Mradi mkubwa wa ujenzi wa Daraja la JPM linalounganisha wilaya ya Misungwi na wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza umefikia asilimia 99 ili kuweza kukamilika .
Hayo yamesemwa na msemaji mkuu wa Serikali Greyson Msigwa mara baada ya kufanya ziara katika Daraja hilo na kujionea hatua ya ujenzi iliyofikiwa ambapo kwasasa yamebakia marekebisho madogo ili kukamilika
Msigwa pia amesema kuwa daraja hilo litakuwa na uhai wa miaka mia moja ambapo siku nyingi litaanza kufanya kazi ili kuondoa changamoto ya wananchi kusubiri kivuko kwa muda mrefu
Aidha kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa ujenzi huo Mhandi Wiliam Sanga kutoka Tanroad amesema kuwa tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi huo jumla ya ajira 33505 ambapo wazawa ni asilimia 91.9 ambapo mpaka sasa wamemlipa mkandarasi shilingi Bilioni 539 .
Katika ziara hiyo ya Msemaji mkuu wa serikali ametembelea na kukagua pia mradi wa ujenzi wa vivuko 5 vinavyojengwa na Songoro Marine pamoja ujenzi wa meli ya Mv Mwanza.