LINDI.....Wakulima wa zao la ufuta kutoka kijiji cha Zinga Kibaoni wilayani Kilwa mkoani Lindi wamelalamika kucheleweshewa malipo yao baada ya kuuza zao hilo kwenye mnada.
Wakukima hao wameyasema hayo katika mnada wa saba uliofanyika katika kijiji cha Zinga Kibaoni Almashauri ya wilaya ya Kilwa ukiwa ni mnada wa saba.
Kwenye mnada huo wa 7 unaoendeshwa kwa chia ya mtandao ukisimamiwa na ofisi ya uendeshaji biashara ya soko la bidhaa Tanzania (TMX) pamoja na chama kikuu cha Lindi Mwambao wameuza kwa bei ya ya juu ikiwa ni sh 3480 na bei ya chini ni sh 3200 na wakulima wameridhia kuuza.
"Nimepima ufuta tokea tarehe 20 mwezi huu lakini sijalipwa na sijui ni kwanini.Magari yanafika kuja kuchukuwa ufuta na mdada unafanyika lakini yakirudi majina ya wanaostahili kulipwa yana rudi machache hili lina tushangaza"amesema Ramadhani Haji mkulima wa ufuta.
Kurwa Masigani amesema kwa mkulima kumcheleweshea malipo ni kumrudisha nyuma kwani anapoenda kupima ufuta anatarajia apate pesa zake afanyie mambo yake lakini wanashangaa kuona wanacheleweshewa malipo yao kama wataendelea kuwacheleweshe kuta wavunja moyo wakulima katika msimu ujao.
Mwanaidi Hashimu amesema anashukuru bei ni mzuri sio mbaya wanashukuru kwa hilo anatamani bei ziendelee kupanda na sio kushuka.
"Mkulima anapolima anatarajia apate pesa sasa anapo mcheleweshea inakuwa sio vizuri kwasababu unamuondoka katika malengo yake hivyo watulipe kwa wakati ili tukafanye mambo yetu tuliyo panga kufanya"amesema Mwanaidi mkulima wa ufuta.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kibaoni Amcos Bakili Kilete amekiri kuwapo kuchelewa kulipwa kwa baadhi ya wakulima kutokana na kuwepo kwa mzigo mwingi kunasababishwa na uchache wa wafanya kazi.
"Tunachelewa malipo sio tatizo la chama kikuu cha Lindi Mwambao na wala sio banki ni sisi wenyewe tumekuwa na wafanyakazi wachache lakini uzalishaji mkubwa sana mnada unapo fika tunaweza tukawa na tani mia nane hadi elfu mmoja hivyo tunachukuwa muda mrefu kwenye kufanya uhakiki hadi kufikia katika malipo"
"Lakini tunapambapana kuhakikisha kila mkulima analipwa kwa wakati wapo walio lipa minada mitatu lakini sisi tumelipa minada mitano hadi sasa amesema Kilete mwenyekiti wa Kibaoni Amcos.