JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Alhamisi, 22 Mei 2025

SUMA JKT YACHANGIA BIL.2.66 KWA SHUGHULI ZA VIJANA WA JKT


 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amesema kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi 2024/25, SUMAJKT limechangia jumla ya Shilingi Bilioni 2.66 kwa ajili ya kugharamia shughuli za malezi ya vijana wa JKT, na limetoa gawio lenye jumla ya Shilingi Bilioni 4.27 kwenda Mfuko Mkuu wa Serikali (HAZINA).

Waziri Dkt. Tax ameyasema hayo leo tarehe 22 Mei 2025 Jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema Wizara hiyo kupitia SUMAJKT pia imefanikiwa kuchangia katika ujenzi wa uchumi ili kuipunguzia Serikali gharama za uendeshaji wa mafunzo kwa vijana wa JKT kwa kutekeleza miradi mbalimbali kama vile Ujenzi wa vituo vya madini katika mikoa ya Tanga (Handeni), Ruvuma (Songea), Katavi (Mpanda), Mbeya (Chunya), Simiyu (Bariadi), Mara (Musoma) na Kagera (Bukoba) na Vile vile, ujenzi wa ukuta katika migodi ya Mirerani Simanjiro, Manyara.

"Kuimarisha viwanda vyake ikiwemo Kiwanda cha Maji ya kunywa Mgulani kilichofikia uwezo wa kuzalisha katoni 2500 za nusu lita na 4400 za lita moja kwa siku, Kiwanda cha ushonaji Mgulani chenye uwezo wa kuzalisha mavazi ya kijeshi 300 hadi 400 kwa siku, Kiwanda cha bidhaa za ngozi Mlalakuwa, Kiwanda cha Kuchakata mahindi Mlale Songea chenye uwezo wa kuchakata tani 20 kwa siku, Kiwanda cha Samani Chang’ombe na kiwanda cha taa za LED kilichopo Dar es Salaam.

"Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia mradi wa REA  katika mikoa ya Morogoro, Shinyanga na ufungaji wa umeme (Installation) katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Singida, Shule ya Mfano jijini Dodoma na Ofisi ya Rais (Ikulu) Chamwino" alisema Waziri Dkt.Tax.

0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio