Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Cdf: Majenerali Wastaafu Wanastahiri Kupongezwa kwaUtendaji Kazi Wao Mzuri

 

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali, John Mkunda amesema maofisa waliofikia cheo cha Brigedia Jenerali, Meja Jenerali na kuendelea wanapostaafu wanautaratibu wao wa kuwaaga ikiwamo kupongezana kwa utendaji wao uliotukuka jeshini.

Jenerali Mkunda alitoa kauli hiyo Agosti 2, mwaka huu wakati wakiwaaga kwa paredi ya kuwasukuma kwenye magari Majenerali sita wakiwamo wenye cheo cha Meja Jenerali wanne kati yao, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaarufu Charles Mbuge na Brigedia Jenerali wawili.

“Kwa kutambua mchango wao katika jeshi letu, tunawasukuma kwenye magari na kuwatakiwa maisha mema, lakini bado utumishi wao utakoma baada ya miaka mitatu tangu wastaafu mpaka sasa wanahesabika kama jeshi la akiba wakati wowote wanaweza kuitwa kazini”alisema Jenerali Mkunda.

Mbali Meja Jenerali Mbuge, wengine ni, Meja Jenerali Gabriel Muhize, Meja Jenerali Ally Katimbe, Meja Jenerali Chelestino Msola, Brigedia Jenerali William Likangaga na Brigedia Jenerali Andrew Mughamba.

Kwa upande wake Meja Jenerali Muhize alisema anawaasa askari na maofisa wa jeshi waliobaki kazini wafanye kazi kwa weledi ili wafikie siku ya ukomo wa utumishi wao kwa Amani.

“Namshukuru Mungu sana kwa siku hii mimi na wenzangu tumelitumikia jeshi l=na kustaafu utumishi kwa usalama na Amani”alisema Meja Jenerali Muhize.

Post a Comment

0 Comments