..................
Na Sixmund Begashe - Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, akiwa ameambatana na Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Utumishi Umma ametembelea Banda la Maliasili na Utalii kwa lengo la kukagua kujionea hatua ya maandalizi kabla ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo, hapo kesho tarehe 17 Juni 2025, Jijini Dodoma.
Aidha Bw. Mkomi ameipongeza Wizara hiyo, kwa hatua ya nzuri ya maandalizi pamoja na ushiriki katika maonesho hayo muhimu kwa maslahi mapana ya Taifa na wananchi kwa ujumla.
Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake inashiriki maonesho hayo kama sehemu ya kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi.
Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia leo tarehe 16 - 23/06/2023.
0 comments:
Chapisha Maoni