JSON Variables

Tuesday, May 6, 2025

RAIS MWINYI AKUTANA NA KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI ZANZIBAR

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Kamati ya Amani ya Viongozi  wa Dini Zanzibar kujadili Mustakabali wa Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba Mwaka  Huu.


Rais Dkt,Mwinyi ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Serikali inafanya kila Juhudi Kuhakikisha Mifumo yote ya Uchaguzi inafanya Kazi kwa  Uhuru ,Amani na Uwazi  wakati wa Kampeni, Upigaji kura na Matokeo ya Uchaguzi kwa dhamira ya kudumisha Amani Iliopo kwa Maslahi ya Nchi.

Rais Dkt, Mwinyi ameishauri Kamati hiyo kuwakutanisha Wanasiasa kufanya Mjadala wa pamoja Kuzungumzia Umuhimu wa Amani ya Nchi pamoja na kudhibiti Viashiria  vya Uvunjifu wa Amani kabla na Baada ya Uchaguzi .


Aidha ameahidi   Serikali Kuendelea kushirikiana na Kamati hiyo ambayo imekuwa ikifanya  Kazi Muhimu ya Kuhubiri Amani tangu ilipoasisiwa Mwaka 2005.


Rais Dkt, Mwinyi amesema  Mshikamano wa Wananchi na Amani ni Tunu Muhimu kwa Mustakabali wa Maendeleo  ya Nchi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati Hiyo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab amesema Mkakati Wa Kamati Hiyo ni Kuhakikisha Mazingira ya Uchaguzi yanakuwa ya Amani wakati wa Uchaguzi, na baada ya Uchaguzi na Wananchi waingie katika Uchaguzi kwa Uwazi, Upendo na Furaha.


Kamati hiyo imemkabidhi Rais Dkt, Mwinyi   Kitabu Maalum cha Muongozo wa Viongozi wa Dini Kuhusu Uchaguzi.

0 comments:

Post a Comment