Ampongeza Dr samia kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mikubwa
USAGARA:
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), *CPA Amos Makalla* amesema kukamilika kwa daraja la Kigongo -Busisi, mradi wa SGR na meli itachochea biashara na kukuza uchumi wa wananchi wa kanda ya ziwa.
Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo ambayo iliyoasisi na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati Dk John Pombe Magufuli na kuanzisha miradi mingine mipya.
Makalla ameeleza hayo leo Mei 21,2025 wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Usagara Wilaya ya Masungwi mkoani mwanza akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Shinyanga.
Makalla amesema amepita kueleza jitihada za serikali na kazi nzuri inayofanya
“Daraja hili ni kubwa lazima wana Mwanza waelewe kuwa ni kubwa na muhimu, ni daraja kubwa namba tano kwa Afrika na umehimubwake mbali ya kurahisisha usafiri lakini daraja hili litaongeza biashara na kukuza uchumi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa ya Jirani,”amesema Makalla
Ameongeza kuwa magari kutoka nchi jirani za Kongo na Rwanda yatapata ambayo yatasaidia kukuza uchumi.
Pia mradi wa pili ambao Rais Samia aliahidi na kuanzisha ni kuendsleza kipande cha kutoka Dodoma hadi Makutupola kwenda Tabora, Isaka hadi Mwanza na alianza kwa kumalisha kipande kilichokuwa kimebaki kutoka Dar es salaam hadi Dodoma.
Pia mradi mwingine ni mradi wa Meli ya MV Mwanza ambayo aliikuta imefikia asilimia 60 ya utekelezaji wake na aliondoka ikiwa imefika asilimia 98 lakini hadi sasa imekamilika itafanya safari kuanzia Mwanza, Bukoba hadi Uganda.
0 comments:
Chapisha Maoni