JSON Variables

Thursday, May 1, 2025

BEGASHE MFANYAKAZI HODARI MALIASILI 2024/2025




 ................

Na Yusufu Kayanda

Afisa Uhusiano Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Sixmund Begashe, amesema heshima kubwa aliyoipata ya kutangazwa kuwa Mtumishi Hodari wa Wizara ya Maliasili na Utalii ni heshima kwa wanahabari wote nchini, pamoja na watumishi wote wa wizara hiyo kutokana na ushirikiano mzuri waliouonesha katika kuufahamisha umma kuhusu matokeo chanya ya utekelezaji wa kazi za wizara na taasisi zake.

Bw. Begashe amesema hayo leo mkoani Singida, mara baada ya kupokea salamu nyingi za pongezi kutoka kwa viongozi wa wizara hiyo, watumishi wenzake, waandishi na wahariri wa vyombo vya habari, pamoja na watu mbalimbali, kufuatia kutangazwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa Mtumishi Hodari wa mwaka 2024/2025.

"Nimeungwa mkono na wanahabari wengi nchini katika kutekeleza majukumu yangu. Wamekuwa ni sehemu ya familia yangu kikazi. Tumeshirikiana vyema na watumishi wenzangu, viongozi katika ngazi mbalimbali, pamoja na familia yangu. Hali hiyo imenipa nafasi ya kufanya vizuri katika kuhabarisha umma kuhusu matokeo chanya ya utekelezaji wa kazi za wizara yetu. Hivyo, uhodari huu ni wetu sote," alisema Bw. Begashe.

Aidha, ameongeza kuwa heshima hiyo inaendelea kumhamasisha kufanya kazi kwa bidii zaidi, huku akiendelea kushirikiana vyema na wanahabari wote chini ya miongozo bora ya msemaji wa wizara pamoja na viongozi wote kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na kuwapongeza watumishi wote wa wizara hiyo kwa kazi nzuri wanazozifanya, alimpongeza Bw. Begashe kwa kutangazwa Mtumishi Hodari na pia kuwatakia watumishi wote nchini Sikukuu Njema ya Mei Mosi.


</

RAIS SAMIA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKISHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI SINGIDA

Wafanyakazi kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi za umma na binafsi wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Maadhimisho ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambazo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Zawadi ya Vikombe kwa Washindi wa michezo Mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi Kitaifa yaliyofanyika Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida leo Mei 01,2025.

KATIBU MKUU LUHEMEJA AHIMIZA UMOJA AFRIKA KUKABILI ATHARI ZA MAZINGIRA

Washiriki wakifuatilia Mkutano wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) tarehe 30 Aprili 2025 katika Ukumbi wa Hotel Verde Mtoni, Zanzibar.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) Dkt. Richard Muyungi akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mkutano huo leo tarehe 2 30 Aprili 2025 katika Ukumbi wa Hotel Verde Mtoni, Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) tarehe 30 Aprili 2025 katika Ukumbi wa Hotel Verde Mtoni, Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Upotevu an Uharibifu Bw. Ibrahima Diong mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) tarehe 30 Aprili 2025 katika Ukumbi wa Hotel Verde Mtoni, Zanzibar.

.....

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuwa na umoja wenye sauti moja yenye nguvu ili kuwa na sauti moja katika mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi. 

Ametoa wito huo wakati akifunga Mkutano wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) tarehe 30 Aprili 2025 uliofanyika Zanzibar ambapo amesema Afrika iliyounganishwa yenye sauti thabiti itatoa nafasi kubwa ya kuwasilisha vipaumbele vyake kwenye mikutano ya kimataifa.

Mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu, umewakutanisha washiriki kutoka nchi 54 barani Afrika ambao pamoja na masuala mbalimbali wamejadili ushirikiano katika uhifadhi wa mazingira.

"Afrika inahitaji kwenda mbali zaidi katika kuzungumzia mabadiliko ya hali ya hewa, na kwa hivyo, tunapaswa kwenda pamoja kukabiliana na changamoto hiyo," amesema.

Mhandisi Luhemeja alisema Afrika si bara masikini, hivyo ipo haja ya kuwa na sera na mikakati inayolinda utajiri wa Afrika kwa maendeleo endelevu ya bara hilo. 

Pia, Katibu Mkuu alisema kwa kuwa Afrika ndiyo iliyoathiriwa zaidi, hivyo kipaumbele cha bara ni kuwa na fedha za uhakika kwa kuzingatia vipaumbele na maslahi mapana ya watu wa barani humo. 

Alisisitiza mfumo wa ruzuku ni muhimu ili kufadhili miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hivyo Afrika lazima ihamasishe upatikanaji wa Dola za Marekani Trilioni 1.3 kufikia mwaka 2025.

Halikadhalika, Mhandisi Luhemeja alisema mkutano huu umesisitiza haja ya kuwa na ufafanuzi wa kupata fedha kutoka kwa Mfuko wa Hasara na Uharibifu, mchakato unaopaswa kurahisishwa kupata fedha hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) Dkt. Richard Muyungi alisema miongoni mwa mijadala iliyojadiliwa ni utafutaji wa kiasi cha shilingi bilioni 300 kwa ajili nishati safi barani Afrika ambayo ni utekelezaji wa maelekezo hayo ya mkutano wa viongozi wakuu wa nchi uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Alisema suala la kuhakikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa ajili ya watu milioni 300 wa Afrika kupata nishati safi lilikuwa ajenda kuu ya mkutano huo kuelekea Mkutano wa 30 Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabiachi (COP30) unaotarajiwa kufanyika Belém, Brazil.

“Kama unavyofahamu sisi Tanzania ni mwenyekiti wa AGN kwa mwaka mzima ambapo kamati hii ilielekezwa tuwe na Sekretarieti ya kudumu ambayo itakuwa na makao makuu pake Addis Ababa nchini Ethiopia na sisi tumeahidi kabla ya mwezi Juni tutaunda kamati ya kusimamia mchakato huo,” alisema Dkt. Muyungi.

Dkt. Muyungi ambaye pia ni Mshauri wa Rais kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira aliongeza kuwa imeazimiwa kuwa Afrika itaendelea kushirikisha, kufundisha na kujenga uwezo wa vijana kupitia kliniki za mabadiliko ya tabianchi kuhakikisha inarithisha ujuzi kwa vizazi kutetea maslahi ya Afrika katika majadiliano ya kimataifa.

Mkutano huo ulifunguliwa tarehe 28 Aprili 2025 na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YANOGESHA MEI MOSI 2025

 

.……....

Na Sixmund Begashe - Singida

Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Leo tarehe 1 Mei 2025, wameungana na wafanyakazi wote Duniani kwenye Maadhimisho Siku ya wafanyakazi Duniani MEI MOSI ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Singida huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Mgeni rasmi.

Maadhimisho hayo yalipambwa na matembezi mbele ya jukwa kuu mapoja na burudani mbalimbali ambapo Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii walinog'esha maadhimisho hayo kwa Mavazi rasmi na mabango yaliyobeba ujumbe wa kutangaza vivutio vya Utanii na kuhamasisha Uhifadhi.

   

MAHUSIANO MAZURI KATI YA SERIKALI NA TAASISI ZA DINI NI CHACHU KATIKA HUDUMA BORA ZA AFYA.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii , Ofisi ya  Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume amesema mahusiano mazuri kati ya Serikali na taasisi za dini yamekuwa chachu katika kufanikisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Dkt. Mfaume ameyasema hayo hivi karibuni  mara baada ya kutembelea katika Hospitali ya Cardinal Rugabwa inayomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki la  Dar es Salaam katika ziara yake inayoendelea mkoani huku yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii.


“Hapa tunaona mitambo kikubwa ya kutolea huduma za afya, Serikali imeiweka mazingira mazuri ya ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini zote ikiwa ni pamoja na uwekezaji kwenye Sekta ya afya” amesema Dkt.Mfaume

Aidha, Dkt. Mfaume amezitaka timu za usimamizi wa afya (CHMT) katika Halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi hizo kwa kuwa zinatekeleza majukumu hayo kwa niaba ya Serikali.


Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Sr.Dkt. Sarah Deogratius amesema ziara ya Mkurugenzi katika Hospitali hiyo imewatia moyo wa  kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

SERIKALI KUTAMBULISHA LESENI MPYA MAALUM YA UZALISHAJI CHUMVI

 

▪️Waziri Mavunde aelekeza mchakato wa mabadiliko ya sheria kuanza.


▪️Aelekeza kanuni kubadilishwa kupunguza tozo kwa hekta kufikia 20,000.


▪️Wazalishaji Chumvi wampongeza Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa ujenzi wa kiwanda cha Chumvi Mkoani Lindi


▪️Serikali kuwezesha wazalishaji chumvi kumiliki viwanda vya kuchakata chumvi


*Dodoma*


Serikali ipo mbioni kutambulisha Leseni mpya ya uzalishaji wa chumvi ili kuiondoa chumvi katika kundi la madini mengine na hivyo kuchochea ukuaji wa tasnia ya uzalishaji chumvi nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde na Uongozi wa Chama cha Wazalisha Chumvi Tanzania(TASPA),kikao ambacho kimelenga kuboresha sekta ya madini kupitia tasnia ya chumvi.


“ Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan ametupa maelekezo mahususi kuwezesha wachimbaji wa madini na wazalishaji wa madini chumvi nchini ili kuchochea ukuaji wa sekta ya madini.

Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu cha uwepo wa Leseni moja ya uzalishaji wa Chumvi ambayo itasaidia kumuendeleza mzalishaji chumvi kwa kupunguza gharama za uzalishaji na kuyaondoa madini chumvi katika kundi la madini mengine.


Naelekeza kuanza mara moja mchakato wa mabadiliko ya sheria ili kuruhusu uanzishwaji wa Leseni maalum ya uzalishaji chumvi ambayo pia tozo yake kwa hekta iangaliwe upya kufikia 20,000 kutoka kiwango kilichopo sasa.


Dhamira ya serikali ni kuona wazalishaji wa chumvi wanaongeza tija na kufikia hatua ya kumiliki viwanda vya uchakataji na usafishaji chumvi nchini ili chumvi yetu iwe yenye ubora na shindani” Alisema Mavunde

Aidha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Eng. Yahaya Samamba ameipongeza TASPA  kwa kazi ya kuwaendeleza na kuwasimamia wazalishaji chumvi na kuahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Wizarani katika utatuzi wa changamoto za wanachama wake.

Akitoa  maelezo yake,Mwenyekiti wa TASPA Bi. Hawa Ghasia ameipongeza wizara ya madini kwa utaratibu wa kuwasikiliza wadau na kutafuta suluhisho ya changamoto zao na kutumia fursa hiyo kumpongeza kipekee Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kusikia kilio cha wazalishaji wa chumvi kwa kujenga kiwanda cha Kuchakata na kusafisha chumvi kinachojengwa mkoani Lindi na Shirika la Madini la Taifa(STAMICO).

UZUSHI NA UONGO KUHUSU MACHINJIO YA VINGUNGUTI UFAFANUZI WATOLEWA NA MEYA KUMBILAMOTO

 

Meya Kumbilamoto  akizungumza na Viongozi wa Wafanyabiashara wa Machinjio ya Vingunguti  ,kikao hiki kilikuwa cha kufafanua Uvumi na Uzushi  Uongo   ulioleta hofu na Taharuki   kwa wachinjaji na wafanyabiashara wa machinjio ya Vingunguti 


Uvumi huo ni kuwa eti Machinjio ya Vingunguti imeuzwa kwa Mwekezaji  na wafanyabiashara wataondolewa  kuchinja mle ndani  watapelekwa  Pugu  ktk ufafanuzi wake Mh Meya ni kuwataka wafanyabiashara kupuuza Mbuli Kumlomo za walimwengu  waendelee na biashara zao km kawaida huku serikali ya Mh 

Rais Dkt Samia ikiendelea kulinda ajira zao na kuboresha biashara zao , wenyeji wa Dar wa Salaam Mtakumbuka kulikuwa na uvumi miaka ya 1990 pale kituo cha polisi buguruni Mtu kageuka CHATU kumbe ni uzushi 


Upatapo taarifa hii mjulishe na mwenzio  kupuuza upuzi huu Safari ya kuifanya Vingunguti kuwa Mji unaovutia kama Istanbul  au Brunei  inaendelea tutaendelea kuwapiga Spana  Mbuli Kumlomo wote 

Kazi    Utu   Tunasongambele mimi Mtumishi wenu Kumbilamoto  .