Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) nchini Tanzania, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema suala la kuoa wake wengi linatafsiriwa kama ni dhambi hivi sasa Mchungaji Lusekelo ameeleza hayo Julai 11, 2024 wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Wasafi FM ambapo amehoji kama agizo la Mungu ni kuja duniani na kuongezeka ni kwa vipi tutaongezeka bila wake wengi. "Mimi kule kwetu ni Chifu hivyo nilitakiwa niwe na wake sita, si kwa maana ya uzinzi, hapana. Mungu amesema mkazae ili muongezeke mkajaze nchi, haiwezekani wakati wa Abraham (kuwa na wake wengi) haikuwa ni dhambi halafu leo iwe ni dhambai, Yesu mwenyewe ambaye ni mwokozi wa dunia ni mtoto wa mama mdogo, Daud alioa mke mdogo, mke wa Uria ndio ikaenda akamzaa Selemani na Yesu huko huko." alisema Mchungaji Lusekelo na kuongeza " Inakuwaje leo kuwa na wake wengi inakuwa ni dhambi?. Wakiristo leo wako tayari wanaume kwa wanaume waoane kanisani lakini si ndoa mbili. Ulaya wanaume kwa wanaume wanaoana, wasagaji wanabarikiwa lakini si suala la kuoa mke wa pili, kuna kitu gani hapa wazungu wanatufunga? "
0 Comments