JSON Variables

Tuesday, May 6, 2025

DAY CARE ZATAKIWA KUSAJILIWA AMA TAFUTENI BIASHARA NYINGINE YA KUFANYA.

 

Mratibu wa Familia na Watoto kutoka Halmashauri ya Jiji la hilo,Christon Cletus, akizungumza na wamiliki na walezi wa watoto katika vituo vilivypo Ilala jijini Dar es Salaam leo wakati wa semina ya namna ya kupambana na ukatili kwa watoto.



NA MWANDISHI WETU



WAMILIKI wa vituo vinavyotoa huduma ya kulea watoto na masomo ya awali ‘Day Care’ wametakiwa kusajili vituo vyao la si sivyo watafute shughuli nyingine za kufanya.

Wito huo umetolewa leo Mei 5, 2025 jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Familia na Watoto kutoka Halmashauri ya Jiji la hilo,Christon Cletus,  wakati akifungua semina ya siku tatu kwa wamiliki na walezi wa watoto wa vituo vya Wilaya ya Ilala.



Semina hiyo yenye lengo la kuwaelimisha watoa huduma hao wa malezi kwa watoto kukabilana na changamoto ya ukatili, imeratibiwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stad, Furahika kilichopo Buguruni Malapa, Ilala jijini Dar es Salaam.

“Nikiangalia mmejitokeza kwa wingi lakini kwa uzoefu wangu nikiwaangalia hapa, nagundua waliosajili vituo vyao hawazidi wawili na sijajua kuna ugumu gani, hivyo natoa wito kwa wale ambao bado hawajasajili kuwasaliana na Ofisa Ustawi husika ili kupata utaratibu na kusajili.


“Mnaposajili inakuwa rahisi kuwafikia inapotokea miradi mbalimbali ya maendeleo na hata inapotokea unyanyasaji kwa kituo furani inakuwa rahisi pia kufika na kuchukua hatua stahiki, naamini wasio sajiliwa baada ya mafunzo hayo watafuata utaratibu na kukamilisha mchakato huo,” amesema.


Pia alimpongeza Mkuu wa Chuo hicho kwa jitihada za kupambana na ukatili wa watoto na kumtaka hasiishie kwa Wilaya ya Ilala pekee bali afanye semina kama hiyo kwa mkoa wote wa Dar es Salaam ili kuwafikia walimiki na walezi wengi.


Naye Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Furahika, Dkt David Msuya amewasistiza washiriki wa semina hiyo kuhakikisha baada ya mafunzo hayo wanakwenda kuwa mabalozi wazuri watakaosaidia kuwajenga watoto katika misingi bora na kuwa na kizazi imara kitakachojenga taifa imara siku za usoni.


Kuna baadhi ya vituo kuna mambo mengi mengi mabaya ya unyanyasaji watoto ambayo yanafanywa wakati mwingine kwa kutojua misingi ya malezi na hiyo inakuja kutokana na kuajiri baadhi ya watumishi wasiokuwa na elimu.


Naamini baada ya mafunzo hayo mambo yatabadilika unyanyasaji utapungua kama si kuundosha kabisa na hapo tutakuwa tumeunga mkono Serikali kwa vitendo katika kupambana na ukatili wa watoto hususan katika  baadhi ya vituo vya ‘Day Care’, amesema.     


Joyce Mndima mshiriki kutoka, Mish Day Care, kilichopo Kata ya Buguruni, amesema anaamini baada ya mafunzo hayo ya siku tatu watatoka na uelewa wa kutosha namna ya kulea watoto toafuti na awali.

“Nashukuru kwa mafunzo hayo kwa maana yatatusaidia kuwalea watoto vizuri na tunakwenda kuwa mabalozi wazuri,” amesema. 

0 comments:

Post a Comment