Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Yasemekanayo Katika Soka la Ulaya July 16, 2024

 Mkufunzi wa Newcastle United Eddie Howe ni mmoja wa makocha wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Gareth Southgate iwapo ataamua kujiuzulu kama kocha wa timu ya taifa ya England. Wachezaji wa zamani wa England Steven Gerrard na Frank Lampard pia wanatazamiwa kuwania nafasi hiyo. (Guardian)




Manchester United wamemuulizia beki wa Ujerumani Jonathan Tah huku Bayern Munich wakishindwa kufikia makubaliano na Bayer Leverkusen kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Florian Plettenberg)


Arsenal wamekataa ofa ya Fulham ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Emile Smith Rowe, 23. (Standard)


Liverpool na Atletico Madrid wanavutiwa na mlinzi wa RB Leipzig Mfaransa Mohamed Simakan mwenye umri wa miaka 24. (Sky Germany



Mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 31, anatazamiwa kujiunga na AC Milan kwa mkataba wa miaka minne kutoka Atletico Madrid. (Fabrizio Romano)


Manchester City wamepiga hatua katika juhudi za kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 26, kutoka RB Leipzig. (Football Insider)


Bayern Munich pia wanavutiwa na Olmo, ambaye alifunga mabao matatu wakati wa Euro 2024 alipoisaidia nchi yake kushinda michuano hiyo. (Fabrizio Romano)


Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Mikel Merino ni mmoja wa wachezaji wanaolengwa na Barcelona kuimarisha safu yao ya kati, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa Real Sociedad. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)


Arsenal pia wanapania kumnunua Merino, ambaye aliwahi kuichezea Newcastle United kabla ya kurejea Uhispania. (Telegraph - usajili unahitajika)


Newcastle United iko tayari kumenyana na Everton katika harakati za kumsajili winga wa Italia Wilfried Gnonto mwenye umri wa miaka 20 kutoka klabu ya Leeds United. (Teamtalk)


Uhispania Mikel Merino

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang mwenye umri wa miaka 35, anakaribia kujiunga na klabu ya Saudi Arabia ya Al-Qadsiah. (Sky Sports)


Southampton wamekubali dili la hadi £18m kumsajili kiungo wa kati wa England Flynn Downes, 25, kutoka West Ham. (Standard - usajili unahitajika)

Post a Comment

0 Comments