Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Nimezikabili Changamoto Zote Nilizo Kutana Nazo Katika Biashara ya Kutembeza matunda barabarani.

Leo Hii Mkisi Digital, Tumekutana na Mwana dada mtafutaji, mpambanaji katika kutafuta fedha za kuweza kuilisha familia yake lakini pia fedha ya kuweza kufikia malengo yake ambayo anayatarajia, Tuungane pamoja katika safari ya MwanaDada huyuu,

Mazungumzo yetu yalitakujua utambulisho wake, Sababu kufanya hii biashara, changamoto pamoja na faida zake, lakini kikubwa tukataka kujua ni yapi matarajio yake katika kazi au biashara hii, huyu hapa twende pamoja,


Jina langu ni Mary Yohana, Ninaumri wa miaka 23, ninaishi Buza Kilungule na nifanya biashara zangu mjini {Kariakoo} alisema Mary , Ninamtoto mmoja ninae mlea.


Mimi ni mzaliwa wa Tanga lakini asili yangu ni mtu wa Iringa huko ndiko baba yangu anako ishi na ndo alikotokea , Hapa Dar es salaam nilikuja mwaka 2022 nilifikia kwa dada yàngu huku nikiwa najitafuta nini cha kufanya ili niweze kujitegemea mwenyewe yani nitoke kwa dada niende nika pange chumba changu nianze kujitegemea


Mwaka 2023 nilifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni moja ya boss mmoja mkubwa hapa dar es salaam, niliajiliwa kwenye nafasi ya mlizi ambapo kampuni yetu ilikuwa ina taasisi nyingi ambazo tuliluwa tunalinda ikiwemo taasisi ya boss mwengine na yeye ni mkubwa hapa nchini alafu pia ni maarufu sana 


Mwanzoni mwa mwaka 2024, niliachana na kazi yangu ya ulinzi, kulikuwa na changamoto nyingi kama mwanamke popote utakapo fanya kazi lazima ukutane na changamoto lakini kubwa kuliko zote mshara ulikuwa hautoshi nilikuwa najikuta nakuwa na madeni mengi kuliko mshara ninaoupata, Ukizingatia hayo yote nina familia ambayo inanitegemea kama mama baada ya kulipa madeni yote niliona nibora niache kazi 


Mary aliendelea kuileza Mkisi digital... Hapo ndipo nilipata akili ya kuanza kuuza na kutembeza matunda barabarani kwa kile kipato kidogo nilicho kuanacho hicho hicho nianza nacho nakuanza rasmi biashara hii 


Hakika kazi hii ni ngumu sana nilipata changamoto wakati nilipo anza hii kazi kwa sababu ilinitaka kuamka asubuhi na mapema sana kwaajili ya kuwahi bidhaa sokoni lakini nilikuwa nina aibu kubwa sana kwa sababu ya ugeni wangu kwwnye hii Kazi, nilipambana kishujaa sana mpaka kuzoea hii kazi 


Kwa sasa nimezoe na ninaipenda kazi yangu licha ya kukumbwa na changamoto za kutakwa kimapenzi na kila mteja ambaye unakutana nae, Alicheka sana Mary , akasema kwamba " Kuna wateja wengine watu wazima na wenye magari yao utakuta ananiambia gawia matunda watu alafu nitakulipa pesa yote uingie kwenye gari" yani kama hujitambui katika biashara hii na kama thamani yako huioni katika biashara hii basi lazima wanaume watakutumia sana


Mimi natamani sana kufanya biashara ya chakula, nilisha wahi kufanya hii biashara ya chakula nilikuwa na pelekea wateja sehemu mbalimbali japo mshahara ulikuwa mdogo sana, Natafuta mtaji ili niweze kuwa na ofisi ya chakula ambayo nitaajiri wasichana kwa wavulana 


Napenda kushauri wasichana wenzangu kama unataka kufanya biashara hii ya kuuza na kutembeza matunda barabarani basi inabidi ujidhatiti kweli kweli, Uwwtayari kukubaliana na changamoto utakazo kumbana nazo, lakini usijirahisishe kwa wanaume ambao watakao kuwa wanakutaka kimapenzi.


Ahsante Sana mfuatiliaji wa Mkisi digital blog kwa kufuatilia simulizi fupi ya Mary Yohana endelea kufuatilia mkisidigital.com kwa Taarifa mbalimbali.



Post a Comment

0 Comments