Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Pango lililogunduliwa mwezini linaweza kuwa makao ya wanadamu

 

Wanasayansi kwa mara ya kwanza wamegundua pango kwenye Mwezi.

Pango hilo lenye kina cha mita 100, linaweza kuwa mahali pazuri kwa wanadamu kujenga makao ya kudumu, wanasema.

Ni moja tu kati ya mamia ya mapango yaliyofichwa katika "ulimwengu wa chini ya ardhi, ambao haujagunduliwa", kulingana na watafiti.

Nchi zinakimbia ili kupata makao kudumu wa binadamu mwezini, lakini zitahitaji kuwalinda wanaanga dhidi ya mionzi, halijoto kali na hali ya hewa ya anga.

Helen Sharman, mwanaanga wa kwanza wa Uingereza kusafiri angani, aliiambia BBC News kwamba pango hilo jipya lililogunduliwa lilionekana kama mahali pazuri kwa makao na alipendekeza kuwa wanadamu wanaweza kuwa wanaishi kwenye mashimo ya mwezi katika miaka 20-30.

Lakini, alisema, pango hili ni la kina sana hivi kwamba wanaanga wanaweza kuhitaji kujificha ndani na kutumia " lifti" ili kutoka.

Lorenzo Bruzzone na Leonardo Carrer katika Chuo Kikuu cha Trento nchini Italia walipata pango hilo kwa kutumia rada kupenya shimo kwenye uwanda wa mawe unaoitwa Mare Tranquillitatis.

Inaonekana kwa macho kutoka Duniani, na pia ndipo Apollo 11 ilitua mnamo 1969.

Kutoka BBC

Post a Comment

0 Comments