Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Tarura Wilaya ya Kibiti yapewa siku 9 Kufanya Marekebisho ya Barabara ya Changarawe ya Bungu kwenda Kijiji cha Mchungu


Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Kibiti imetoa siku 9 kwa Wakala wa Barabara vijijini TARURA Wilaya ya Kibiti kurekebisha Barabara ya changarawe ya bungu kwenda Kijiji Cha Mchungu ambayo serikali imekwishalipa zaidi ya shilingi milioni 300.

Akitoa maelekezo baada ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya CCM Wilaya ya Kibiti Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibiti Juma Ndaruke TARURA wilaya ya Kibiti wapitie upya mikataba waliyoingia na Wakandarasi kujenga barabara wilayani humo ili wajiridhishe kama kilichotekrlezwa kinaendana na kiasi cha fedha serikali imelipa sambamba na kuangalia ubora wa barabara hizo.

Amesema "TARURA wapitie upya kuhakiki ubora wa utekelezaji wa miradi ya Barabara wilayani humo ili utekelezaji wa miradi uendane na thamani ya fedha za serikali zilizolipwa".

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph kolombo amesema barabara vijijini hutengenezwa kwaajili ya kurahisisha huduma za usafi ikiwemo usafirishaji wa mazao Yao kwa urahisi.

Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibiti Eng. Ayubu Ngereza amesema changamoto ya Barabara hiyo ni kutokana na mvua nyingi zilizonyesha wilayani humo na kuahidi kuifanyia ukarabati haraka kama walivyoagizwa.







Post a Comment

0 Comments