Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komred Kheri James amewatembelea Wananchi katika Vijiji vya Tarafa ya Mlolo lengo likiwa ni kukagua miradi ya maendeleo, kuhamasisha shughuli za maendeleo na kuwasikiliza Wananchi.
Akizungumza na Wananchi katika kijiji cha Ihemi, Itwaga na Wenda Komred James amewahimiza Wananchi kuchapa kazi, umuhimu wa elimu, umuhimu wa lishe bora, Ulinzi na usalama, Faida za kupima, kupanga na kumilikisha aridhi pamoja na kuzingatia mpango wa Matumizi bora ya aridhi.
Katika ziara hiyo Wananchi wameipongeza Serikali kwa kuwajengea mradi wa maji, Ukarabati wa Zahanati na ujenzi wa miondombinu ya elimu na Barabara.
Ziara ya Kijiji kwa Kijiji wilayani Iringa ni mkakati maalumu wa kuwafikia Wananchi na kupata fursa ya kuwasikiliza na kuwapa taarifa juu ya mafanikio, mipango na maelekezo mbalimbali ya Serikali ili kujenga uelewa wa pamoja.
0 comments:
Chapisha Maoni