JSON Variables

Tuesday, March 25, 2025

REAL MADRID HAWANA MUDA WA KUPOTEZA WAKIKUHITAJI

 Mlinzi wa pembeni wa Liverpool na England Trent Alexander-Arnold, 26, amekubaliana na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano na atajiunga na wababe hao wa Uhispania bila malipo. (Sky Sports)



Real pia inamfuatilia winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 22, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 62m (£51.8m), iwapo nyota wa Brazil Vinicius Jr, 24, atajaribiwa na uhamisho wa kitita kinono kwenda Saudi Arabia. (Fichajes)

Manchester United inapanga kuwaruhusu wachezaji 10, akiwemo mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 33 - kuondoka kabisa katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)

United pia inamtazama mchezaji wa Fenerbahce Yusuf Akcicek, 19, katika kutafuta mlinzi mwingine wa kati, ingawa Tottenham Hotspur, Bayern Munich, Atletico Madrid, Napoli na RB Leipzig pia wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Mirror)

Barcelona wanatazamia kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle na Italia Sandro Tonali, 24, pamoja na ofa inayoweza kumnunua mchezaji mwenza wa klabu hiyo, mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25. (Mundo Deportivo)

Mlinzi Muingereza Jarrad Branthwaite, 22, anafikiria hatma yake katika klabu ya Everton huku Manchester United na Liverpool zikimtaka. (Mirror)

Jarrad Branthwaite

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tottenham Hotspur wametoa ofa ya mapema kwa kiungo wa kati wa Sunderland Chris Rigg kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi, kwa dau la pauni milioni 37 kumnunua Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 17. (Fichajes)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong anataka kusalia katika klabu hiyo na yuko kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ukiisha 2026. (NY Times)

Mustakabali wa kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 20, katika Chelsea haujulikani, lakini anatumai kuungana tena na mchezaji mwenzake wa kimataifa Estevao Willian katika klabu hiyo ya London baada ya muda wake wa mkopo Strasbourg. Willian, 17, atajiunga na The Blues mwezi Julai kutoka Palmeiras. (Evening Standard)

Winga wa zamani wa Liverpool na Rangers Ryan Kent yuko kwenye mazungumzo ya juu ya kujiunga na Seattle Sounders inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka. Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mchezaji huru baada ya kuachana na Fenerbahce ya Uturuki Oktoba mwaka jana. (Sounder at heart)

MALENGO YA PEDRI NI TOFAUTI KABISA NA MBAPPE

 Wakati Mbappe akiota kutwaa Ballon d or hali hi tofauti kwa kiungo mahiri wa FC Barcelona  Pedri ambaye  amezungumza wazi kuhusiana na tuzo ya kifahari ya Ballon d’Or. Licha ya kuwa alishinda Kombe la Kopa mnamo 2021 na kukosa uteuzi wa 30 bora wa mwaka huu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 tayari anaonekana kama mshindani mkubwa wa tuzo hiyo katika msimu huu.

 Amekuwa katika kiwango cha hali ya juu, akicheza mechi 42 katika mashindano yote msimu huu, akichangia kwa mabao 5 na kusaidia 7. Katika hafla ya hivi majuzi iliyofanyika ili kuzindua kitabu chake cha katuni, "Pedri and the Legend of the Golden Shoe", aliviambia vyombo vya habari kwamba mafanikio ya timu ni muhimu kuliko heshima ya mtu binafsi.

 "Ningependelea kushinda mataji matatu kuliko Ballon d'Or," alisema. "Iwapo inakuja, iwe hivyo, lakini mataji ya pamoja ni muhimu zaidi kwangu. Kuteuliwa ni ndoto, lakini kushinda vikombe ni muhimu. Tuko katika wakati ambapo kila kitu kiko hatarini. Unaweza kupoteza mechi tatu na kuondolewa kwenye mashindano matatu."

 Mtazamo huu ni wa kustaajabisha sana, hasa ikizingatiwa nia kali ya nyota wa soka kutwaa tuzo ya Ballon d’Or, iliyodhihirishwa na wachezaji kama Kylian Mbappé, ambaye anaichukulia hadharani tuzo hiyo kama lengo kuu la kibinafsi.

JUVENTUS YAMFANYIA UBAYA UBWELA THIAGO MOTTA

  Taarifa mpya zimeibuka kuhusu kutimuliwa kwa Thiago Motta katika wadhifa wake kama kocha mkuu wa klabu ya Juventus ya Turin, na kutoa mwanga kuhusu hali iliyopelekea klabu hiyo kutoa uamuzi wa mwisho na taarifa kwa kocha huyo.

Kulingana na gazeti la La Gazzetta dello Sport, Thiago Motta alifahamu kuhusu kufukuzwa kwake wakati alipopigiwa simu. Wakati huo, alikuwa akifurahia likizo huko Ureno na familia yake.

Kando na Motta, sehemu ya wakufunzi wake pia waliondoka katika klabu hiyo, wakiwemo wasaidizi sita waliojitolea ambao walijiunga naye miezi minane iliyopita.

Msaidizi mpya wa kocha mkuu wa Juventus, ambaye sasa ni Igor Tudor, atakuwa Ivan Yavorchic, ambaye hapo awali alifanya kazi pamoja na mtaalamu huyo mwenye umri wa miaka 46 huko Lazio.

HILI NI ANGUKO KUU KWA GIGGS,AMEANZA KUFILISIKA?

 Ryan Giggs anadaiwa mshahara wa pauni 40,000 kwa wafanyakazi baada ya mgahawa wake kuharibiwa ghafla.Takwimu mpya zinaonyesha kuwa wafanyakazi 22 wanamdai nyota huyo baada ya kuacha kazi Biashara hiyo inadaiwa jumla ya £495,145 kulingana na Taarifa rasmi kuhusu kuanguka kwa kampuni iliyowasilishwa kwa Companies House siku chache zilizopita.


Mgahawa wa George's Dining Room na Baa yake iliyo karibu na , karibu na Manchester, vilifungwa 'papo hapo' mnamo Februari na biashara nyingine zilifutwa kwa hiari.HMRC inadaiwa takriban £117,000 kwa michango ya kodi na Bima ya Kitaifa, kuna bili ya gesi ya £15,000 na £35,000 kwa benki ya Nat West.

Ryan Giggs alifungua mgahawa na marafiki zake Kelvin Gregory na Bernie Taylor mnamo 2014 .Taylor anadaiwa karibu £13,000 na Gregory zaidi ya £53,000.Giggs hapo awali alizungumza kuhusu jinsi ukumbi huo ulivyotimiza moja ya ndoto zake za maisha ya kufungua mgahawa na marafiki zake wa shuleni . Watatu hao walikuwa wamesema walitaka kusaidia kufanya Worsley kuwa 'sehemu sahihi kwa chakula'.

Ryan alisema wakati huo, 'Tumefahamiana kwa miaka 30, na kila mara tulisema itakuwa nzuri kufanya kitu kama hiki pamoja.'Sisi sote ni vijana wa ndani na tumeishi katika eneo hili maisha yetu yote kwa hivyo tulitaka kufanya kitu huko Worsley na tunafikiri tuna toleo tofauti kabisa kwa eneo hilo.'

Tangu alipozindua George's, Ryan pia ameungana na mchezaji mwenzake wa zamani Gary Neville na kuunda kundi la GG likiwa na maana Gigs and Garry lenye umiliki wa Hoteli huko Old Trafford, na kisha Hoteli ya nyingine iko katika Soko la Hisa katikati mwa jiji.

WAFANYAKAZI WASHAURIWA KUWEKEZA KABLA YA KUSTAAFU

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Erick Mvati, akikabidhiwa vipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bw. Santley Kibakaya, vyenye mada mbalimbali ikiwemo akiba, mikopo na uwekezaji ambazo zitafundishwa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Erick Mvati, akiwasikiliza Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Erick Mvati, akizungumza alipokutana na Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Afisa Masoko Mwandamizi, Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS, Bw. Rahim Mwanga, akiwafungulia akaunti ya uwekezaji watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakifuatilia mada mbalimbali ikiwemo akiba, mikopo, uwekezaji, bima, kujiandaa kustaafu wakati wa  mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akiteta jambo na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, baada ya kumalizika kwa mafunzo ya elimu ya fedha kwa watumishi hao yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, akitoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Mwanza)

.........................

Na. Josephine Majura, WF, Mwanza 

Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi wameshauriwa kujifunza kuhusu uwekezaji mapema ili kuhakikisha kuwa baada ya kustaafu wanaendelea kuishi maisha mazuri, kama walivyokuwa kazini.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Masoko Mwandamizi, Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS, Bw. Rahim Mwanga, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa watumishi wa Halmashauri hiyo na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake.  

Aliongeza kuwa kustaafu hakupaswi kuwa chanzo cha matatizo ya kifedha, kwa mfanyakazi yoyote aliyekuwa analipwa mshahara bali iwe fursa ya kufurahia matunda ya kazi ya muda mrefu. 

“Tukijijengea utamaduni wa kuwekeza mapema kutatusaidia sisi wafanyakazi kuepuka changamoto za kifedha baada ya kustaafu na kuwa na maisha ya uhakika”, alisema Bw. Mwanga. 

Aidha aliwasisitiza wafanyakazi wote nchini kuhakikisha michango yao inalipwa kwa wakati na waajiri wao lakini pia watumie Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayotoa faida kubwa. 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Erick Mvati, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kufika katika Mkoa wa Mwanza kutoa elimu ya fedha ambayo ni muhimu kwa wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi. 

Aliongeza kuwa elimu hiyo ikifika kwa wananchi wote katika makundi mbalimbali itasaida kupunguza matatizo katika jamii kwa kuwa wananchi wataelewa haki zao lakini pia watajua sheria mbalimbali zitakazowaongoza na kujiepusha na migogoro ya mikopo.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Santley Kibakaya, alisema kuwa Wizara inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi ili wafahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika Sekta ya Fedha.

Aliongeza kuwa Sekta ya Fedha imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali, kupitia elimu hiyo inayoendelea kutolewa, wataalamu hao wanapata fursa ya kusikiliza changamoto, ushauri na maoni yanayotolewa na wananchi kwa ajili ya kufanyiwa utatuzi zile ambazo zinatakiwa kufanyiwa utatuzi, ushauri na maoni kwa ajili ya kuboresha zoezi hilo kwa mikoa ambayo haijafikiwa.

VETA YAFADHILI MAFUNZO KWA WANAWAKE 3000 JIJINI DODOMA


........................

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetoa ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwa wanawake 3000 jijiji Dodoma, yatakayotolewa katika Chuo cha VETA Dodoma.

Akizungumza jana, tarehe 24 Machi, 2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo yanayotolewa kupitia kikundi cha Wanawake na Samia, Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore kwa ufadhili wa mfunzo hayo.

Senyamule amesema wanawake wengi, hawana ujuzi, hivyo mafunzo ya stadi kwao ni muhimu ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

“Dodoma sasa ni mji wa kitalii na watu wengi wanakuja kwa ajili ya kupata huduma sa Kiserikali. Wapo wengine kutoka mataifa mbalimbali. Hivyo tunahitajika kutoa huduma za kiwango cha kimataifa na hilo linawezekana ikiwa tutapata mafunzo,” Senyamule amesema.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, Bi Fatuma Madidi ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA na Mkuu wa chuo cha VETA  Dodoma kwa kuridhia  mafunzo hayo kutolewa kwa wanwake wa Dodoma kupitia chuo  cha VETA Dodoma.

“Ukimsomesha mwanamke umesomesha jamii nzima, tunaahidi kuwa watulivi na kujifunza kwa bidii,” Madidi amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema VETA itagharamia mafunzo hayo kwa wanawake na Samia na kuongeza kuwa anaamini ujuzi watakaoupata utawasaidia kuendesha shughuli zao za uzalishaji na kujingiizia kipato.

WAZIRI MKUU AZINDUA LANGO LA UTALII HIFADHI YA MKOMAZI


.....................

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 25, 2025 amezindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyoko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Uzinduzi wa lango hilo ambalo limegharimu Shilingi Milioni 350 ni sehemu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kuchochea na kuongeza vivutio vya utalii nchini.

Akitoa taarifa ya lango hilo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Emmanuel Mwailama amesema ujenzi wa lango hilo utaongeza idadi ya watalii katika mbuga hiyo ambao wengi wanakwenda kuona maisha ya wanyama pembezoni mwa ziwa jipe, Faru weusi pamoja na tembo.

RAIS MSTAAFU KIKWETE AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA SENEGAL


..............

RAIS Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, leo tarehe 24 Machi 2025, amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Senegal, Mhe. Bassirou Diomaye Faye katika Ikulu ya Rais huyo jijini Dakar, Senegal.