JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatatu, 16 Juni 2025

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA,KATIBU MKUU ATEMBELEA BANDA LA NCC

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma S. Mkomi akisoma maelezo kwenye Banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) alipotembelea banda hilo leo akiwa na viongozi wengine mbalimbali kutoka katika ofisi yake.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma S.  Mkomi, akiingia kwenye Banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Bw. Juma S. Mkomi akipewa maelezo na Afisa Habari na Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi  (NCC), Bi. Namsembaeli Mduma, kuhusu majukumu ya Baraza hilo wakati alipotembelea banda la NCC akiwa na viongozi wengine kutoka katika ofisi yake.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Benard Makhanda akisaini kitabu cha wageni katika Banda la NCC baada ya kupata maelezo mbalimbali kuhusu NCC.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Jafari Maganga akisaini kitabu cha wageni katika Banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) baada ya kusikia Maelezo kuhusu Baraza hilo. Be  Maganga alikuwa ameambatana na Mkurugenzi Makhanda pamoja na Katibu Mkuu wa UTUMISHI kutembelea banda hilo.

....................

Katibu Mkuu Utumishi apongeza maandalizi ya banda la NCC
Aelezwa kuhusu majukumu yanayotekelezwa na kupongeza

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (UTUMISHI), Bw. Juma S. Mkomi, ametembelea banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo na kukagua maandalizi yake.

Akiwa na viongozi wengine kutoka katika ofisi hiyo ya Rais (UTUMISHI) miongoni mwao akiwa ni Mkurugenzi Benard Makhanda na Mkurugenzi Msaidizi Jafari Maganga, Katibu Mkuu amepongeza maandalizi ya banda hilo na kusikiliza maelezo kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na NCC.

Katika maelezo hayo yaliyotolewa na Afisa Habari na Uhusiano Mkuu wa NCC, Bi. Namsembaeli Mduma, Katibu Mkuu alielezwa baadhi ya majukumu hayo kuwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu, uratibu wa usuluhishi wa migogoro inayohusu sekta ya ujenzi na uandaaji wa fahirisi ya bei ya vifaa vya ujenzi.

Majukumu mengine ni kuratibu na kufanya utafiti, ukaguzi wa kiufundi wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa nchini, kutoa mafunzo yakuwajengea uwezo wadau wa sekta ya ujenzi, wakiwemo wahandisi, wakadiriaji majenzi, wabunifu majengo na wengine kutoka katika sekta mbalimbali.

Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16, mwaka huu, itazinduliwa rasmi kesho na kuhitimishwa Juni 23, mwaka huu.

0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio