JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Alhamisi, 22 Mei 2025

DKT. NATU MWAMBA ATETA NA BALOZI WA IRELAND NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na  Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Ireland. 


Dkt. Mwamba aliishukuru Serikali ya Ireland kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania kupitia ufadhili wa programu mbalimbali za maendeleo, zikiwemo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) na Mfuko wa Pamoja wa Afya (Health Basket Fund).

Kwa upande wake, Balozi wa Ireland alishukuru kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili na akasisitiza kuwa Ireland itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kufanikisha malengo ya pamoja ya maendeleo.


Aidha, viongozi hao walijadili kwa kina maoni na maazimio yaliyotokana na Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika tarehe 28 Februari 2025, Hazina-Dodoma, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa maazimio ya mkutano huo.

Katika kikao hicho, Mhe. Balozi Nicola Brennan, aliambatana na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini, Bi. Mags Gaynor na Meneja Programu anayesimamia masuala ya Uchumi Jumuishi, katika Ubalozi wa nchi hiyo, Bw. Francis Sampa na kwa upande wa Tanzania alikuwepo pia Bw. Norbert Mwitta, Mchumi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha.

 




0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio