Na.Moshi said
Dar es salaam
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepokea ugeni kutoka Idara ya Huduma za Hali ya Hewa ya Zimbabwe (MSD) uliowasili nchini kwa ziara ya mafunzo yenye lengo la kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu huduma za hali ya hewa.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za MSD kuboresha huduma zao kwa kujifunza kutoka kwa TMA, taasisi iliyotambuliwa kwa mafanikio yake makubwa katika kuimarisha huduma za hali ya hewa nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Ugeni huo umeichagua TMA kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya huduma za hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa, ushirikiano wa kikanda na kimataifa, pamoja na utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati kwa umma na wadau mbalimbali.
TMA imeeleza kufurahishwa na ziara hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine barani Afrika kwa lengo la kuboresha huduma za hali ya hewa na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
KUHUSU TMA
TMA ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na. 2 ya mwaka 2019, kupitia Tangazo la Serikali Na. GN 459 la tarehe 14 Juni 2019. Mamlaka hii ina jukumu la kuratibu, kudhibiti na kutoa huduma za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali, huduma za hali ya hewa nchini zilitolewa na Wakala wa Hali ya Hewa Tanzania, uliokuwa umeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala (Executive Agencies Act), Sura Na. 245, marejeo ya mwaka 2022.
Kabla ya kuanzishwa kwa wakala, huduma hizo zilitolewa na Idara ya Hali ya Hewa (Directorate of Meteorology) iliyoundwa mwaka 1977, kufuatia kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Idara hiyo ilitekeleza jukumu la kutoa taarifa na uangalizi wa hali ya hewa nchini.
Kabla ya hapo, huduma hizo zilitolewa chini ya taasisi ya wakoloni waliokuwa wakitawala wakati huo.
TMA ipo chini ya Wizara ya Uchukuzi na inasimamia Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kilichopo Kigoma, ambacho hutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wataalamu whali ya hewa nchi
0 comments:
Chapisha Maoni