Baadhi ya waendesha bodaboda mkoa wa mwanza maarufu boda boda na samia wamefanya maandamano ya amani kutoka mkolani hadi kwa katibu wa CCM wa mkoa wa mwanza kwalengo la kuendelea kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwanamna kinavyoendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Maandamo hayo yamefanyika leo April 28, 2025 huku wakieleza dhamira yao ya kuendelea kutoa hamasa ili Rais Dkt. Samia Suluhu ashinde kwakishindo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika October mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kufika kwenye ofisi za Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Mwenyekiti wa Boda boda na samia Ramadhan Musabi, amesema wameridhishwa na utendaji kazi wa Rais hivyo wataendelea kumuunga mkono ili azidi kutawala na kuwaletea wananchi maebdeleo zaidi.
Kwaupande wake katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Omary Mtuwa amesema Nia ya kikundi hicho ninzuri kwani wameamua kuwa wazalendo wa kukipigania chama chao cha Ccm .
Nao baadhi ya makatibu wa chama cha mapinduzi kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wamepongeza juhudi za boda boda hao kwa kukiunga mkono chama hicho kwani kina nia njema na wananchi .