JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatatu, 28 Aprili 2025

RAIS SAMIA IPONGEZA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE KWA KUFUZU KATIKA MASHINDANO YA FUTSAL KWA AFRICA


 Hongereni wanangu Timu ya Taifa ya Wanawake katika Mchezo wa Futsal kwa kufuzu kuingia fainali ya mashindano hayo kwa Bara la Afrika, na wakati huo huo kufuzu kucheza Mashindano ya Kombe la Dunia la Futsal kwa Wanawake 2025 ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), yatakayofanyika huko Manila, Ufilipino baadaye mwaka huu. 

Nimefurahishwa na juhudi na nidhamu yenu katika mashindano haya. Ushindi wenu ni heshima kwa nchi yetu, na hamasa zaidi kwa watoto wa kike kushiriki katika michezo, si tu kwa burudani lakini pia kama ajira. Ninawapenda na ninawatakia kila la kheri.


MAONO YA RAIS DKT. SAMIA YAMEIPAISHA SEKTA YA ANGA-MAJALIWA

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Anga.

 

Amesema hayo leo Jumatatu (Aprili 28, 2025) wakati alipofungua Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege kwa Ukanda wa Afrika (ACI Afrika) unaofanyika kwenye Hotel ya Mount Meru.

 

Amesema kuwa moja ya eneo ambalo Rais Dkt. Samia ameendelea kusimamia ni ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege nchini ikiwemo ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha msalato kilichopo jijini Dodoma.

 

Ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea na uboreshaji wa viwanja vingine vya kimkakati vya Kilimanjaro, Unguja, Pemba, Mwanza, Kigoma, Tabora, Shinyanga na Sumbawanga. “Pia tunaendeleza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti unaolenga kukuza utalii wa mazingira huku tukihifadhi mfumo ikolojia wa Serengeti”.

 

Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imewekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya mawasiliano kwenye viwanja wa ndege na masafa marefu ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa ndege na abiria.

 

Amesema kuwa kutokana na jitihada mbalimbali za Serikali za kuiimarisha Sekta ya anga, Tanzania imetajwa na Shirika la ICAO kushika nafasi ya nne barani Afrika kwenye masuala ya usalama wa anga

 

Kadhalika Uwanja wetu wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere umefanikiwa kushinda Tuzo ya Usalama ya Baraza la Viwanja vya Ndege Duniani, katika viwanja vyenye miruko ya ndege 50000 kwa mwaka”

 

Akizungumzia kuhusu shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Waziri Mkuu amesema hivi sasa ndege zake zinatoa huduma ya usafiri katika viwanja 15 vya ndani na nje ya nchi katika nchi za Dubai, Mumbai, Guangzhou, Johannesburg, Nairobi, Harare, Lusaka, Entebe na Kinshasa

 

“Shirika pia linatarajia kuongea safari zake katika miji ya London, Lagos, Accra, Juba, Muscat na maeneo mengine ya masoko ya kimkakati ili kuiunganisha Tanzania Kikanda na Kimataifa”

 

Kwa Upande wake, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa mkutano huo Inatoa jukwaa adimu linalowaleta pamoja viongozi na wasimamizi wa usafiri wa anga, waendeshaji wa viwanja vya ndege kujadili na kubadilishana mawazo katika kuboresha na kuikuza sekta ya usafiri wa Anga.

 

Naye Rais wa Baraza la Viwanja vya Ndege Afrika Emmanuel Chaves amesema kuwa mafanikio endelevu sekta ya anga afrika sio tu kwenye utungaji wa Sera bali kwenye maamuzi tunayoyafanya sasa katika kushirikiana “Kama tutaamua kwa dhati tutajenga Afrika yenye muunganiko na ushindani katika sekta ya anga”

BODA BODA NA SAMIA WAANDAMANA HADI OFISI ZA KATIBU WA CCM MKOA MWANZA

 

Baadhi ya waendesha bodaboda mkoa wa mwanza maarufu boda boda na samia wamefanya maandamano ya amani kutoka mkolani hadi kwa katibu wa CCM wa mkoa  wa mwanza kwalengo la kuendelea kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwanamna kinavyoendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Maandamo hayo yamefanyika leo April 28, 2025 huku wakieleza dhamira yao ya kuendelea kutoa hamasa ili Rais Dkt. Samia Suluhu ashinde kwakishindo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika October mwaka huu.


Akizungumza mara baada ya kufika kwenye ofisi za Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Mwenyekiti wa Boda boda na samia Ramadhan Musabi, amesema wameridhishwa na utendaji kazi wa Rais hivyo wataendelea kumuunga mkono ili azidi kutawala na kuwaletea wananchi maebdeleo zaidi.

Kwaupande wake katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Omary Mtuwa amesema Nia ya kikundi hicho ninzuri kwani wameamua kuwa wazalendo wa kukipigania chama chao cha Ccm .


Nao baadhi ya makatibu wa chama cha mapinduzi kutoka wilaya mbalimbali za  mkoa wa Mwanza wamepongeza juhudi za boda boda hao kwa kukiunga mkono chama hicho kwani kina nia njema na wananchi .

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU UTAKAO HUSISHA NCHI HAMSINI (50)

 

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi, utakao husisha nchi hamsini na nne na kufanyika Zanzibar. 


Mshauri wa Rais na mjumbe maalum katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, pia Mwenyekiti wa Kikundi cha Waafrika cha Kujadili Mabadiliko ya Tabia Nchi (AGN), Dkt. Richard Muyungi, ameeleza kuwa mkutano huu ni muhimu kutokana na mabadiliko katika siasa za kimataifa yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.


Aidha, Dkt. Muyungi amesema mkutano huo utajadili jinsi nishati safi inavyosaidia bara la Afrika, ambapo asilimia kubwa ya wananchi hawatumii nishati safi ya kupikia, na pia faida zitokanazo na juhudi za kimataifa katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.


Mgeni rasmi katika mkutano huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemedi Suleiman Abdullah.

KAMPUNI YA PERSEUS YATANGAZA KUANZA UJENZI WA MGODI WA DHAHABU WA NYANZAGA WILAYANI SENGEREMA


 ▪️Mradi wa ujenzi wa mgodi kugharimu Trillioni 1.4


 ▪️Dhahabu ya kwanza kuanza kuzalishwa robo ya kwanza ya Mwaka 2027


▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira bora ya uwekezaji


▪️Mgodi kuzalisha Ajira na mapato kwa serikali


Kampuni ya Perseus ya Nchini Australia yatoa tangazo rasmi la kuanza ujenzi wa mgodi wa dhahabu wa Nyanzaga uliopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza utakaomilikiwa na Kampuni ya Ubia ya Sotta ambapo Kampuni ya Perseus ina umiliki wa hisa za 84% na Serikali ya Tanzania ina umiliki hisa zisizofifishwa za 16% .

Taarifa hiyo iliyotolewa leo tarehe 28 Aprili, 2025 imeeleza kuwa takribani kiasi cha Shilingi Trilioni 1.4 sawa na Dola za Kimarekani Milioni 523 (pamoja na dharura) zitawekezwa kujenga mgodi mkubwa unaotarajiwa kuzalisha dhahabu ya kwanza katika robo ya kwanza ya Mwaka 2027.


"Fedha zote za kujenga mgodi zitafadhiliwa na Perseus kupitia mikopo isiyo na riba, ambayo itapelekwa kwenye mradi wa Nyanzaga moja kwa moja. Na fedha hizo zote zipo kwani *Perseus* ina salio la pesa taslimu na bullion la dola za Marekani milioni 801 kufikia tarehe 31 Machi 2025" ilifafanua taarifa hiyo.

Kwa kutarajia maamuzi ya mwisho ya kuwekeza (Final Investment Decision - FID) katika mradi huo yangepitishwa na uongozi wa juu wa Kampuni ya Perseus, tayari Perseus imetumia takriban dola za Marekani milioni 27.5 katika kutekeleza shughuli za awali za maandalizi ya uwekezaji.


Shughuli hizo za awali za kujenga mradi wa Nyanzaga zilizokuwa zinaendelea ni pamoja na kama kuanzisha eneo la kufanyia kazi (site establishment), _earthworks_ , ujenzi wa kempu pamoja na kutekeleza Mpango wa Utekelezaji wa Uhamisho (RAP) na kujenga makao mapya kwa watu walioathiriwa na mradi.


Mara baada ya kutoka kwa tangazo hilo la Perseus, Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* amesema taarifa hiyo ni njema kwenye kukuza sekta ya madini na ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu mpendwa *Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan* ambayo imeweka mazingira mazuri yanayoendelea kuvutia uwekezaji mkubwa nchini.

Vilevile, *Mheshimiwa Mavunde* alibainisha kwamba kutolewa kwa tangazo hilo na Kampuni ya Perseus kumeleta matumaini makubwa na kukata kiu ya wananchi wa Sengerema ambao wameusubiri mradi huo kwa muda mrefu na sasa ndoto yao inakwenda kutimia kwa kuona mradi mkubwa wa kuzalisha dhahabu unaanza ambao utasaidia upatikanaji wa mapato ya serikali,Ajira kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya Wilaya ya Sengerema na nchi kwa ujumla.


Aidha, Waziri Mavunde amesisitiza kwamba Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya madini nchini ili kufanikisha adhma yao na kupelekea kukuza uchumi wa Nchi na wananchi kwa ujumla.

MAPEPELE AMKABIDHI KIJITI HOSSEAH

...............

Na Sixmund Begashe

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nteghenjwa Hosseah amekabidhiwa rasmi ofisi na aliekuwa Mkuu wa Kitengo hicho Bw. John Mapepele ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, ili kuendelea kuwatumiaka wananchi kwenye ofisi yake hiyo.

Katika zoezi hilo la kihistoria lililofanyika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Patrick Marcelline alimpongeza Bw. Mapepe kwa Utumishi wake mwema kwenye Wizara hiyo na kumtakia kila laheri katika ofisi yake mpya, huku akimkaribisha Bi.Hosseah na kumuahidi ushirikiano wakutosha kwenye utekelezaji wa majukumu yake ndani ya Wizara hiyo inayojishughulisha na Uhifadhi pamoja na Utalii nchini.

Aidha Bi.Hosseah ambaye awali alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini OR-TAMISEMI, ameushukuru uongozi wa Wizara hiyo kwa kumpokea vizuri na kuahidi Utumishi mwema katika kuiongoza vyema timu nzima ya mawasiliano ili kufikia lengo la Wizara na Taifa kwa ujumla kupitia Maliasili na Utalii, huku Bw. Mapepele akiushukuru uongozi, maafisa wa Kitengo cha Habari, Watumishi wote wa Wizara hiyo kwa ushirikiano mzuri waliompatia katika kipindi chote alichohudumu hapo.

 

NGORONGORO,MLIMA KILIMANJARO VYAVUTIA WENGI OSAKA EXPO 2025.

 

Osaka, Japan.


Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro vimeonekana kuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya uchumi na biashara maarufu EXPO Japan 2025 yanayoendelea katika jiji la Osaka Kansai Japan ambapo wageni kadhaa wamekuwa wakitaka kujua namna ya kuweza kufika na kujionea vivutio hivyo.


Katika banda la Tanzania kwenye maonesho hayo wageni hao wamekuwa wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Tanzania na wengi wao kushangazwa na jinsi  nchi hiyo ilivyokuwa na utalii wa vivutio vingi vya kuvutia.

"Nimevutiwa sana leo kupata maelezo sahihi kuhusu hifadhi ya Ngorongoro,natamani siku moja kutembelea hifadhi hii ili niweze kuona wanyama hawa wanaoonekana kupitia picha mbalimbali, mimi ni mpenzi wa utalii wa kuangalia  wanyama,alisema bi Matsuda Ikamoto mkazi wa Osaka.


Bi Ikamoto alisema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akisikia kuhusu uwepo wa wanyama ambao hawafugwi katika maeneo ya kufugia wanyama na hivyo amepata maelezo sahihi kuhusiana na jinsi eneo la hifadhi ya Ngorongoro linavyoweza kuwalinda na kuwatunza wanyama hao.


Naye Bw. Yuri Toshiba alieleza matamanio yake ya siku moja kupanda mlima Kilimanjaro na hivyo kuweka historia  kwa kuwa miongoni mwa wajapan waliopanda mlima huo.

Wengi wa watembeleaji wa maonesho hayo wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa Tanzania kuendelea kuvitunza vivutio hivyo ili viweze kuendelea kuwepo hasa kutokana na dunia kukumbwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.


Akitoa maelezo kwa wageni mbalimbali waliotembelea maonesho hayo Afisa Utalii Mkuu kutoka Bodi ya Utalii Tanzania Bi Alistidia Karaze amesema Tanzania inaendelea kuimarisha vivutio na huduma kwa watalii ili kuongeza idadi ya watalii kila mwaka.


"Tanzania tuna vivutio vingi ambapo ukiachia utalii wa wanyama pia tuna fukwe mzuri pamoja na utalii wa malikale hivyo mtakapofika na kutembelea Tanzania mtafurahia vitu vingi ambavyo hamjawahi kuviona katika maeneo mengine.”alisema Bi Karaze. 

Tangu kufunguliwa kwa maonesho hayo Tanzania imekuwa ikifanya vizuri kwa kupokea wageni wengi kwenye banda ambao wamekuwa wakielimishwa kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu utalii,uchumi,biashara na sekta nyingine.

BARUA YA PAPA FRANCIS KWA MH. RAIS. SAMIA SULUHU HASSAN.

 Hii hapa barua ya Papa Francis aliyo muandikia Mh. Rais Samia Suluhu Hassan siku chache kabla ya kufariki.

"Kwa unyenyekevu na shukrani, nimepokea ujumbe wa hayati Papa Francisko kwangu, kwa nchi yetu na kwa Watanzania wote, aliouandika siku chache kabla Mwenyezi Mungu hajamwita kwake, na kumkabidhi Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino".


Tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu alale mahali pema.



Listen Mkisi Radio