Mwandishi Wetu Harare Zimbabwe.
Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe Mheshimiwa Suzan Kaganda, amewasili Nchini humo tayari kuanza majukumu yake katika Balozi hiyo huku akiwaomba watumishi kushirikiana ili kutimiza azima ya viongozi wa Nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali.
Ametoa kauli hiyo leo Mei 05, 2025, Jijini Harare wakati alipowasili kwa mara ya kwanza na alipofanya kikao na maafisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe ambapo amesisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi na tija kwa mataifa hayo.
Balozi Kaganda ameongeza kuwa, matarajio ya viongozi wakuu wa Tanzania na Zimbabwe wanategemea kuona Balozi hizo zinaleta matokeo chanya na kutangaza fursa zilizopo katika nchi hizo.
Vilevile amesisitiza kuwa, ni vyema kudumisha umoja uliopo baina ya maafisa katika kutekeleza sera ya Mambo ya Nje.