JSON Variables

Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts

Tuesday, April 29, 2025

MALIASILI SC YATIKISA SINGIDA.


Na Sixmund Begashe 

Club ya Michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii maarufu kama MNRT SPORTS CLUB imeibua gumzo la shangwe Mkoani Singida kwenye mashindano ya Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Duniani MEI MOSI 2025, Mkoani Singida, kutokana ushujaa wa timu zake hususani timu ya mchezo wa kuvuta kamba wanaume iliyofanya vizuri mpaka mwisho.

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Singida na viunga vyake wamesikika wakiwapongeza wachezaji wa timu za Club hiyo yenye wachezaji wenye mbinu na ujuzi mkubwa, kwa kupambana vikali kwenye michuano hiyo hali inayoleta hamasa ya watu kupenda michezo na burudani ya aina yake.

Akizungumza na Maliasili Media, Bi. Mwantum Shabani wa Manyoni Singida amesema japo timu ya Maliasili Sports Club Wanaume Kamba imeshika nafasi ya pili lakini imeonesha upinzani mkali dhidi ya timu zingine pinzani.

" Singida kama burudani tumepata, mimi timu yangu ilikuwa Maliasili, si kwa sababu tu wanatulindia Maliasili zetu na kutuletea mapato kupitia Utalii, pia kwa namna walivyojipanga kwenye michezo hii, yaani ukishangilia hii timu haikuangushi, najivunia kuona wameibuka na Kombe hili naamini mwakani watakuwa washindi wa kwanza". Aliongeza Bi. Shabani.

Akizungumzia mashindano hayo makubwa hapa nchini, Mwenyekiti wa MNRT SPORTS CLUB Bw. Gervas Mwashimaha ameushukuru uongozi wa Wizara hiyo kwa kuiunga mkono club hiyo hali iliyowatia moyo na hari kubwa Kipindi chote cha michuano hiyo na kuahidi kuendelea kufanya vyema zaidi katika michezo mingine watakayo shiriki.

Katika mchezo wa Fainali wa Kamba wanaume, timu ya Maliasili imeshika nafasi ya pili dhidi ya timu 47 zilizoshiriki mashindano hayo huku timu ya Uchukuzi wanaume Kamba ikishika nafasi ya kwanza. 

Monday, April 28, 2025

RAIS SAMIA IPONGEZA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE KWA KUFUZU KATIKA MASHINDANO YA FUTSAL KWA AFRICA


 Hongereni wanangu Timu ya Taifa ya Wanawake katika Mchezo wa Futsal kwa kufuzu kuingia fainali ya mashindano hayo kwa Bara la Afrika, na wakati huo huo kufuzu kucheza Mashindano ya Kombe la Dunia la Futsal kwa Wanawake 2025 ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), yatakayofanyika huko Manila, Ufilipino baadaye mwaka huu. 

Nimefurahishwa na juhudi na nidhamu yenu katika mashindano haya. Ushindi wenu ni heshima kwa nchi yetu, na hamasa zaidi kwa watoto wa kike kushiriki katika michezo, si tu kwa burudani lakini pia kama ajira. Ninawapenda na ninawatakia kila la kheri.


Sunday, April 27, 2025

SIKU HAZIGANDI HATA UKIZIWEKA KWENYE FRIJI

 

Macho na akili za mashabiki wa mpira wa miguu nchini tanzania na duniani kote waliokuwa wakiisubilia siku ya leo tarehe 27.04.2025 kuushuhudia mtanange wa maamuzi makubwa sana , Baadhi ya mashabiki wa club ya Simba wamesema wapotayari kufanya chochote na popote imradi timu yao iweze kushinda


Juma hamis ni mkazi wa Temeke Mwembeyanga anasema yeye ni mnazi wa club ya Simba na leo hii simba anaibuka na ubingwa na kusonga kwenye fainali kisha kurudi na kombe nyumbani baada ya ushindi katika fainali itakayo fanyika baada ya Simba kushinda mechi ya leo ninafuraha sana kwa sababu hii siku niliisubilia kwa hamu sana nimeamini kwamba SIKU HAZIGANDI HATA UKIZIWEKA KWENYE FRIJI


Kwa upande wake Rose Anthony mkazi wa Dodoma ambaye yeye ni shabiki kindaki ndaki wa club ya Young Africans, Amesema watani wetu wameweza kupiga hatua kubwa sana kufikia hii leo kiasi kwamba ninawivu sana kwaajili yao, japokua mimi ni shabiki wa yanga sina kinyongo na watani wetu wa jadi kwa sababu wanacho kifanya wanaiwakilisha Taifa kiujumla kwa hiyo sina budi kuwa shabikia katika michuano hii ya kimataifa, wamalize salama waje na kombe nyumbani lakini wajue kwamba kwenye ligi yetu ya NBC sisi ndiyo mabingwa licha ya viporo walivyo bakisha


BIG SCREEN ya kumuangalia Mnyama akitinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika inakusubiri pale viwanja vya Mbagala Zakhiem. Mo Cola wamesimamia mpango mzima kufanikisha hili.

NJE SPORTS YAICHABANGA WIZARA YA AFYA

 

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) imeendelea kuonesha ubora mkubwa kwa kuichapa Wizara ya Afya na kufuzu hatua ya nusu fainali katika mchezo wa mashindano ya Mei Mosi uliopigwa katika uwanja vya Airtel, eneo la Mtipa mkoani Singida. 


Mchezo huo uliokuwa wa kuvutia, ulimalizika kwa sare ya 1-1 katika dakika 90 za kawaida ambapo mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penati na Nje Sports iliibuka kidedea kwa penati 4-2.


Kocha Mkuu wa Nje Sports, Bw. Shaban Maganga, ameonyesha furaha yake kutokana na juhudi kubwa za wachezaji wake waliopambana hadi mwisho wa mchezo. Ameeleza kuwa nidhamu na utekelezaji mzuri wa maelekezo ndio silaha ya ushindi wao.


"Nawapongeza wachezaji kwa kuonesha nidhamu na kufuata maelekezo, ndiyo siri ya ushindi wetu leo. Tunaendelea kujiandaa zaidi kwa nusu fainali." Alisema kocha Maganga.


Mwenyekiti wa timu, Bw. Ismail Abdallah, naye hakuficha furaha yake, akieleza kuwa ari ya wachezaji na sapoti waliyoipata kutoka kwa uongozi wa wizara ndiyo iliyowasaidia kupata matokeo mazuri.


"Wachezaji wameonyesha juhudi kubwa. Salamu za hamasa tulizopokea leo kutoka kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara yetu zimewapa nguvu ya ziada. Tunapambana hadi kulichukua kombe," alisema.


Mashindano haya ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi kitaifa, yakihamasisha mshikamano na afya miongoni mwa watumishi wa umma.

Wednesday, April 23, 2025

NJE SPORTS YATINGA ROBO FAINALI KWA KISHINDO, YAILAZA TPDC 36-23

 

Timu ya netiboli ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (NJE Sports) imeendelea kung’ara katika michezo ya Mei Mosi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 36-23 dhidi ya TPDC, katika mchezo uliopigwa kwenye viwanja vya Mwenge, mkoani Singida.


Mchezo huo ulianza kwa kasi, huku NJE Sports wakionyesha ubora wa hali ya juu na kumaliza kipindi cha kwanza wakiongoza kwa mabao 19-13. Kipindi cha pili walizidi kuimarika, wakiboresha safu ya ulinzi na kushambulia kwa ufanisi zaidi.


Akizungumza baada ya mchezo, Kocha wa NJE Sports, Bw. Mathew Kambona, amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma na kufuata maelekezo. “Tunajipanga upya kwa hatua inayofuata, tukilenga kuongeza kasi na nidhamu ya ushindi,” alisema.


Kwa matokeo hayo, NJE Sports imefuzu rasmi hatua ya robo fainali katika mashindano hayo ya kitaifa yanayoshirikisha timu kutoka wizara na taasisi mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

MH. S. S. H, AMPONGEZA ALPHONCE BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA PILI KWENYE MBIO ZA BOSTON

 

Pongezi za dhati kwa Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Mbio ya Boston (Boston Marathon). Umefanya kazi nzuri.


Ushindi wako ni matokeo ya kujituma kwa bidii, maandalizi mazuri, nidhamu yako kuanzia jeshini, kwenye mazoezi hadi kwenye mashindano, ukilibeba kwa heshima ya hali ya juu jina la nchi yetu. 


Endelea kuipeperusha vyema bendera ya Taifa letu.

Sunday, April 20, 2025

MALIASILI SC YAIBURUZA TAMISEMI 2-1

.......

Na Sixmund Begashe

Timu ya Wanawake ya mchezo wa kuvuta kamba ya MNRT Sports Club ya Wizara ya Maliasili na Utalii, imeiburuza vikali 2-1 timu ya TAMISEMI wanawake katika mchezo wa marudiano uliofanyika leo Mkoani Singida kwenye mashindano ya Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Duniani (MEI MOSI 2025).

Wakizungumzia michezo hiyo inayoshika kasi Mjini Singida, mashabiki mbalimbali wamesikika wakisema kuwa mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto mkubwa kutokana na timu za Wizara hiyo inayojishighulisha na Uhifadhi na Utalii nchini kuwa moto mkali kwa timu zingine pinzani.

"Hawa wachezaji wa Maliasili, sijui mwaka huu wamekula nini, wamekuwa na nguvu zaajabu mithili ya tembo wa Tarangire, hii inatupatia rahaa sana, wameleta changamoto kubwa kwa timu pinzani" alisema Bw. Ally Ramadhan, mkazi wa Gidasi Manyara.

Katika mchezo uliochezwa jana jioni timu ya Mpira wa Miguu wanaume iliwalegezea nguvu wapinzani wao timu ya Ardhi na kuwapa heshma ya sare (0-0), huku Mwenyekiti wa Club hiyo Bw. Gervas Mwashimaha, amesema bahati ya zawadi ya Sikukuu ya Pasaka waliyoipata timu ya Ardhi isitegemewe kwa timu nyingine yeyote kwenye michezo hiyo itakayofikia kilele chake siku moja kabla ya sherehe za Mei Mosi 2025 Mkoani Singida.

 

Thursday, April 17, 2025

NJE SPORTS YAICHAPA WIZARA YA UJENZI 1-0 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI SINGIDA



Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Wizara ya Ujenzi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Mwenge, mkoani Singida.


Mchezo huo, ambao ulikuwa na ushindani mkubwa na nidhamu ya hali ya juu kutoka kwa timu zote mbili, ulikuwa sehemu ya maandalizi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yanayotarajiwa kufanyika Mei Mosi, 2025.


Bao pekee la Nje Sports lilifungwa katika kipindi cha pili na mshambuliaji Juma Jongo, aliyepokea pasi safi kutoka kwa kiungo Mukrim, baada ya shambulizi la pamoja lililotokana na umiliki mzuri wa mpira katikati ya uwanja.


Licha ya juhudi za Wizara ya Ujenzi kusawazisha bao hilo, safu ya ulinzi ya Nje Sports ilionyesha uimara mkubwa, huku kipa wao Adam Mlele akiokoa michomo kadhaa ya hatari na kudhihirisha uwezo mkubwa langoni.


Timu hizo zipo mkoani Singida kushiriki michezo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu.

Tuesday, March 25, 2025

YANGA WANAHANGAIKA NA TFF ,SIMBA YAJA NA MPANGO KABAMBE DHIDI YA AL MASRY

 Wakati mjadala mzito wa kuahirishwa ukiendelea kuunguruma miongoni mwa mashabiki wa soka nchini ,hali ni tofauti kwa uongozi wa klabu ya Simba. Uongozi wa klabu hiyo umejikita kuimarisha ushirikiano na mashabiki wake kuelekea mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry yanchini misrimchezo wa raundi ya kwanza utakaopigwa April 2.

Simba wamekaa kimya katika sakata hilo na kuwaacha wapinzani wao wa jadi Yanga waendelee kupambana na Bodi ya Ligi na TFF wakati wao wakiendelea na mazoezi makali kwa ajili ya mchezo huo muhimu unaoweza kwenda kubadili historia ya klabu hiyo. 


Simba yaja na mbinu za kivita kuelekea mchezo wa April 2

Uongozi wa Simba unaamini utulivu ndiyo msingi wa mafanikio ya klabu yao, Klabu hiyo ni mnufaaika mkubwa wa mashabiki wake hasa linapokuja suala la mechi za kimataifa.Si Al Ahly,Zamalek,Kaiser Chief wala Asec Mimosa anayependa kuja dimba la Benjamini mkapa kwa sababu mashabiki wa Simba wamekuwa wakileta msisimko wa kipekee kwa wachezaji wao na kuwapoteza wapinzani wao.

Kuelekea michezo ya tarehe 02 na 09 April Simba imeanza kampeni zake za kuwaweka pamoja mashabiki na hilo limefanyika kwa kuanza na kampeni ya WESE LA UBAYA UBWELA inayowataka mashabiki wa Simba kujaza mafuta katika vituo vya Lake Energies na kufanya hivyo kutainufaisha klabu kwa mapato yatakayokusanywa.


naye msemaji wa klabu hiyo Bw.Ahmed Ally amenukuliwa akisema “Hii ni bidhaa mpya ambayo Simba na Lake Energy tumeingiza sokoni. Bidhaa hii inaweza kutumiwa na Wanasimba na watu wengine. Lakini pia ni mpango maalumu wa kujitengenezea mapato. Kwa kufahamu kwamba uhitaji wa mafuta ni mkubwa nchini, Simba Sports Club tukaiona fursa kushirikiana na Lake Energy ili kuwahudumia Wanasimba lakini pia kuwawezesha kuchangia klabu yao lakini pia kwa Lake Energy kurudisha kwa Jamii.”

“Kwenye vituo vyote vya Lake Energies kutakuwa na namba maalumu au sehemu ya ku’scan’ na ukishaweka mafuta utawambia unalipa kwa njia ya mtandao iwe kwa benki au mitandao ya simu. Huduma hii inafanya kazi kwa njia ya mtandao tu na kila lita unayoweka kuna asilimia inakuja Simba.”
“Jukumu la kuipatia mapato Simba ni jukumu la kila Mwanasimba hivyo kuanzia sasa kwa kila Mwanasimba, kituo chake cha kuweka mafuta ni Lake Energies. Na ukilipa tumia njia ya mtandao, ukilipa kwa cash hiyo siyo yetu lakini ukilipa kwa mtandao tunapata chetu, tunakwenda kuwalipa kina Chasambi, kina Mpanzu wanakwenda kutufanyia ubaya.”

REAL MADRID HAWANA MUDA WA KUPOTEZA WAKIKUHITAJI

 Mlinzi wa pembeni wa Liverpool na England Trent Alexander-Arnold, 26, amekubaliana na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano na atajiunga na wababe hao wa Uhispania bila malipo. (Sky Sports)



Real pia inamfuatilia winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 22, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 62m (£51.8m), iwapo nyota wa Brazil Vinicius Jr, 24, atajaribiwa na uhamisho wa kitita kinono kwenda Saudi Arabia. (Fichajes)

Manchester United inapanga kuwaruhusu wachezaji 10, akiwemo mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 33 - kuondoka kabisa katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)

United pia inamtazama mchezaji wa Fenerbahce Yusuf Akcicek, 19, katika kutafuta mlinzi mwingine wa kati, ingawa Tottenham Hotspur, Bayern Munich, Atletico Madrid, Napoli na RB Leipzig pia wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Mirror)

Barcelona wanatazamia kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle na Italia Sandro Tonali, 24, pamoja na ofa inayoweza kumnunua mchezaji mwenza wa klabu hiyo, mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25. (Mundo Deportivo)

Mlinzi Muingereza Jarrad Branthwaite, 22, anafikiria hatma yake katika klabu ya Everton huku Manchester United na Liverpool zikimtaka. (Mirror)

Jarrad Branthwaite

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tottenham Hotspur wametoa ofa ya mapema kwa kiungo wa kati wa Sunderland Chris Rigg kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi, kwa dau la pauni milioni 37 kumnunua Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 17. (Fichajes)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong anataka kusalia katika klabu hiyo na yuko kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ukiisha 2026. (NY Times)

Mustakabali wa kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 20, katika Chelsea haujulikani, lakini anatumai kuungana tena na mchezaji mwenzake wa kimataifa Estevao Willian katika klabu hiyo ya London baada ya muda wake wa mkopo Strasbourg. Willian, 17, atajiunga na The Blues mwezi Julai kutoka Palmeiras. (Evening Standard)

Winga wa zamani wa Liverpool na Rangers Ryan Kent yuko kwenye mazungumzo ya juu ya kujiunga na Seattle Sounders inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka. Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mchezaji huru baada ya kuachana na Fenerbahce ya Uturuki Oktoba mwaka jana. (Sounder at heart)

MALENGO YA PEDRI NI TOFAUTI KABISA NA MBAPPE

 Wakati Mbappe akiota kutwaa Ballon d or hali hi tofauti kwa kiungo mahiri wa FC Barcelona  Pedri ambaye  amezungumza wazi kuhusiana na tuzo ya kifahari ya Ballon d’Or. Licha ya kuwa alishinda Kombe la Kopa mnamo 2021 na kukosa uteuzi wa 30 bora wa mwaka huu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 tayari anaonekana kama mshindani mkubwa wa tuzo hiyo katika msimu huu.

 Amekuwa katika kiwango cha hali ya juu, akicheza mechi 42 katika mashindano yote msimu huu, akichangia kwa mabao 5 na kusaidia 7. Katika hafla ya hivi majuzi iliyofanyika ili kuzindua kitabu chake cha katuni, "Pedri and the Legend of the Golden Shoe", aliviambia vyombo vya habari kwamba mafanikio ya timu ni muhimu kuliko heshima ya mtu binafsi.

 "Ningependelea kushinda mataji matatu kuliko Ballon d'Or," alisema. "Iwapo inakuja, iwe hivyo, lakini mataji ya pamoja ni muhimu zaidi kwangu. Kuteuliwa ni ndoto, lakini kushinda vikombe ni muhimu. Tuko katika wakati ambapo kila kitu kiko hatarini. Unaweza kupoteza mechi tatu na kuondolewa kwenye mashindano matatu."

 Mtazamo huu ni wa kustaajabisha sana, hasa ikizingatiwa nia kali ya nyota wa soka kutwaa tuzo ya Ballon d’Or, iliyodhihirishwa na wachezaji kama Kylian Mbappé, ambaye anaichukulia hadharani tuzo hiyo kama lengo kuu la kibinafsi.

JUVENTUS YAMFANYIA UBAYA UBWELA THIAGO MOTTA

  Taarifa mpya zimeibuka kuhusu kutimuliwa kwa Thiago Motta katika wadhifa wake kama kocha mkuu wa klabu ya Juventus ya Turin, na kutoa mwanga kuhusu hali iliyopelekea klabu hiyo kutoa uamuzi wa mwisho na taarifa kwa kocha huyo.

Kulingana na gazeti la La Gazzetta dello Sport, Thiago Motta alifahamu kuhusu kufukuzwa kwake wakati alipopigiwa simu. Wakati huo, alikuwa akifurahia likizo huko Ureno na familia yake.

Kando na Motta, sehemu ya wakufunzi wake pia waliondoka katika klabu hiyo, wakiwemo wasaidizi sita waliojitolea ambao walijiunga naye miezi minane iliyopita.

Msaidizi mpya wa kocha mkuu wa Juventus, ambaye sasa ni Igor Tudor, atakuwa Ivan Yavorchic, ambaye hapo awali alifanya kazi pamoja na mtaalamu huyo mwenye umri wa miaka 46 huko Lazio.

HILI NI ANGUKO KUU KWA GIGGS,AMEANZA KUFILISIKA?

 Ryan Giggs anadaiwa mshahara wa pauni 40,000 kwa wafanyakazi baada ya mgahawa wake kuharibiwa ghafla.Takwimu mpya zinaonyesha kuwa wafanyakazi 22 wanamdai nyota huyo baada ya kuacha kazi Biashara hiyo inadaiwa jumla ya £495,145 kulingana na Taarifa rasmi kuhusu kuanguka kwa kampuni iliyowasilishwa kwa Companies House siku chache zilizopita.


Mgahawa wa George's Dining Room na Baa yake iliyo karibu na , karibu na Manchester, vilifungwa 'papo hapo' mnamo Februari na biashara nyingine zilifutwa kwa hiari.HMRC inadaiwa takriban £117,000 kwa michango ya kodi na Bima ya Kitaifa, kuna bili ya gesi ya £15,000 na £35,000 kwa benki ya Nat West.

Ryan Giggs alifungua mgahawa na marafiki zake Kelvin Gregory na Bernie Taylor mnamo 2014 .Taylor anadaiwa karibu £13,000 na Gregory zaidi ya £53,000.Giggs hapo awali alizungumza kuhusu jinsi ukumbi huo ulivyotimiza moja ya ndoto zake za maisha ya kufungua mgahawa na marafiki zake wa shuleni . Watatu hao walikuwa wamesema walitaka kusaidia kufanya Worsley kuwa 'sehemu sahihi kwa chakula'.

Ryan alisema wakati huo, 'Tumefahamiana kwa miaka 30, na kila mara tulisema itakuwa nzuri kufanya kitu kama hiki pamoja.'Sisi sote ni vijana wa ndani na tumeishi katika eneo hili maisha yetu yote kwa hivyo tulitaka kufanya kitu huko Worsley na tunafikiri tuna toleo tofauti kabisa kwa eneo hilo.'

Tangu alipozindua George's, Ryan pia ameungana na mchezaji mwenzake wa zamani Gary Neville na kuunda kundi la GG likiwa na maana Gigs and Garry lenye umiliki wa Hoteli huko Old Trafford, na kisha Hoteli ya nyingine iko katika Soko la Hisa katikati mwa jiji.

Monday, March 24, 2025

URENO YAISAMBARATISHA DENMARK IKITINGA NUSU FAINALI KIBABE

 Timu ya Taifa ya Ureno chini ya Kapteni Cristiano Ronaldo imefanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Denmark. Mchezo huo mgumu uliopigwa dimba la Estádio José Alvalade nchini Ureno uliibua hisia kwa mashabiki wa soka duniani kote baada ya Cristiano Ronaldo kukosa penati muhimu lakini alisahihisha makosa hayo na kufunga bao muhimu.


Tathmini ya Mchezo

Ureno waliingia vichwa chini katika mchezo huo baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao 1-0 nchini Denmark  kwa bao la mshambuliaji kinda Hojlund. Ureno walianza mchezo huo kwa mashambulizi makali na kujipatia penati dakika ya 6 lakini mpigaji  Cristiano Ronaldo alishindwa kufunga baada ya golikipa wa Denmark Kasper Schmeichel kudaka mpira mwepesi.

Ureno walizidisha mashambulizi na dakika ya 38 Joachim Andersen wa Denmark alijifunga na kuwafanya Ureno kwenda mapumziko kwa bao 1-0. Dakika ya 56 Rasmus Kristen wa Denmar  alifanikiwa  kusawazisha bao.

Dakika ya 72 Ronaldo alirejesha furaha kwa mashabiki wa Ureno kwa kufunga bao la pili na kusawazisha makosa ya kukosa penati lakini Cristien Eriksen alisawazisha bao hilo dakika ya 76 na matokeo kuwa 2-2.

Kocha wa Ureno alifanya mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wote wakiongozwa na Ronaldo ,Rafael Leao na na kuwapa nafasi Trincao aliyefunga mabao mawili ya dakika ya 86 na 91kisha bwana mdogo goncalo Ramos kufunga bao la 5 dakika ya 115 na kuwaondosha Denmark kwenye michuano hiyo.

Matokeo hayo yanawafanya Ureno kutinga nusu fainali ya Ligi ya ulaya wakichuana na Ujerumani katika hatua hizo,kama watashinda mchezo huo basi watatinga fainali ya michuano hiyo

Thursday, March 20, 2025

KUMBE TONI KROOS ALISHAJIPANGA KABLA YA KUSTAAFU,UTAJIRI WAKE NI GUMZO

 Mara baada ya kustaafu soka la kulipwa Toni Kroos amefanikiwa kuingia ubia na kampuni ya Sports 360 ambayo ilisimama kama wakala wake akiwa mchezaji wa vilabu mbalimbali ikiwemo Real Madrid na Bayern Munich. Mara baada ya kusaini mikataba ya kununua sehemu ya hisa za kampuni hiyo nyota huyo wa zamani wa tiu ya taifa ya Ujerumani alinukuliwa akisema  "Ninafuraha kutoa ushauri kwa baadhi ya wachezaji kwenye safari zao za michezo na kushiriki uzoefu wangu."


Tangu atangaze kustaafu soka la kulipwa msimu uliopita, Toni Kroos ameanzisha miradi kadhaa kama 

▪️ Klabu ya Soka ya Grassroots: Alianzisha klabu ya soka ya ngazi ya chini inayoitwa 'Toni Kroos' mjini Madrid, kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka la Kifalme la Madrid na Klabu ya Las Encinas Boadilla.

▪️Ligi ya Picha: Alizindua 'The Icon League', mseto wa soka na burudani, inayoakisi mbinu yake ya ubunifu kwa mchezo.

. Academy: Alifungua akademia mpya huko Madrid, kwa sasa anafundisha zaidi ya watoto 200, akisisitiza maendeleo ya vijana.

Zaidi ya mipango hii, Kroos amebadilisha uwekezaji wake:

▪️Majengo: Mnamo 2020, alianzisha Kroos Properties XXI SL, kampuni ya mali isiyohamishika iliyoko Madrid.

▪️Kuanzisha Uwekezaji:

📊 Alipata takriban 14% ya kampuni ya kuanzia ya kukodisha magari yenye makao yake makuu mjini Berlin, Duke.

📊 Aliwekeza katika HMNC Brain Health, kampuni ya dawa mfadhaiko iliyoanzishwa pamoja na Carsten Maschmeyer.

📊 Ana karibu asilimia 3 ya hisa katika kampuni ya afya inayoanzisha Rebirth Active.

▪️Mapendekezo: 

📊 Ameshirikiana na chapa kama Adidas na Hugo Boss, akiboresha uwepo wake nje ya uwanja

WALLACE KARIA NA ENG.HERSI WAZIDI KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA

 Siku chache zilizopita Rais wa klabu ya Yanga Hersi Saidi alikuwa nchini Morocco yaliko makao makuu ya CAF kusaini mkataba wa ushirikiano baina ya CAF pamoja na Chama cha vilabu Afrika (ACA) akiwa kama mwenyekiti wa chama hicho cha vilabu.

Lakini pia Raisi Hersi aliungana na Raisi wa TFF Wallace Karia wakati wa uchaguzi wa mkuu wa CAF na Patrick Motsepe kuchaguliwa kwa mara ya pili kuwa raisi wakati Wallace Karia akichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CAF. Kwa matukio haya Tanzania tunaendelea kupeperusha vyema bendera ya Soka 


Kwani raisi wa Yanga yuko wapi

 Wakati nchi nzima ikilaani na kulalamikia maamuzi ya Bodi ya Ligi kuahirisha mchezo baina ya Yanga na Simba uliopangwa kufanyika tarehe 8 machi mambo ni tofauti kwa raisi wa klabu ya Yanga Hersi Said. Kwanza hajatoa tamko lolote mpaka sasa kuzungumzia tukio hilo na mchezo huo pili yupo nchini Hispania akiendelea na majukumu yake ya Shughuli za usimamiaji wa chama cha vilabu Afrika (Africa Clubs Association) akiwa yeye ndiye mwenyekiti.

Haya ni maendeleo makubwa kwa soka letu na uweledi wa viongozi hawa umeendelea kuinua soka letu la Tanzania


Rais Hersi Saidi ameutumia mtandao wake kwa kuandika haya

''Kama Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu vya Kiafrika, kuhudhuria hafla ya Jumuiya ya Vilabu ya Ulaya huko Madrid sio tu heshima bali ni fursa muhimu ya kujifunza na kuunganishwa na vilabu vya Uropa. 

Kushirikiana na washikadau wakuu katika jumuiya ya soka huturuhusu kubadilishana mawazo, mbinu bora, na mikakati bunifu inayoweza kuinua vilabu na michezo yetu katika bara la Afrika. 

Kwa pamoja, tunaweza kukuza ushirikiano, kuongeza ukuaji, na kuhamasisha kizazi kijacho cha vipaji vya soka. Furahi kwa majadiliano mbele!''

ACA kukutana na ECA!


SALEH JEMBE: NI WAKATI SAHIHI KWA MATOLA KUACHANA NA SIMBA

  Kocha Pitso Mosimane aliamua kumsajili Selemani Matola katika kikosi cha Super Sport ya Afrika Kusini bila ya majaribio. Katika mahojiano yangu naye mwaka 2006, alisema hakukuwa na haja wakati huo kumjaribu tena Matola sababu mechi mbili Simba Vs Asante Kotoko ya Ghana na Tusker ya Kenya ambao wote walifungwa na Simba katika nusu Fainali na Fainali ya Tusker Cup, Matola alikuwa nyota wa mchezo.


Kwa sasa Matola ni mmoja wa makocha bora wazalendo licha ya kwamba wangeweza kuwa bora zaidi wakishika usukani wa kocha Mkuu.
Matola kajifunza mengi kupitia Simba akiwa msaidizi. Amesimama nyuma ya makocha wa nchi mbali mbali wenye filosofia tofauti na za aina tofauti. Hii inamfanya kuwa bora zaidi.
Licha ya kwamba amekuwa na DAMU YA KUNGUNI, Kila Simba ikiyumba anaangushiwa GARI BOVU lakini uhalisia sahihi yeye ni DARAJA katika ya klabu yake na makocha wa kigeni.
Amekuwa ndiye anayewaelekeza Simba inataka nini, upi ni utamaduni wa maisha ya soka la Simba lakini kwa wachezaji ni Imani naye kubwa na taarifa za uwezo wake kwa kuwa akiwa nahodha aliwahi KUIVUA ubingwa wa Afrika na UBORA wa Afrika Zamalek. Tena jijini Cairo.
Angekuwa si MZAWA angeonekana BONGE LA KOCHA, uzalendo wake umekuwa ADHABU KWAKE lakini amebahatika KHERI ya SUBRA na kuna siku asipokuwepo Simba.... Watu wengi WATATAMANI arejee kwa kuwa yeye ni Simba kuanzia JEZI YENYE JASHO UWANJANI na sasa ni MAPAMBANO KWENYE BENCHI.

RONALDO AFUNGUKA NAMNA WABRAZIL WALIVYOMUHUJU

 Ronaldo (Luís Nazário de Lima) ameamua kujitolea kwa kazi yake katika mpira wa miguu. Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa zamani wa "Inter", " AC Milan", "Real Madrid", na "Barcelona" aliona kuwania kwake urais wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) kushindikana kutokana na mradi wake mkubwa kuzuiwa kutokana na kukosa kuungwa mkono na mashirikisho ya serikali.



 Licha ya hadhi yake ya hadithi na hamu ya kuunganisha nchi karibu na wazo la kawaida, "El Fenômeno" alilazimika kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho, akisema kuwa mashirikisho 23 kati ya 27 ya ndani yalikataa hata kumsikiliza, na hivyo kuandaa njia ya kuteuliwa tena kwa rais wa sasa Ednaldo Rodrigues.

''Baada ya kutangaza hadharani nia yangu ya kugombea urais wa CBF katika kikao cha mashauriano, niliondoa dhamira yangu rasmi. Iwapo walio wengi ambao wana haki ya kufanya maamuzi wanaamini kwamba soka la Brazil liko mikononi mwa kuaminika, maoni yangu hayana umuhimu mkubwa.''

Wazo langu lilikuwa kutoa sauti na nafasi kwa vilabu, pamoja na kusikiliza mashirikisho ya ndani ili kuboresha ushindani na maendeleo ya mchezo katika mikoa yote. Hata hivyo, wakati wa mawasiliano yangu ya kwanza na wanachama 27, nilikuta milango 23 imefungwa... Mashirikisho yalikataa tu kunikubalia na kunisikiliza, kwa madai kuwa wameridhishwa na utawala uliopo na wanaunga mkono uchaguzi wake wa marudio.

Sikuweza kuwasilisha mradi wangu kama nilivyotaka. Hakukuwa na fursa ya mazungumzo. Sheria inayapa mashirikisho kura nyingi, na kwa hivyo ni wazi kwamba hakuna njia ya kufikia makubaliano. Viongozi wengi wa majimbo wanamuunga mkono rais wa sasa. Hii ni haki yao, na ninaiheshimu, bila kujali imani yangu, - Ronaldo alisema.

Inafurahisha, hali kama hiyo ilitokea katika uchaguzi wa rais wa Chama cha Soka cha Kiukreni. Kumbuka kwamba huko Ukraine, UAF imekuwa ikiongozwa na Andriy Shevchenko tangu Januari 2024, ambaye alichukua nafasi ya binamu yake Andriy Pavelko kabla ya ratiba. Wanasoka wengine maarufu, akiwemo Roman Zozulia, pia walitarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo. Walakini, walieleweka kuwa ugombea wa Shevchenko ulikubaliwa kwa kiwango cha juu zaidi, na mwishowe, Andriy Mykolyovych aligeuka kuwa mgombea pekee, bila washindani katika mbio hizo.

MOTO UMEANZA KUWAKA NDANI YA CHELSEA TAJIRI AMEKASIRIKA

 Chelsea inaweza kuuza hadi wachezaji 11 msimu huu wa joto - ikiwa ni pamoja na Waingereza wawili, mshambuliaji Raheem Sterling, 30, na beki mwenye umri wa miaka 28 Ben Chilwell - ili kupata fedha za kununua mshambuliaji mpya. (Mail)


Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Muitaliano Moise Kean, 25, ambaye hapo awali alikuwa na msimu usio na mafanikio katika klabu ya Everton. (Tuttomercatoweb)

Manchester United imeongeza washambuliaji wawili wa Bundesliga - Mslovenia wa RB Leipzig Benjamin Sesko, 21, na Mfaransa wa Eintracht Frankfurt Hugo Ekitike, 22 - kwenye orodha ya wachezaji itakaowasajili katika majira ya joto. (Sky Sports)

Man Utd pia wanavutiwa na kiungo wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 21, ambaye walijaribu kumsajili huko nyuma kabla ya kuhamia Ujerumani kwa mkataba wa kudumu katika dirisha la Januari. (Sky Sports)

s

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Benjamin Sesko

Real Betis watakutana na Manchester United kujadili mustakabali wa winga Mbrazil Antony, 25, ambaye amefanya vyema katika kipindi cha mkopo katika ligi ya La Liga. (ABC)

Bournemouth wanamtaka beki wa kushoto wa Club Brugge raia wa Ubelgiji Maxim de Cuyper, 24, iwapo watahitaji kusajili mbadala wa beki wao wa pembeni wa Hungary Milos Kerkez, 21, ambaye anasakwa na Liverpool. (Football Insider)

Atletico Madrid wanasema mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 25, hauzwi kutokana na kuripotiwa kuwa anawindwa na Liverpool. (Kioo)

Winga wa Chelsea wa Uingereza Noni Madueke, 23, analengwa na klabu ya AC Milan ya Serie A katika majira ya msimu wa joto. (Fichajes)

Kiungo wa kati wa Lille na England Angel Gomes, 24, amegoma kwenda West Ham, licha ya klabu hiyo ya ligi kuu Enlgand kumpa mkataba wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki ili ajiunge nayo pale mkataba wake na Lille utakapomam=lizika msimu huu wa joto. (Guardian)

a

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Angel Gomes

Barcelona wanataka kumsajili tena mshambuliaji wa Argentina na Inter Miami Lionel Messi, 37, katika msimu wa joto wa mwaka 2026. (TNT Sports)

Beki wa Real Madrid Mhispania Raul Asencio, 22, anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na wababe hao wa Uhispania. (Fabrizio Romano)

Real Betis ni moja ya klabu tatu za La Liga zinazotaka kumsajili beki wa kushoto wa Leeds Junior Firpo, 28, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto wakati mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Dominika utakapomalizika. (Teamtalk).