JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatatu, 28 Aprili 2025

HIZI HAPA HABARI ZILIZO PEWA NAFASI KWENYE KURASA ZA MBELE YA MAHAZETI LEO TAREHE 28.04.2025

 Good morning Habari gani popote ulipo Nikukaribishe kupitia vichwa vya habari kwenye magazeti ya leo tarehe 28.04.2025




































Jumapili, 27 Aprili 2025

BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA KWA KUSIMAMIA VIZURI UCHUMI WAKE

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akiwa na Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, walipokutana na kufanya mazungumzo kwenye Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), ukiwa katika mazungumzo na Timu ya Benki ya Dunia ikiongozwa na Makamu mpya wa Rais wa Benki hiyo anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, kwenye Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C, Marekani)

TANZANIA NA CHINA KUKUZA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIDIPLOMASIA

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiwa ameongozana na Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiwa katika mazungumzo mafupi na Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, baada ya kumpokea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akipitia baadhi ya taarifa alizokabidhiwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, wakati alipoongoza ujumbe wa Tanzania kumpokea Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri Bw. Twaha Mwakioja.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akisalimiana na Bw. Chu Kun, Kansela wa Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, alipowasili kwa ajili ya kumpokea Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na China.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

....................

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania kumpokea Mhe. Tang Wenhong, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe April 26 hadi 29, 2025.

Katika ziara hiyo inatarajiwa kuwa na vikao mbalimbali vya majadiliano kati ya ujumbe wa Tanzania na China, yanayolenga kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

MNDOLWA: 'MZIKI' WA RAIS SAMIA BADO UNAENDELEA UMWAGILIAJI


Mradi wa Membe Kunusuru SGR

Dodoma: Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa amesema kuwa kasi  ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan bado inandelea katika miradi ya umwagiliaji na kwamba kila mkoa utafikiwa. 

Mndolwa amesema miradi yote inaendelea vyema na itakamilika kwa wakati lengo likiwa kuwawezesha wakulima nchini kulima kilimo biashara chenye tija na kuachana na kilimo cha mazoea kinachotumia nguvu nyingi lakini manufaa yake ni madogo. 

Mkurugenzi Mndolwa amesema hayo katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ilipotembea Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji Membe mkoani Dodoma. 

"Sisi Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji tuna nafuu sana. Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na miradi yote inaendelea. 

"Rais Samia anatekeleza kwa vitendo ahadi zake, kila mkoa utafikiwa na miradi ya umwagiliaji na uchimbaji wa visima, yote ni kuhakilisha serikali inawawezesha wakulima kupata tija, nchi iwe na chakula cha uhakika na ziada tuuze nje, " alisisitiza. 

Mndolwa alisema mathalani kwa sasa Mkoa wa Manyara kuna miradi yenye thamani ya sh bilioni 80 inatekelezwa ukiwamo uchimbaji wa mabwawa na visima vya umwagiliaji, ufugaji wa samaki na utalii.

Akizungumzia Mradi wa Membe uliokamilika kwa zaidi ya asilimia 90, Mndolwa alisema bwawa hilo lenye ujazo wa lita bilioni 12 ambalo lina uwezo wa kumwagilia hekta 2,500 likikamilika litanufaisha watu zaidi ya 1,500.

Alisema mradi huo ni kati ya miradi 22 ukikamilia utawawezesha wakulima kulima na kuvuna mwaka mzima badala ya kusubiri kuvuna kwa msimu. 

'Kubwa zaidi mradi huu ni kati ya miradi ya kimkakati wenye lengo la kudhibiti miundombinu ya Reli yetu ya Kisasa ya SGR isiharibike kwa mafuriko. 

"Sote ni mashahidi eneo la Kilosa kila mwaka tunashuhudia uharibifu mkubwa unaotoka na mafuriko. Ukipita na SGR katika eneo hilo kuna maporomoko mengi ya maji na chanzo chake ni hiki lakini ujenzi wa Bwawa hili utasaidia maji kupugua na reli yetu kuwa salama kutoka na maji hayo. "

Alisema ujenzi wa mradi huo una faida kuu tatu, moja ni killimo na ufugaji ukiwamo wa samaki, utalii na uboreshaji wa miundombinu. 

Alieleza kuwa, mradi huo utaokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumiwa na serikali kwa wanachi wa Kilosa kuokoa maisha, kununua chakula na kukarabati miundombinu mara kwa mara. 

Katibu Tawala Msaidizi Sekfa ya Uchumi, Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba alisema changamoto kubwa kwa jiji la Dodoma ni maji na kwamba ujenzi wa bwawa hilo ni fursa kubwa kwani litasababisha wakulima kulima kwa uhakika. 

"Mwaka huu Mkoa wa Dodoma tumepata mvua pungufu jambo ambalo ni hatari kwa kilimo chetu, lakini kuwepo kwa bwawa hili kutabadili kilimo chetu kiwe cha biashara na hali ya uchumi wa mwananchi mmoja itaboreka na hatimaye kuongeza pato la taifa," alifafanua Aziza.




 

PROF. MBARAWA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA BIASHARA WA CHINA.

 

Na Mwandishi wetu

Dar es salam.

Waziri wa Uchukuzi  Prof Makame Mbarawa  amezungumza  na Naibu Waziri wa Biashara wa China Mhe Tang Wenhong   Jijini Dar es Salaam ambapo   Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya usafirishaji na biashara, hasa kupitia maboresho ya miundombinu ya bandari, Reli ya TAZARA na  Ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR

Kupitia Mkutano huo viongozi  hao  wamewejadili   mikakati ya kuharakisha utiaji saini wa Mikataba ya miradi ya maboresho na ukarabati wa Reli ya TAZARA, kuongeza matumizi ya bandari yetu katika kusafirisha shehena, ambapo Naibu Waziri wa Biashara wa China amesisitiza dhamira ya serikali yao kuendelea kuwekeza nchini Tanzania, huku akieleza kuwa maendeleo yaliyofanyika  kwenye bandari, Ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaoendelea, na ukarabati wa reli ya TAZARA utakaofanyika vitakuwa kichocheo kikubwa cha biashara na mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo   Prof.Mbarawa   ameeleza kuwa ushirikiano uliopo baina ya Nchi hizi mbili ni muhimu kwa uchumi wa Taifa na unafungua fursa zaidi kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kanda nzima ya Afrika Mashariki. 

Aidha  Mkutano huo  unaenda  kuimarisha zaidi urafiki na ushirikiano wa kimaendeleo.

Vilevile  Mkutano huo umehudhuriwa  na baadhi ya Viongozi na watumishi kutoka TPA,TAZARA, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

DKT. BITEKO AMWAKILISHA RAIS SAMIA UWEKWAJI WAKFU ASKOFU MTEULE JIMBO LA IRINGA

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Askofu wa Mafinga, Mhashamu Vincent Mwagala wakati alipowasili katika Ibada ya kumsimika na kumuweka wakfu Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali iliyofanyika katika Viwanja vya Kichangani, Mjini Iringa, Aprili 27, 2025.

Dkt. Biteko anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu Mteule, Romanus Elamu Mihali kuwa Askofu wa Jimbo la Kitume la Iringa.


KONGAMANO LA KWANZA LA KISWAHILI LAFANYIKA NCHINI NAMIBIA.

 

Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia kwa kushirikiana na Chuo cha Triumphant ziliandaa Kongamano la Kwanza la Kiswahili lililozungumzia mchango wa lugha ya Kiswahili katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika hususan Namibia.

 

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo lililofanyika Aprili 25, 2025 alikuwa Mheshimiwa Lt.Gen.(Rtd) Epaphras  Denga Ndaitwah, Mwenza wa Mheshimiwa Rais wa Namibia.

Mtoa mada Mkuu kutoka Tanzania alikuwa Bi.Consolata Mushi, Katibu Mtendaji wa BAKITA ambaye alimwakilisha Mhe.Prof.Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (MB), Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo.


Watoa mada wengine kutoka Tanzania walikuwa Balozi Lt.Gen.(Rtd) Abdulrahman Shimbo, Balozi Brig.Gen.(Rtd) Francis Mndolwa na Dkt .Eliah Victor, Mkurugenzi wa Vipindi kutoka TBC. 

Kwa upande wa Namibia,mtoa mada alikuwa ni mmoja wa Wapigania Uhuru wa Namibia aliyeishi Kongwa, Dodoma nchini Tanzania.


Aidha ,Kongamano hilo lilihudhuriwa wa Wapigania Uhuru wa Namibia walioishi Tanzania,Vijana wa Namibia waliozaliwa uhamishoni, Mabalozi, Wanazuoni,Wanafunzi pamoja na Waandishi wa Habari.


Listen Mkisi Radio