JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatatu, 16 Juni 2025

ETDCO YAKAMILISHA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KILOVOLTI 132 TABORA - KATAVI


............................

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imekamilisha ujenzi wa laini mpya ya umeme yenye msongo wa kilovolti 132 kutoka mkoani Tabora hadi Katavi.

Laini hiyo, yenye urefu wa kilomita 383, kukamilika kwake ni hatua muhimu ya kuunganisha Mkoa wa Katavi na Gridi ya Taifa.

Akizungumza leo, Juni 16, 2025, wakati wa majaribio ya laini hiyo katika kituo cha kupoza umeme cha Mpanda mkoani Katavi, Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO, CPA Sadock Mugendi, amesema ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 100.

CPA.  Mugendi ameishukuru Serikali na Wizara ya Nishati kupitia TANESCO kwa kuiamini kampuni hiyo kutekeleza mradi huo wa kimkakati.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa ETDCO, Mhandisi Dismas Massawe, amesema gharama ya mradi huo ni shilingi bilioni 116, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania. 

Amesema kuwa gharama hiyo inahusisha ujenzi wa laini ya kusafirisha umeme kwa umbali wa kilomita 383 kutoka Tabora hadi Mpanda hadi Katavi.

Mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kupeleka umeme wa uhakika wa Gridi ya Taifa kwenye maeneo ambayo hayakuwa yameunganishwa awali, kama Mkoa wa Katavi ikiwa na lengo la kuchochea maendeleo kwa kutumia nishati safi, salama, na rafiki kwa mazingira.


 

0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio