Mwenyekiti Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo Taifa, Janeth Rithe akihutubia mkutano wa hadhara huko Kasulu Kigoma jana.
MWENYEKITI wa Ngome ya Wanawake ya Chama cha ACT-Wazalendo Taifa, Janeth Rithe amepinga tabia ya askari wa Jeshi la Polisi nchini kuwajengea hofu wananchi badala ya kuwa walinzi bora wa rai na mali zao.
Kwa msingi huo, mwenyekiti huyo wa Ngome ya Wanawake amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kufumua mfumo mzima kwa kuunda upya jeshi la Polisi ili liweze kufanyakazi sambamba na wananchi kuliko ilivyo sasa ambapo wanaonekana maadui.
Rithe aliyasema hayo Julai 26/2024 katika mkutano wa hadhara wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo yeye na viongozi wengine wapo katika mikoa mbalimbali kuimarisha uhai wa chama.
“Ninaitaka Serikali kuacha kuchezea upatu maisha ya Watanzani, wakulima wananyanyasika na Jeshi la polisi ambalo lilitakiwa kulinda raia na mali zake lakini badala yake limegeuka kuwa chombo cha kuwanyanyasa raia”alisema Rithen a kuongeza kuwa:
“Wakulima wanachomewa mazao yao kwa kisingizio cha kulima eneo ambalo sio rasmi, unyonyaji huu wa jeshi la polise limepoteza weredi wa kuitwa jeshi la wananchi badala yake wamekuwa waporaji na wanyanyasaji wa wananchi.”alisema
Kufuatia hali hiyo, mwenyekiti huyo wa Ngome ya wanawake aliwataka wananchi kufanya mabadiliko kwa kuchagua viongozi wanaotokana na ACT- Wazalendo ili kuleta mabadiliko kuanzia ngazi ya chini kabisa na kuwafanya wananachi kuwa na maisha bora kutoka kwa viongozi wenye dhamira ya dhati kwa kuwatumikia wananchi na sio Cham Cha Mapinduzi (CCM).
0 Comments