitiza ni kosa kukilazimisha chama cha siasa kushiriki uchaguzi

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Emmanuel Nchimbi ameweka wazi hakuna sababu ya kuilazimisha CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwani vyovyote watakavyoamua iwe kushiriki au kutoshiriki ni sawa.

Amesema ni kosa kubwa kukilazimisha chama cha siasa kushiriki uchaguzi huku akibainisha hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kuzuia Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) unaofanyika Songea Mjini mkoani Ruvuma leo, Dk.Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuzungumzia ya kauli mbiu ya ‘No Reforms No Election’ ya CHADEMA ambayo lengo lake ni kuzuia uchaguzi mkuu mwaka huu.

Akitumia sauti ya upole iliyokuwa ikipenya katika masikio ya kila mhariri aliyekuwepo katika mkutano huo, Dk.Nchimbi amesema nchi yetu inautaratibu wa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.

“Tumekuwa tukifanya hivyo tangu mwaka 1961 ,kila baada ya miaka mitano Uchaguzi Mkuu. Ukifika mwaka wa uchaguzi mkuu hakuna raia yeyote anayeweza kuzuia uchaguzi

“Hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi, hata Makamu wa Rais hawezi, Waziri Mkuu hawezi kulitamkia Taifa kuzuia uchaguzi mkuu.

“Kwasababu hilo ni takwa la kikatiba ,ninataka niwahakikishie sio wahariri bali Watanzania wote kuwa uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais mwaka 2025 utafanyika.”

Dk.Nchimbi pia amesema pamoja na haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni kosa kubwa kukilazimisha chama kingine cha siasa kuingia kwenye uchaguzi.

Amesisitiza ameanza kusikia taarifa za baahi ya wananchi na wengine wana CCM wakishinikiza CHADEMA iingie kwenye Uchaguzi Mkuu.

“Ni haki  yao kususia na uchaguzi huu sio wa mwisho, nataka niwape salamu zao CHADEMA yupo rafiki yangu pale Tundu Lissu watu wasiowaonee bure uchaguzi huu sio wa mwisho…

“Kuna uchaguzi mkuu mwingine mwaka 2025, 2030,2035,2040,2045, 2050 na kuendelea…wakikosa kufanya uchaguzi huu iko miaka mingine ya uchaguzi. Mtu yeyote asiwalazimishe ni haki yao kugomea.

“Kwa mujibu wa Katiba yetu hata chama kikiwa kimoja kinagombea wananchi watapiga kura ya ndio au hapana. Kuwasema sema CHADEMA sio sawa.

“Kwa hiyo namwambia rafiki yangu Tundu Lissu anahaki ya kuzuia chama chake kutogombea na tutawaunga mkono vyovyote watakavyoamua.

“Kugombea na kutogombea vyote ni sawa, ni haki yao. Hata hivyo kama watagomea wasisahau kura zao au sio… ndio jadi yetu kwani ukikosa haki ya kuchaguliwa usipoteze haki ya kuchagua.

“Angalau katika hizo haki mbili hakikisha unaipata mojawapo. Ukishindwa kuchaguliwa basi chagua. Unakuwa umetutendea haki na ninaamini rafiki yangu Tundu Lissu na wenzake haki ya kuchagua wataitumia vizuri,” amesema Dk.Nchimbi.

Wakati Dk.Nchimbi akieleza hayo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu jana amefanya kikao na waachama wa Chama hicho katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam na kutoa msimamo wake kuwa bila mabadiliko hakuna uchaguzi na katika hilo hatanii.

Akatoa maelezo kwa wana CHADEMA kuwa wale ambao hawako tayari kufuata msimamo huo milango iko wazi maana hakuna atakayeshikiwa bunduki kulazimishwa ‘No Reform No election’.  

Thursday, April 3, 2025

KAMATI YA PAC YARIDHISHWA UJENZI BWAWA LA MEMBE

NIRC Dodoma.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi mradi wa bwawa la Umwagiliaji Membe lililopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Kamati hiyo imesema, ujenzi wa bwawa umeendana na thamani ya fedha iliyowekwa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo katika mradi wa wa bwawa la Membe Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka, amesema kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi huo kwani thamani ya fedha unaendana na ujenzi.

“Si tu kujenga bwawa bali ni kuhakikisha bwawa hilo linatumika katika shughuli zote za Umwagiliaji wa mashamba na kuleta tija katika kilimo,”amesema.

Amesisitiza kuwa, kukamilika kwa mradi wa bwawa la Membe kutaongeza uzalishaji wa mazao hivyo Wizara ya Kilimo ina wajibu kuhakikisha wakulima wanapata uhakika wa masoko ili kuepuka changamoto zitakazojitokeza.

Mhe. Kaboyoka ameishauri Tume kutoa elimu kwa wakulima kupanda miti katika eneo hilo, ili kukabiliana na hali ya ukame iliyopo mkoani Dodoma.

Baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Mhe. Aloyce Kamwelwe wameipongeza Tume kwa kuwa na weledi katika usimamizi wa mradi na kuhakikisha unazingatia viwango vya ubora vilivyopo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) Bw. Raymond Mndolwa, amesema mradi wa ujenzi bwawa la Membe umefikia asilimia 87.5% ya utekelezaji.

Amesisitiza kuwa ujenzi wa Bwawa hilo la Membe litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo bilioni 12. 

“Maji haya yataweza kumwagilia hekta 2,500 za mashamba kwa wakulima zaidi ya 1,500 wa kata ya Membe,”amesema.

Nao baadhi ya wakulima wa Membe akiwemo Jemima Kalebi, wameishukuru Serikali kupitia Tume kwa hatua ya utekelezaji wa mradi huo kwani unaleta matumaini.

Jemima amesema, wana matarajio makubwa katika kilimo cha Umwagiliaji kuwa kitainua uchumi wao na kuwa na uhakika wa chakula.  

WADAU WAITIKIA WITO WA UONGEZAJI THAMANI MADINI NCHINI

▪️Ni utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan

▪️Kiwanda cha kuchakata madini ya shaba chajengwa Wilayani Chunya,

▪️Serikali yaahidi kuwezesha viwanda zaidi vya uongezaji thamani madini

▪️Wachimbaji wadogo kunufaika na soko la uhakika la Madini Shaba

Kufuatia utekelezaji wa Mkakati wa kutosafirisha madini ghafi nje ya Nchi, Serikali yapongeza Wadau kwa kuitikia wito wa *Mheshimiwa Rais Dkt. Samia S. Hassan* wa kujenga viwanda vya uongezaji thamani madini nchini.

Hayo yemesemwa leo na Waziri wa Madini, *Mh. Anthony Mavunde (Mb)* alipotembelea kujionea ujenzi wa kiwanda cha uongezaji thamani madini ya shaba kilichopo Kata ya Mbugani Wilayani Chunya kinachomilikiwa na Kampuni ya Mineral Access System Tanzania (MAST).

"*Mh. Rais* ametuelekezaee kuhakikishia tunasimamia Sheria na Kanuni ili kuwezesha madini kuongezwa thamani hapa nchini kabla yayajasafirishwa nje ili nchi kunufaika na sekta ya madini.

"Tutaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa wadau na wawekezaji wengine walio tayari kuunga mkono jitihada hizi za Mhe. Rais ili kama Nchi tupate manufaa zaidi ya kiuchumi ikiwemo kuongeza upatikanaji wa ajira kwa wananchi wetu na kukuza pato la Taifa" alibainisha Mhe. Mavunde.

Aidha, Waziri Mavunde alieleza kuwa madini ya shaba yanahitaji kuongezwa kiwango kwa kuchakatwa kufikia asilimia 20 au zaidi ili yaweze kuuzwa nje, Ile hali madini yanayopatikana nchini yana kati ya 0.5% mpaka 2%, na kwamba kiwanda kitakuwa kinazalisha shaba kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 70, ambapo alisisitiza ni mageuzi makubwa sana ya kiuchumi nchini.

Vilevile, Waziri Mavunde alioneshwa kufurahishwa na mpango wa Kiwanda cha MAST wa kuhudumia wachimbaji wadogo kupitia kutoa elimu, kugharamia uchimbaji na kuwa soko la shaba yao ya kiwango cha chini ambayo awali walikuwa wakihangaika na soko. Hili litakuwa ni suluhisho tosha kwa wachimbaji wadogo kwani nguvu zao hazitakwenda bure.

Akisisitiza mikakati ya Serikali kwa wachimbaji wadogo, Mhe. Mavunde alibainisha kuwa Wizara ipo mbioni kuanzisha Vituo vya ukodishaji wa mitambo ya uchimbaji Nchi nzima ili kusogeza huduma hiyo kwa wachimbaji wadogo na kwa gharama nafuu.

Awali, akimkaribisha Waziri katika kiwanda hicho, *Bw. Georgefrey Kente*, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MAST aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kuahidi kwamba Kampuni yake inakwenda kujenga viwanda vingine kama hivyo katika Mkoa wa Dodoma na Lindi ili kufikia malengo yao ya uzalishaji.

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Chunya ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya, *Bw. Michombero Anakleth* aliishukuru Serikali kwa kuwezesha ujenzi wa kiwanda hicho kwa kasi kubwa na kueleza bayana kuwa Uongozi wa Wilaya ya Chunya unaunga mkono kwa asilimia 100 zoezi la ufutaji wa leseni za madini zisizoendelezwa ili wapewe wawekezaji wenye nia njema kwa manufaa ya Nchi yetu. 

MHE.JERRY SILAA ASHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA AKILI UNDE, RWANDA


...................

Waziri Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Bw. Kundwe Moses Mwasaga, leo Machi 03, 2025 wameshiriki katika kikao cha mawaziri kuhusu matumizi ya Akili Unde ambacho kimefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kigali jijini Kigali, nchini Rwanda.

Kikao hicho kimeratibiwa na Taasisi ya Tony Blair (Tony Blair Institute for Global Change - TBI) ambacho kimejikita katika kubainishi namna Akili Unde inavyoweza kutumika na inavyotumika katika maeneo mbalimbali na kuleta ufanisi katika Sekta ya Umma barani Afrika.

Kikao hicho ni sehemu ya Mkutano wa Kimataifa wa Akili Unde Barani Afrika unaondelea nchini Rwanda kuanzia Aprili 3-4, 2025.


Wednesday, April 2, 2025

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025


...................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kusimamia kwa dhati na kwa haki misingi ya demokrasia na kuhakikisha wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi kwa uhuru, kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuchagua viongozi wenye sifa wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka  2025.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani. Ametoa wito kwa wananchi wote hususan vijana kuwa waangalifu na watu wasioitakia mema nchi kwa kuepuka kutumiwa vibaya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.

Makamu wa Rais amesema Wadau wote wa uchaguzi, hususan vyama vya siasa wanahimizwa na kukumbushwa kuwa wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika katika hali ya amani na utulivu, kwa kuendesha kampeni zenye staha na kuzingatia Sheria na miongozo mbalimbali ya uchaguzi.

 Ameongeza kwamba Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 42(2) na 65, Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 2024 pamoja na  Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Na. 4 ya mwaka 2018.

Halikadhali Makamu wa Rais  ameagiza Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa ushirikiano  wa hali ya juu kwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, ili waweze kutekeleza jukumu la kizalendo walilokabidhiwa la kuhakikisha kuwa wanawafikia wananchi na kuwapa taarifa sahihi kuhusu sera, mipango, miradi na mikakati ya Serikali katika kuwaletea Maendeleo.

Vilevile Makamu wa Rais amesema Mbio za Mwenge pamoja na mambo mengine zitaangazia masuala ya lishe bora, mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhini ya VVU na UKIMWI, mapambano dhidi ya dawa za kulevya pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

Makamu wa Rais amesema wazo la kukimbiza mwenge wa uhuru nchi nzima na kila mwaka lilitolewa na Vijana wa TANU katika kikao chao kilichofanyika tarehe 26 Juni, 1964. Lengo kuu likiwa ni kutekeleza kwa vitendo azma ya Baba wa Taifa ya kuhamasisha umoja, upendo, amani na ujenzi wa Taifa kwa kuhamasisha maendeleo. Tangu wakati huo, mwenge umekuwa ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo  kupitia mbio hizo hamasa kubwa imetolewa ili kuendelea kudumisha amani, na kujenga uzalendo, umoja na mshikamano. Katika kipindi chote hicho, mbio za mwenge zimekuwa na mafanikio makubwa yanayosadifu maono ya waasisi wa Taifa letu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2025 zinabeba kauli mbiu isemayo "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu" ambayo inalenga kuwakumbusha na kuwasisitiza Watanzania wote kutumia kikamilifu haki yao ya kikatiba ya kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

 

Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2025 unatarajiwa kukimbizwa kwa muda wa siku 195, katika Mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Serikali itafikisha ujumbe kwa wananchi na kuhamasisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kutembelea, kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.

Uzinduzi wa Mbio za Mwenge kwa Mwaka 2025 umehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Dotto Biteko, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Said,  Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu, Viongozi wa Mahakama, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa pamoja na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali.


WABOBEZI KATIKA SAYANSI WAKUTANA KUJADILI MABADILIKO YA HALI YA HEWA


.................................

Wabobezi katika sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi wamekutana nchini Tanzania katika kongamano kwa ajili ya kujadili mchango wa kukabiliana masuala mbalimbali ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Kongamano hilo limeratibiwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, likijumuisha wataalamu wa sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tasnia zinazohusiana kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.

Akifungua kongamano hilo Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Jaji Mshibe Ali Bakari, amesisitiza ushiriki wa wataalamu wengi kutoka Afrika Mashariki katika mchakato wa IPCC kutoka Afrika Mashariki.

“Ni matumaini yangu kuwa kupitia makongamano kama haya ya uhamasishaji wa wanasayansi kujihusisha katika kufanya tafiti zinazokidhi matakwa ya IPCC, wataalam wengi zaidi kutoka Afrika Mashariki wataweza kutoa mchango kikamilifu katika utayarishaji wa ripoti za tathmini ya Saba ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi ya IPCC (IPCC AR7)” amesema Jaji. Mshibe

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa IPCC, Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema kuwa ripoti za IPCC zimekuwa na mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi kimataifa na nchi moja moja.

Dkt. Chang’a amesema kuwa ripoti ya IPCC ya AR7 inayoandaliwa inatarajiwa itakuwa na jukumu muhimu katika mustakabali wa hatua za kuchukua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa natabianchi kwa kuzingatia taarifa za kisayansi.

“Taarifa hizo zitakuwa zimehakikiwa vyema ambapo zina mchango mkubwa katika kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi kikanda na Duniani kote,” amesema Dkt. Chang’a.

Kongamano hilo limeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuongeza uelewa kuhusu shughuli za Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Ripoti zitakazoandaliwa katika mzunguko wa saba wa IPCC (AR7) kuhusu tathmini ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi na fursa za kushiriki katika mchakato huo.

Mchakato huo ikijumuisha uandishi, uteuzi wa wataalamu na mapitio ya ripoti za IPCC pamoja na kuhamasisha wanasayansi hasa vijana, watendaji, wakufunzi na wanafunzi kufuatilia na kushiriki katika mchakato mzima wa shughuli za IPCC katika mzunguko wa saba ulioanza mwaka 2023 na unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 au 2030.

 

WANANCHI WATAKIWA KUKOPA MIKOPO INAYOTOLEWA NA SERIKALI NA TAASISI RASMI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Bw. Binuru Shekidele, akikabidhiwa vipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mnzava, vyenye mada mbalimbali ikiwemo akiba, mikopo na uwekezaji ambazo zitafundishwa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Bw. Binuru Shekidele, akikabidhiwa vipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mnzava, vyenye mada mbalimbali ikiwemo akiba, mikopo na uwekezaji ambazo zitafundishwa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Bw. Binuru Shekidele, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akitoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Sengerema, mkoani Mwanza, walioshiriki mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Bw. Jacob Nkungu, akifafanua jambo kwa wananchi wa Sengerema, walioshiriki mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Sengerema, mkoani Mwanza, wakifuatilia mada mbalimbali ikiwemo akiba, mikopo, uwekezaji, bima, kujiandaa kustaafu wakati wa  mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, wakazi wa Sengerema, mkoani Mwanza,  wakiangalia filamu yenye mada mbalilimbali ikiwemo mikopo, akiba na uwekezaji zilizofundishwa wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, Bw. Boniface Maxmilian, akiuliza swali namna ya kuitambua Taasisi iliyosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania  (BoT), wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Sengerema,  yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Sengerema, Mwanza)
................

Na. Josephine Majura, WF, Sengerema, Mwanza 

Wananchi wametakiwa kukopa mikopo inayotolewa na Serikali na Taasisi rasmi ili kujiepusha na udhalilishaji unaoweza kutokea kutokana na kukopa mikopo yenye masharti magumu kutoka kwa Taasisi zisizo rasmi na kwa Wakopeshaji Binafsi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Bw. Binuru Shekidele, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambayo ipo mkoani Mwanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali.

Aliongeza kuwa mikopo rasmi inayotolewa na Serikali na Taasisi zilizoidhinishwa hufuata taratibu za kisheria ambazo zinalinda haki za wakopaji na kuhakikisha wanapata huduma za kifedha kwa masharti nafuu.

“Mikopo rasmi kutoka serikalini ina masharti nafuu, riba ya chini, na inalenga kuwawezesha wananchi kuboresha maisha yao bila kuingia kwenye matatizo ya kifedha”, alisema Bw. Shekidele.

Alifafanua kuwa ni muhimu kwa wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu masharti ya mikopo wanayochukua ili kuhakikisha wanakopa kwa uangalifu na kulipa kwa wakati bila kuingia katika changamoto zisizo za lazima.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Bw. Jacob Nkungu, aliwashauri watoa huduma za fedha kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi bila kuwakandamiza.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha mkazi wa Sengerema, Bw. Boniface Maxmilian, alishauri elimu ya fedha ifike kwa wananchi wote katika ngazi zote ili waweze kuwa na uelewa mpana wa masuala ya fedha ikiwemo kufahamu mikopo salama, kuwa na uelewa wa masuala ya bajeti na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.

Naye Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Santley Kibakaya, alisema kuwa baada ya kutoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali wananchi watabadilisha utaratibu wa maisha, ikiwemo kuacha kukopa kwenye Taasisi ambazo sio rasmi, kuwashirikisha wenza wao kabla ya kuchukua mikopo na kutotumia mali za familia kama dhamana ya mkopo bila ridhaa ya wanafamilia wengine.

“Katika mikoa yote tuliyopita kumekua na mwitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza kupata elimu, naamini kupitia elimu tuliyowapa watajikomboa kiuchumi wakizingatia yale tuliyowafundisha”, alisema Bw. Kibakaya.

Hadi sasa Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi zake, imetoa elimu ya fedha katika mikoa 16, ikiwemo Mkoa wa Kagera, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Pwani, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mtwara, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mara na Mwanza.

MWISHO.

Tuesday, April 1, 2025

SAMIA LEGAL AID YATOA ELIMU YA MSAADA WA KISHELIA ILI HAKI IWEZE KUPATIKANA

 

 Na Prisca Libaga, Arumeru


Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Amir Mkalipa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia Kampeni ya Msaada wa  Kisheria ya Mama Samia katatua migogoro na malalamiko yao yanayosababishwa na kukosekana elimu ya msaada wa kisheria ili haki iweze kupatikana.

Mkalipa ameyasema  hayotarehe 31 Machi, 2025 wakati alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro wakati wa  uzinduzi  wa Kampeni  ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliyozinduliwa katika kata ya Makiba wilayani Arumeru.
 
Amesema Rais Samia anastahili pongezi kubwa kwa kuja na wazo la kuanzisha kampeni hiyo ambayo inakwenda kutatua migogoro mingi ya kisheria ambayo wao kama watawala wamekuwa wakishindwa kuitatua.

" Unajua sisi kama watawala linapokuja suala la mahakama tunashindwa kuingilia kati lakini kampeni hii ina wataalam wa sheria ambao wao ndio wamekuwa wakishinda mahakamani, wamekuja kumaliza kero hizo za wananchi watawaelekeza nini cha kufanya na mwisho kila mwananchi atapata haki yake," amesema Mkalipa.

Amesema ijapokuwa siku kumi za kusikiliza kero za kisheria wilayani humo ni chache, lakini sio haba kwa kuwa sehemu kubwa ya migogoro itapatiwa ufumbuzi na wananchi watapunguza kufika ofisi za wilaya. 
Wakiwasilisha migogoro yao mbele ya Mkuu wa Wilaya wananchi wa kijiji cha Malula wamelalamikia kutaka kupokonywa mashamba ambayo wamekuwa wakiyalima tangu mwaka 1972.

Wananchi hao wamemtaja mwananchi mmoja kwa jina la Zara kuwakataza kulima mashamba hayo akidai yeye ndio mmiliki wa mashamba hayo tangu miaka ya 1960 akiyarithi kutoka kwa marehemu wazazj wake.

Mkuu wa Wilaya Amir Mkalipa aliwaeleza wananchi hao kuwa mgogoro huo anaufahamu vizuri na kwamba mashamba hayo ni mali ya Serikali na imeshayatenga kwaajili ya eneo la uwekezaji (EPZ), na kwamba hakuna mtu yoyote aliyemilikishwa.
" Mashamba ya malula ni eneo la Serikali, yameshatengwa kwaajili ya uwekezaji wa EPZ lakini kama Serikali tutakuja kuwasikiliza na tutawapanga kwa muda ili muendelee kuyalima lakini sio kuwamiliķisha na watu wachache waliojenga nyumba zao zinaenda kubomolewa,"Amesema DC Mkalipa.

Kwa upande wake mkurugenzi  wa huduma za msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema kuwa,  Kampeni hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kupata  huduma za mawakili  bure pamoja na elimu ya maswala ya kisheria.