MBETO : INEC, ZEC TUME HURU ZA UCHAGUZI ZENYE UWAZI NA HAKI

 

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeutaka Upinzani kutozibeza  Tume za   Uchaguzi , INEC na ZEC  na kudai si huru wakati  Chadema na ACT  Wazalendo , vimekuwa vikiongeza idadi  vya Viti vya Udiwani ,Uwakilishi, Ubunge  na kupata kura nyingi  za urais   .


CCM kimesema Tume hizo ziko huru na kutenda haki zikiongozwa na  binadamu na kwamba  Tume  yoyote  itakayoundwa kwa mfumo wowote ,  zitaendelea kuongozwa na binadamu si  Malaika  .


Matamshi  hayo yametamkwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zazibar Idara ya Itikadi  , Uenezi na Mafunzo , Khamis  Mbeto  Khamis ,  aliyesema madai ya upinzani kuhusu  Tume za Uchaguzi  hayana mantiki  , mashiko na  kukosa  nguvu  ya hoja.


Mbeto  alisema  grafu ya idadi ya Viti vilivyokwenda upinzani , kuanzia Mwaka 1995 hadi 2020, imekuwa ikipanda katika    Uchaguzi za  Serikali za Mitaa, Udiwani, Uwakilishi ,Ubunge  na kuongezeka kura za Urais. 


Alisema katika Uchaguzi Mkuu  wa Kwanza Mwaka 1995 , NCCR-MAGEUZI  na CUF , vilipata Viti   kwa uchaguzi wa   Tanzania  Zanzibar , ambapo  CCM  mwaka huo ilipata Viti   24  na CUF 23  vya Ubunge na  Uwakilishi.


"Nafikiri   maana ya uwazi na  demokrasia   kwa upinzani hadi itangazwe CCM kimeshindwa  kura  za urais. Uchaguzi ni  mchakato wa  kukubalika  kwa chama cha siasa na wananchi .  CCM kina  Mizizi mirefu ,  Nyenzo, Rasimali Fedha na watu kuliko Upinzani " Alisema Mbeto 


Hivyo  basi, Mwenezi  huyo katika maelezo  yake ,alisema, haiwezekani  vyama  vilichosajiliwa Mwaka 1993 na kuendelea  , kama  Chadema  NCCR-MAGEUZI ,  CUF , ACT au CHAMA viwe na  ubavu wa  kukiangusha CCM .


"CCM  ni jiti  kubwa lenye Matawi  mapana na    Mizizi mirefu .Gogo na shina la  mti  wake halikatiki kirahisi  . Kuchuana na CCM  katika  Uchaguzi kunahitajika upinzani  wenye  mbavu nene za  kisiasa   " Alisisitiza Mbeto 


Aidha  Katibu huyo Mwenezi  akitoa mfano, alisema   uchaguzi wa Mwaka 2015, Chadema  kilipata Viti vya Ubunge maeneo  ya Mijini na kukosa  Vijijini ,  kutokana na uchanga wake kisiasa. 


Mbeto  alitaja kuna Wabunge wa Chadema  wamekuwa bungeni  kwa   zaidi ya  vipindi viwili  ,ushindi  wao  umetangazwa na  Tume  ambazo leo  wanaibeza na kudai  si huru. 


'Kina Tundu Lissu, John Heche, John Mnyika, Godbless Lema, Halima Mdee ,Ester Bulaya, Boniface Jackob ,Peter Msigwa, Said Kubenea na joseoh Mbilinyi wote wametangazwa washindi na  Tume ya uchaguzu iliopo sasa  " Alieleza Mwenezi  huyo 


Akizungumzia Katiba  ya Tanzania na Zanzibar , Mbeto alisema Katiba hizo , zimeongoza nchi  kwa miaka    61 bila   misukosuko  ya aina yoyote,  kila  katika wakati  mgumu Katiba  hizo zilitoa majibu  na kuelekeza.



'Serikali ya   Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliunda  Tume iliokusanya maoni ya wananchi ilioongozwa na  Joseph Warioba. Likaundwa Bunge Maalum la Katiba.  Ilipoandikwa Katiba  inayopendekezwa. Chadema na CUF  wakawatoa wabunge wao kabla ya Bunge  Maalum la katiba hakijafikia tamati " Alisema 


Mbeto alieleza kuwa  leo  unapoisoma Katiba  iliopendekezwa kwa utuo ,  utulivu  na umakini, utaona ilivyozingatia changamoto  na kutekeleza ushauri na maoni   yaliotolewa na watanzania  kwa ustadi na mazingatio .

Post a Comment

Previous Post Next Post