Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi, utakao husisha nchi hamsini na nne na kufanyika Zanzibar.
Mshauri wa Rais na mjumbe maalum katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, pia Mwenyekiti wa Kikundi cha Waafrika cha Kujadili Mabadiliko ya Tabia Nchi (AGN), Dkt. Richard Muyungi, ameeleza kuwa mkutano huu ni muhimu kutokana na mabadiliko katika siasa za kimataifa yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha, Dkt. Muyungi amesema mkutano huo utajadili jinsi nishati safi inavyosaidia bara la Afrika, ambapo asilimia kubwa ya wananchi hawatumii nishati safi ya kupikia, na pia faida zitokanazo na juhudi za kimataifa katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
Mgeni rasmi katika mkutano huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemedi Suleiman Abdullah.