JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumanne, 20 Mei 2025

HABARI KUBWA ZILIZO PEWA NAFASI KWENYE KURASA ZA MBELE YA MAGAZETI LEO TAREHE 20.05.2025


Habari gani popote ulipo Nikukaribishe kupitia vichwa vya habari kwenye magazeti ya leo tarehe 20.05.2025






























 

SERA MPYA YA MAMBO YA NJE IWE NYENZO YA KUTETEA MASLAHI YA TANZANIA KIMATAIFA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania ya mwaka 2001, toleo jipya la mwaka 2024, ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na ni nyenzo madhubuti ya kulinda na kutetea maslahi ya taifa ndani na nje ya mipaka.


Aidha, amesema kuwa Sera hiyo inalenga kufungua milango ya fursa mpya za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa pande zote za Muungano, hususan Zanzibar, ambayo kwa kiwango kikubwa inategemea sekta ya nje kwa maendeleo yake.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika uzinduzi wa Sera mpya uliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jana tarehe 19 Mei 2025, Jijini Dar es Salaam.


Vilevile, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kusimama imara maboresho ya Sera hiyo, pamoja na hatua kubwa zilizochukuliwa za kuimarisha diplomasia.


Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa sekta ya utalii, usafirishaji wa baharini, uzalishaji wa bidhaa kama mwani na karafuu, pamoja na uwekezaji wa miradi ya maendeleo, ni mifano ya utegemezi mkubwa wa Zanzibar katika diplomasia ya kiuchumi.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi ameihimiza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhakikisha inashawishi mataifa rafiki kuanzisha ofisi za uwakilishi Zanzibar ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wageni. Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia pia kukuza uwekezaji, kuimarisha sekta ya utalii, na kurahisisha mazingira ya ufanyaji biashara.

Jumatatu, 19 Mei 2025

MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI WAPEWA SOMO USIMAMIZI WA MIRADI NA USULUHISHI WA AKAUNTI


Angela Msimbira, PWANI


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sospeter Mtwale, amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa kuhakikisha wanazisimamia Halmashauri zote kufanya usuluhishi wa akaunti za kibenki, hususani tunapoelekea mwishoni mwa mwaka wa fedha wa Serikali.


Akizungumza leo Mei 19, 2025 katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yanayofanyika mkoani Pwani,  Mtwale amesema bado kuna baadhi ya Halmashauri ambazo zimekuwa na akaunti ambazo hazijafanyiwa usuluhishi kwa muda mrefu, hali inayokwamisha uwajibikaji na utawala bora wa fedha za umma.

“Mikoa ni taasisi wezeshi. Hakikisheni kuwa mnazisimamia Halmashauri zilizo chini yenu kuhakikisha usuluhishi wa akaunti unafanyika kikamilifu kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha,” amesisitiza.


Aidha, amewakumbusha viongozi hao wajibu wao wa msingi katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika maeneo mbalimbali ya mikoa, akiwataka kuhakikisha miradi hiyo inakidhi viwango na kuendana na thamani ya fedha inayotolewa na serikali.


Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa Makatibu Tawala Wasaidizi kushirikiana kikamilifu katika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa wakati na kwa weledi, ili kupunguza idadi ya hoja za ukaguzi zinazojitokeza kila mwaka.

“Serikali ina sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya usimamizi wa rasilimali watu na fedha. Ikiwa viongozi mtaisimamia kikamilifu, hoja za ukaguzi zitapungua kwa kiasi kikubwa. Nendeni mkalisimamie hili kwa umakini mkubwa,” amesisitiza.


Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa serikali kupitia Taasisi ya Uongozi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI wa kuimarisha uwezo wa viongozi wa ngazi ya mikoa katika kusimamia utekelezaji wa sera na miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

TUMEJIZATITI KUPUNGUZA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA YA ELIMU

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti katika kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi zikiwemo za sekta ya elimu.


Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Mei 19, 2025) wakati akizungumza na wananchi katika mikutano wa hadhara iliofanyika Sengerema mjini na Buchosa wilaya ya Sengerema akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

 

Waziri Mkuu amesema miongoni mwa hatua ambazo Serikali imezichukua ni pamoja na kuendelea kutoa elimu msingi bila ya ada na hivyo kuwawezesha watoto wa kitanzania wenye umri wa kwenda shule kupata elimu.

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika maeneo mbalimbali nchini hususani katika yale yenye msongamano mkubwa wa wanafunzi.

 

”Mkakati mwingine mkubwa unaoendelea kutekelezwa na Serikali ni ujenzi wa mabweni, nyumba za walimu, pamoja na kujenga shule za amali ili wanafunzi watakapomaliza shule hizi waondoke na ujuzi.”

 

Akizungumzia kuhusu changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, Waziri Mkuu amesema kwa sasa Serikali inatekeleza miradi ya maji ikiwemo ya kutoa maji katika Ziwa Victoria na kuyasambaza kwa wananchi, hivyo amewataka waendelee kuwa na subira.

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema uhakikishe unakamilisha mchakato wa ujenzi wa mradi wa soko la halmashauri hiyo ili Sengerema iweze kuwa kituo kikubwa cha biashara.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewahakikishia wakazi wa wilaya ya Sengerema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kumkabidhi mkandarasi kazi ya ujenzi wa barabara ya Sengerema-Nyehunge ili aanze ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

‎RC SERUKAMBA AITAKA TRA KUDHIBITI RISITI FEKI, KUHAMASISHA ELIMU YA KODI


‎Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Peter Serukamba, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo kuhakikisha wanadhibiti utoaji wa risiti feki kwa bidhaa mbalimbali, akisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFD) ili kuongeza mapato ya serikali.

‎Akizungumza leo Mei 19, 2025 ofisini kwake baada ya kupokea ugeni wa Viongozi kutoka TRA Makao makuu uliofika kwa ajili ya kuanza kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi kwa njia ya "Mlango kwa Mlango", Serukamba alisema kuwa ni muhimu kwa maofisa wa TRA kutumia elimu na si nguvu wakati wa kukusanya kodi. 


‎Aidha, Mhe Serukamba amewahimiza wafanyabiashara wote mkoani Iringa kupokea elimu hiyo kutoka kwa wataalamu wa TRA na si kufunga maduka au kuwaogopa. 

‎Sambamba na hilo kampeni ya "Mlango kwa Mlango" inalenga kuelimisha wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari, matumizi sahihi ya mashine za EFD, na kutoa risiti kwa kila mauzo. 

‎"Ni muhimu kwa kila mfanyabiashara kutoa risiti halali kwa kila mauzo na kulipa kodi stahiki na hii itasaidia serikali kupata mapato ya kutekeleza miradi ya maendeleo,"amesema Serukamba



MASHAHIDI WA MAJI DAR WAPAZA SAUTI UCHAFUZI WA MITO



Na Mussa Khalid

Mashahidi wa Maji Taka na Maji safi Mkoa wa Dar es salaam wameiomba serikali kupitia Mamlaka za usimazizi wa mazingra kusimamia Sheria ,sera na kanuni katika kuwachukulia hatua watu au viwanda vinavyofanya uharibifu wa mazingra ikiwemo kwenye mito katika maeneo mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Mashahidi wa Maji Mkoa wa Dar es salaam Zaharani Omary wakati waliposhirikiana na watendaji wa serikali za mitaa Kigogo na VINGUNGUTI kupofanya ziara ya kukagua mito Msimbazi,Kibangu na Tenge ili kuangalia maeneo korofi yanayotiririsha Maji yasiyomazuri katika mito hiyo.

Aidha amesema kuwa lengo lao ni kuikumbusha serikali kusaidia kutatua changamoto hiyo katika mito hiyo ambayo Maji mabaya yamekuwa yakiingia kutoka viwandani na hivyo kuathiri Wananchi.

"Tumepita katika kiwanda cha Betri Yuwasa tumekuta Kuna Maji yasiyomazuri yanatiririshwa katika mito Msimbazi,pia tumepita kiwanda Cha Nida tumekutana na kadhia hiyo na hata ushahidi wa picha upo kutokana na shida hiyo kwani Kuna baadhi ya Wananchi wanapatashida na Maji hayo"amesema Zaharani

Amesema kutokana na serikali kuwa ni sikivu inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wanaimani watasaidia katika kufanya utatuzi wa siala hilo ili kuweza kuisaidia jamii.

Akitolea mfano kuwa kutokana na uharibifu unaofanywa na baadhi ya viwanda katika mito hiyo inasababisha mpaka viumbe hai vinavyokaa kwenye Maji kutokuwepo kutokana na kushindwa kuhimili Maji hayo yenye sumu.

Aidha amesema kuwa wataendelea kupaza sauti kila wakati ili kuhakikisha changamoto ambazo zinaikumba jamii kupitia uharibifu unaofanywa na baadhi ya watu au viwanda katika mito inapatiwa ufumbuzi.

Huo umekuwa ni muendelezo wa Mashahidi wa Maji kupita na kujionea kadhia ya uharibifu wa mazingra husuani katika rasiliali maji katika maeneo mbalimbali ili kupaza sauti Kwa kuzijulisha Mamlaka za ufanyaji maaamuzi kufanya utatuzi wa changamoto hizo.


Mbeto amtaka Jussa atangaze sera za ACT, Maalim Seif yuko mbele ya haki


Na Mwandishi Wetu ,Zanzibar


Chama Cha Mapinduzi  kimemkanya Makamu Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo,  Ismail Jussa Ladhu ,kutaja  sera za chama chake na kumtaka  aache kulitumia jina la Hayati  Maalim  Seif Sharif  Hamad kama msingi wa sera.


Pia kimesisitiza iwapo ACT  hakina sera za kimaendeleo , akae kimya na kuacha kuwapumbaza wananchi kwa siasa za  porojo na uchepe.


Matamshi hayo yametamkwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanziabr, Idara ya itikadi ,Uenezi na Mafunzo Khamis  Mbeto  Khamis, aliyemtaka Jussa asilitumie jina la Maalim  seif aliyetangulia mbele ya haki


Mbeto alisema kwa wananchi wa  zanzibari  hakuna hata mtu mmoja asiyejua  Jussa alikuwa rafiki  mwandani wa  Maalim seif kwa ukuruba na mnasaba wao.


Alisema wananchi wanataka  kusikia sera za ACT  , kisha wazilinganishe na sera zilizoleta  maendeleo chini  ya serikali ya Rais Dk  Hussein Ali Mwinyi .


"Kwa Chama cha siasa  makini  duniani sera huwa ndiyo dira ya ushindani  badala ya  porojo ,kejeli na matusi kama afanyavyo Jussa na wenzake" Alisema Mbeto.


Aidha  alimtaka  Jussa asiwafanye wazanzibari  kama watu wasio na  macho ya kuona  yale  yaliofanyika , au hawajui kutofautisha  maendeleo yaliokuwepo  awali na yaliopo sasa.


Mbeto alimtaka Jussa  kuelewa kuwa wazanzibari ni watu werevu mno  wana akili, maarifa na hekima hivyo hawaghilibiwi kwa porojo na siasa zake za chuki


'Wazanzibari hawako tayari    kuendelea kugawanywa kwa siasa za chuki  na hasama .Kiu yao ni  maendeleo ya nchi yao ,Umoja ,Usalama  na Ustawi  wa Amani "Alieleza


Katibu  huyo  Mwenezi  alimtaja   Jussa na wenzake mara nyingi  wamekuwa wakihubiri ubaguzi ambao kwa miaka mingi umechangia kuwagawa wananchi  wa Unguja  na Pemba


"Maalim Seif  hana sifa ya kuitwa shujaa au  jemedari wa Zanzibar. Jemedari Mkuu wa Mapinduzi  yalioleta zanzibar ukombozi  ni  Hayati Mzee  Abeid  Amani  Karume kupitia ASP  " Alisema Mbeto.


Aliongeza kusema kuwa Maalim  Seif ni atabaki kuwa kiongozj aliyekiwa na heshima  baada ya kupikwa ,kuandaliwa kisiasa na kiuongozi toka  akiwa mwanachama wa CCM.


Pia Katibu  huyo Mwenezi  alimkanya na kumueleimisha Makamu huyo Mwenyekiti  wa ACT  akimtaka aache kuvuruga  historia ya zanzibar kwa kudai  Maalim  seif ni jemedari na shujaa  wa Zanzibar.


"Maalim Seif ataheshimika kama Kiongozi  aliyewahi kuwa Waziri  wa Elimu ,Waziri  Kiongozi  pia Makamo  wa kwanza  wa Rais  SMZ si vinginevyo " Alisiaitiza  Mbeto .


Kwa upande  mwingine  Mbeto slimtaka Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo  Othman  Masoud  Othman ,ajiandae kushindwa katika uchaguzi mkuu ifikapo oktoba  mwaka  huu.


"Jussa  huwezi kuzifananisha sifa za uongozi alizokuwanazo  Hayati  Maalim  Seif na Othman  .Wazanzibari  wanahitaji kupata viongozi wenye maono na wapigania   maendeleo hivyo  asimlinganishe  Othman  na Maalim  Seif  "Alisema


Kadhalika  Mwenezi  huyo alisema Wazanzibari  hawawezi kutoa kura zao na kumpigia  othman  kwa nafasi ya urais kwani hata hiyo kazi ya kuwa makamo wa Rais  SMZ  imekuwa ikimshinda

RAIS WA NAMIBIA DKT NETUMBO NANDI-NDAITWAH KUFANYA ZIARA NCHINI MEI 20-21,2025


Rais wa Jamhuri ya Namibia Dkt Netumbo Nandi-Ndaitwah anatarajiwa kufanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia kesho tar 20 hadi 21 Mei mwaka huu kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Ikulu Shaaban Kissu imeeleza kuwa Ziara hiyo ya kwanza ya Rais Dkt Nandi-Ndaitwah chini Tanzania tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Namibia tar 21 Machi,2025 na inalenga kukuza ushirikiano wa kisiasa,kiuchumi na kijamii ikiwemo katika nyanja za biashara,uwekezaji na elimu.

Tanzania na Namibia zimejenga uhusiano wa muda mrefu wa kidugu na kidiplomasia,hivyo ziara hiyo itafungua fursa mpya za ushirikiano zitakazowawezesha wananchi wan chi zote mbili kunufaika kiuchumi




 

Listen Mkisi Radio