Jumatatu, 16 Juni 2025
BEI YA KUJAZA GESI (LPG) KWA MATUMIZI YA KUPIKIA NI HIMILIVU – KAPINGA
MKOMI AKAGUA BANDA LA MALIASILI.
WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA,KATIBU MKUU ATEMBELEA BANDA LA NCC
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma S. Mkomi akisoma maelezo kwenye Banda la Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) alipotembelea banda hilo leo akiwa na viongozi wengine mbalimbali kutoka katika ofisi yake.
ETDCO YAKAMILISHA MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KILOVOLTI 132 TABORA - KATAVI
TRA WAAGIZWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTUMISHI WA UMMA
Jumapili, 15 Juni 2025
SERIKALI YAHAMASISHA WADAU KUWEKEZA KATIKA UTALII ENDELEVU
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa wito kwa wadau katika sekta ya utalii kuongeza uwekezaji na juhudi za pamoja katika usimamizi wa utalii katika maeneo yanayolindwa ili kuwa na Utalii endelevu.
Mhe. Khamis ameongeza kuwa kuwekeza katika utalii wa maeneo yaliyolindwa sio tu kunafaida kwa uhifadhi, bali pia unahamasisha maendeleo ya kimkakati ya jamii inayozunguka maeneo hayo.
Akifungua warsha ya kujadili umuhimu wa Uhifadhi, Ukuaji wa Utalii na Ustawi wa Jamii iliyofanyika kwenye hotel ya Mt. Meru jijini Arusha leo tarehe 14.06.2025 amesema ni wakati sasa wadau kujitokeza kwa wingi kuwekeza na kujikita katika usimamizi wa Rasilimali za utalii ili ziweze kutuletea faida kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Pia amesisitiza juu ya umuhimu wa kubadilishana uzoefu utakaosaidia katika kuchunguza fursa zilizopo kwenye Maliasili zitakazoweza kunufaisha jamii kama kichocheo muhimu cha maendeleo.
Amesema bila wanayama hakuna Utalii, bila misitu hakuna utalii hivyo ni vyema tukahamasisha watu kutumia nishati safi ili kuendelea kutunza misitu yetu, kulinda na kuhifadhi wanyama wetu ili utalii uendelee na uingize pato kwa Taifa na jamii ya maeneo husika ipate manufaa.
Akizungumza wakati wa warsha huyo ya Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Kanda ya Tanzania Nathan Belete amesema kukuza ushirikiano kati ya wadau ni njia bora ya kusaidia juhudi za uhifadhi.
"Utafiti umeonesha kuwa utalii katika maeneo yanayolindwa una faida kubwa, unatoa ajira, na unaingiza Taifa pato kubwa ambalo hurudishwa kwa jamii kwa kuwekezwa katika miradi ya maendeleo’
Alibainisha kuwa, katika baadhi ya nchi, kila dola moja iliyowekezwa katika maeneo yanayolindwa huzalisha hadi dola 28 ambapo ni faidi kwa jamii na Taifa lwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda kutoka Benki ya Dunia Anna Wellenstein amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na mafunzo
"Warsha hii imetujengea uwezo kwamba rasilimali asilia si muhimu tu kwa bioanuai ila pia ni injini yenye nguvu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii," alisema.
Amesema mkutano huu wa siku mbili umtengeneza jukwaa lililowezesha washiriki kujifunza kutoka kwa kila mmoja kati ya nchi na nchi, Taasisi kwa Taasisi, Sekta binafsi pamoja na wadau wa utalii.
Warsha hii ya siku mbili imehudhuriwa na wataalamu wa kitaifa na kimataifa zaidi ya 100 kutoka katika Taasisi za Serikali, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, na washirika wa maendeleo kujadili mambo muhimu ya kuhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.
Jumamosi, 14 Juni 2025
RAIS SAMIA NA RAIS WA BENKI YA AFRIKA AfDB WAKAGUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE MSALATO
Muonekano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025. ujenzi wa Kiwanja hicho cha Msalato unahusisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway) jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na Miundombinu mengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Nala Jijini Dodoma mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato pamoja na ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma yenye urefu wa km (112.3) tarehe 14 Juni, 2025.
Matukio mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Nala Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.
DC MSANDO AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA MAZINGIRA MKOA WA DAR,ASISITIZA NISHATI SAFI

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Albert Msando akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya mazingira kimkoa ambayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Makuburi kwenye Wilaya hiyo Leo tar 14/6/2025.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya mazingira kimkoa ambayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Makuburi Ubungo Leo tar 14/6/2025 jijini Dar es salaam.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya mazingira kimkoa ambayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Makuburi Ubungo Leo tar 14/6/2025 jijini Dar es salaam.
...........................
NA MUSSA KHALID
Serikali imeendelea kuweka msisitizo wa kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kwa shughuli za kupikia ili kuepukana na changamoto ya uharibifu wa mazingira.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam katika maadhimisho ya Siku ya mazingira kimkoa ambayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Makuburi kwenye Wilaya hiyo,yakienda sambamba na kauli mbiu ya "Mazingira yetu na Tanzania Ijayo,tuwajibike sasa dhibiti matumizi ya Plastiki"
DC Msando amesema kuwa kauli mbiu hiyo inatoa chajizo la kila mwananchi kuhakikisha anahifadhi mazingira ikiwemo kuhamasisha na kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa mazingira kwa kudhibiti matumizi ya plastika.
"Nitoe wito kwa vyombo vya Habari,taaisisi zote za serikali na zisizoza serikali pamoja na wadau mbalimbali kushirikiana katika kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza uharibifu wa mazingira nchini Kwa kudhibiti matumizi ya Plastiki"amesema DC Msando
Aidha amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ameziagiza Halmashauri zote katika Mkoa huo kuendeleza juhudi za ukusanyaji wa taka ngumu na laini ili kudumisha usafi wa mazingira kwenye maeneo yao.
Pia amewaagiza wakandarasi wote waliopewa kazi ya kukusanya taka kwenye Mkoa huo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kimkataba Kwa ufanisi.
Awali wakizungumza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinonondoni Songoro Mnyonge amesema wataendelea kutoa elimu ikiwemo kuhamasisha matumizi ya nishati safi huku Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha akisisitiza kuthaminiwa Kwa watu wanaofanya shughuli za kuokota na kukusanya taka katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bonde la Wamiruvu Mkoa wa Dar es salaam Bi Diana Kimbute amesema mazingira yanapotunzwa ndivyo pia vyanzo vya Maji vinatunzwa.
Katika Maadhimisho yao yamezikutanisha kwa pamoja Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam ambapo pia wameshiri wadau kutoka Taasisi mbalimbali wa mazingira ikiwemo Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya HUDEFO,Taasisi zinazojihusisha na masuala ya nishati,wanafunzi na wazalishaji wa mitungo ya gesi

