Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WAZIRI WA ZAMANI PROF SARUNGI AFARIKI DUNIA


...................

Waziri wa zamani, Profesa  Phillemon Sarungi amefariki dunia.

Profesa Sarungi ambaye alikuwa  Daktari bingwa wa Mifupa amefariki jana Jumatano, Machi 5,2025 jijini Dar es Salaam. 

Profesa Sarungi, baba wa  Maria Sarungi Tsehai, mtetezi wa haki za binadamu na mhariri wa vyombo vya habari huru nchini Tanzania amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.

Enzi za uhai wake Profesa Sarungi ameshika nafasi mbali mbali za uongozi ikiwa ni pampja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Profesa Sarungi alifahamika kwa utaalamu wake wa mifupa na mara kadhaa palipotokea ajali alilazimika kuacha majukumu yake ya uwaziri na kuingia hospitalini kuongoza madaktari katika upasuaji wa mifupa.

  Miaka ya 2000 Taifa lilishudia ajali mbaya ya treni iliyosababisha vifo vingi na kuacha majeruhi Profesa Sarungi wakati huo aliwa Waziri wa Ulinzi alikwenda kuungana na madaktari wengine kusimamia upasuaji wa majeruhi hao katika Hospitali ya Kibaha..

 

Post a Comment

0 Comments