JSON Variables

Sunday, April 27, 2025

GESI YA HELIUM YAGUNDULIKA KINA CHA KM 1.14 CHINI YA ARDHI

 

●  Utafiti wafanyika katika visima vinne

● Utafiti umegundua gesi ya Helium yenye ubora wa mkusanyiko wa asilimia 7.9 na 5.5

● Zaidi ya ajira 100 zatolewa kwa jamii


Momba, Songwe.


Imeelezwa kwamba utafiti wa gesi ya helium uliofanywa na kampuni ya HeliumOne nchini Tanzania  umefanikiwa kupata gesi hiyo katika umbali wa kilomita 1.14 kutoka chini ya ardhi katika visima vya Itumbula West 1 na Tai 3.


Msimamizi wa mradi huo Emmanuel Ghachocha alibainisha kwamba, majibu ya utafiti katika kisima cha Itumbula West 1 yalionesha kuwa na wingi wa mkusanyiko wa gesi ya helium juu ya kisima yenye ubora wa kiwango cha asilimia 7.9 jambo lililoleta matumaini ya kuendelea na utafiti wa kina.

Ghachocha alifafanua kuwa, utafiti wa kina (Extended Well Test) ulionesha uwepo wa mkusanyiko wa gesi hiyo kwa kiwango cha asilimia 5.5 iliyopanda juu ya ardhi  kutoka  kisima cha Itumbula West1 ambayo ubora wake ni mzuri kulingana na majibu ya sampuli zilizochunguzwa katika maabara mbalimbali ndani na nje ya nchi.


Akielezea kuhusu matumizi ya teknolojia katika utafiti hususan katika utumiaji  wa mashine za kisasa kwenye  utafiti Ghachocha alisema kuwa, kampuni ya Helium One ilifanikiwa kununua mitambo yake yenyewe ikiwamo winchi za unyanyuaji vifaa pamoja na mtambo wa uchimbaji (Predator drilling rig) jambo ambalo limeongeza ufanisi katika kipindi cha utekelezaji wa utafiti huo.


Kuhusu Mpango wa Wajibu wa Kampuni kwa Jamii inayozunguka Mgodi (CSR) Ghachocha alisema kuwa, mpaka sasa kampuni imetoa  ajira za kudumu na zisizo za kudumu zaidi ya 100 zimetolewa na kampuni kwa jamii inayozunguka   mgodi na nje ya mgodi.

Sambamba na hapo mwaka 2021/2022 kampuni ilichangia zaidi ya milioni 50 katika maboresho ya shule za  Kata ya Itumbula, Mpapa, Mkulwe na Ivuna.


Mwaka 2023 kiasi cha shilingi milioni 54 zilitolewa na  heliumOne katika kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mkonko na kutoa msaada wa vifaa tiba na samani za  zaidi ya takribani shilingi milioni 20 kwa ajili ya zahanati hiyo na kituo cha afya cha Kamsamba. Pia takribani shilingi milioni 15 zilitolewa  kwa jamii ya  Itumbula iliyopata madhara ya kimbunga.


Itakumbukwa kwamba kampuni ya HeliumOne iliwasilisha maombi ya leseni ya madini kwa ajili ya eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 480 lililojumuisha Bonde la Rukwa Kusini , mwezi Machi 2025 Helium One ilikubali rasmi ofa ya leseni hiyo kutoka Wizara ya Madini kwa hatua za utekelezaji wa uzalishaji wa gesi hiyo nchini.


*#*Vision2030: MadiniNiMaishanaUtajiri*

*#*MineralValueAddition*

*#*InvestInMiningSector*

SIKU HAZIGANDI HATA UKIZIWEKA KWENYE FRIJI

 

Macho na akili za mashabiki wa mpira wa miguu nchini tanzania na duniani kote waliokuwa wakiisubilia siku ya leo tarehe 27.04.2025 kuushuhudia mtanange wa maamuzi makubwa sana , Baadhi ya mashabiki wa club ya Simba wamesema wapotayari kufanya chochote na popote imradi timu yao iweze kushinda


Juma hamis ni mkazi wa Temeke Mwembeyanga anasema yeye ni mnazi wa club ya Simba na leo hii simba anaibuka na ubingwa na kusonga kwenye fainali kisha kurudi na kombe nyumbani baada ya ushindi katika fainali itakayo fanyika baada ya Simba kushinda mechi ya leo ninafuraha sana kwa sababu hii siku niliisubilia kwa hamu sana nimeamini kwamba SIKU HAZIGANDI HATA UKIZIWEKA KWENYE FRIJI


Kwa upande wake Rose Anthony mkazi wa Dodoma ambaye yeye ni shabiki kindaki ndaki wa club ya Young Africans, Amesema watani wetu wameweza kupiga hatua kubwa sana kufikia hii leo kiasi kwamba ninawivu sana kwaajili yao, japokua mimi ni shabiki wa yanga sina kinyongo na watani wetu wa jadi kwa sababu wanacho kifanya wanaiwakilisha Taifa kiujumla kwa hiyo sina budi kuwa shabikia katika michuano hii ya kimataifa, wamalize salama waje na kombe nyumbani lakini wajue kwamba kwenye ligi yetu ya NBC sisi ndiyo mabingwa licha ya viporo walivyo bakisha


BIG SCREEN ya kumuangalia Mnyama akitinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika inakusubiri pale viwanja vya Mbagala Zakhiem. Mo Cola wamesimamia mpango mzima kufanikisha hili.

NJE SPORTS YAICHABANGA WIZARA YA AFYA

 

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) imeendelea kuonesha ubora mkubwa kwa kuichapa Wizara ya Afya na kufuzu hatua ya nusu fainali katika mchezo wa mashindano ya Mei Mosi uliopigwa katika uwanja vya Airtel, eneo la Mtipa mkoani Singida. 


Mchezo huo uliokuwa wa kuvutia, ulimalizika kwa sare ya 1-1 katika dakika 90 za kawaida ambapo mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penati na Nje Sports iliibuka kidedea kwa penati 4-2.


Kocha Mkuu wa Nje Sports, Bw. Shaban Maganga, ameonyesha furaha yake kutokana na juhudi kubwa za wachezaji wake waliopambana hadi mwisho wa mchezo. Ameeleza kuwa nidhamu na utekelezaji mzuri wa maelekezo ndio silaha ya ushindi wao.


"Nawapongeza wachezaji kwa kuonesha nidhamu na kufuata maelekezo, ndiyo siri ya ushindi wetu leo. Tunaendelea kujiandaa zaidi kwa nusu fainali." Alisema kocha Maganga.


Mwenyekiti wa timu, Bw. Ismail Abdallah, naye hakuficha furaha yake, akieleza kuwa ari ya wachezaji na sapoti waliyoipata kutoka kwa uongozi wa wizara ndiyo iliyowasaidia kupata matokeo mazuri.


"Wachezaji wameonyesha juhudi kubwa. Salamu za hamasa tulizopokea leo kutoka kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara yetu zimewapa nguvu ya ziada. Tunapambana hadi kulichukua kombe," alisema.


Mashindano haya ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi kitaifa, yakihamasisha mshikamano na afya miongoni mwa watumishi wa umma.

MBETO : INEC, ZEC TUME HURU ZA UCHAGUZI ZENYE UWAZI NA HAKI

 

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeutaka Upinzani kutozibeza  Tume za   Uchaguzi , INEC na ZEC  na kudai si huru wakati  Chadema na ACT  Wazalendo , vimekuwa vikiongeza idadi  vya Viti vya Udiwani ,Uwakilishi, Ubunge  na kupata kura nyingi  za urais   .


CCM kimesema Tume hizo ziko huru na kutenda haki zikiongozwa na  binadamu na kwamba  Tume  yoyote  itakayoundwa kwa mfumo wowote ,  zitaendelea kuongozwa na binadamu si  Malaika  .


Matamshi  hayo yametamkwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zazibar Idara ya Itikadi  , Uenezi na Mafunzo , Khamis  Mbeto  Khamis ,  aliyesema madai ya upinzani kuhusu  Tume za Uchaguzi  hayana mantiki  , mashiko na  kukosa  nguvu  ya hoja.


Mbeto  alisema  grafu ya idadi ya Viti vilivyokwenda upinzani , kuanzia Mwaka 1995 hadi 2020, imekuwa ikipanda katika    Uchaguzi za  Serikali za Mitaa, Udiwani, Uwakilishi ,Ubunge  na kuongezeka kura za Urais. 


Alisema katika Uchaguzi Mkuu  wa Kwanza Mwaka 1995 , NCCR-MAGEUZI  na CUF , vilipata Viti   kwa uchaguzi wa   Tanzania  Zanzibar , ambapo  CCM  mwaka huo ilipata Viti   24  na CUF 23  vya Ubunge na  Uwakilishi.


"Nafikiri   maana ya uwazi na  demokrasia   kwa upinzani hadi itangazwe CCM kimeshindwa  kura  za urais. Uchaguzi ni  mchakato wa  kukubalika  kwa chama cha siasa na wananchi .  CCM kina  Mizizi mirefu ,  Nyenzo, Rasimali Fedha na watu kuliko Upinzani " Alisema Mbeto 


Hivyo  basi, Mwenezi  huyo katika maelezo  yake ,alisema, haiwezekani  vyama  vilichosajiliwa Mwaka 1993 na kuendelea  , kama  Chadema  NCCR-MAGEUZI ,  CUF , ACT au CHAMA viwe na  ubavu wa  kukiangusha CCM .


"CCM  ni jiti  kubwa lenye Matawi  mapana na    Mizizi mirefu .Gogo na shina la  mti  wake halikatiki kirahisi  . Kuchuana na CCM  katika  Uchaguzi kunahitajika upinzani  wenye  mbavu nene za  kisiasa   " Alisisitiza Mbeto 


Aidha  Katibu huyo Mwenezi  akitoa mfano, alisema   uchaguzi wa Mwaka 2015, Chadema  kilipata Viti vya Ubunge maeneo  ya Mijini na kukosa  Vijijini ,  kutokana na uchanga wake kisiasa. 


Mbeto  alitaja kuna Wabunge wa Chadema  wamekuwa bungeni  kwa   zaidi ya  vipindi viwili  ,ushindi  wao  umetangazwa na  Tume  ambazo leo  wanaibeza na kudai  si huru. 


'Kina Tundu Lissu, John Heche, John Mnyika, Godbless Lema, Halima Mdee ,Ester Bulaya, Boniface Jackob ,Peter Msigwa, Said Kubenea na joseoh Mbilinyi wote wametangazwa washindi na  Tume ya uchaguzu iliopo sasa  " Alieleza Mwenezi  huyo 


Akizungumzia Katiba  ya Tanzania na Zanzibar , Mbeto alisema Katiba hizo , zimeongoza nchi  kwa miaka    61 bila   misukosuko  ya aina yoyote,  kila  katika wakati  mgumu Katiba  hizo zilitoa majibu  na kuelekeza.



'Serikali ya   Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliunda  Tume iliokusanya maoni ya wananchi ilioongozwa na  Joseph Warioba. Likaundwa Bunge Maalum la Katiba.  Ilipoandikwa Katiba  inayopendekezwa. Chadema na CUF  wakawatoa wabunge wao kabla ya Bunge  Maalum la katiba hakijafikia tamati " Alisema 


Mbeto alieleza kuwa  leo  unapoisoma Katiba  iliopendekezwa kwa utuo ,  utulivu  na umakini, utaona ilivyozingatia changamoto  na kutekeleza ushauri na maoni   yaliotolewa na watanzania  kwa ustadi na mazingatio .

HALI YA UMEME ARUSHA YAZIDI KUIMARISHWA

Dkt. Biteko aipongeza TANESCO kuendelea kuwapa watanzania huduma ya umeme wa uhakika


 Ni kufuatia upanuzi wa Kituo cha kupoza umeme cha Njiro


Kituo chafungwa transforma yenye MVA 210 kutoka MVA 90 ya awali 

NA MWANDISHI WETU 

Mkoa wa Arusha sasa umewezeshwa kupata umeme wa uhakika baada ya upanuzi wa Kituo cha kupooza na kusafirisha umeme cha Njiro, kwa kuongeza Transfoma yenye uwezo wa MVA 210 kutoka MVA 90 ya hapo awali.

Akizungumza na wananchi katika hafla za Sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mkoani Arusha, mara baada ya kuzindua kituo hicho Aprili 28, 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kwa ajili ya upanuzi wa Kituo hicho ili kukiongezea Kituo uwezo kuendana na ongezeko la matumizi ya umeme.

“Katika ukanda huu, mahitaji ya umeme kwenye Mkoa wa Arusha ni megawati 107, Tanga Megawati 126, Manyara Megawati 14, na Kilimanjaro Megawati 68, na leo tumezindua upanuzi wa Kituo cha kupoza umeme cha Njiro, ambacho kina njia kumi za kusambaza umeme katika Mkoa wa Arusha na kuuwezesha Mkoa huu kukidhi mahitaji ya umeme kufikia Megawati 200 kulinganisha na mahitaji ya sasa ambayo ni Megawati 107” amesema Mhe. Dkt. Biteko

Aidha Mhe. DKt. Biteko amesema kuwa Serikali ipo kwenye mpango wa utekelezaji wa kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme ikiwa ni maagizo ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha miundombinu ya umeme chakavu yote inafanyiwa ukarabati wa njia za kusafirisha umeme. 

“Umeme tunaweza kuwa nao kwenye uzalishaji, lakini ikawa changamoto kwenye miundombinu, ndio maana Mhe. Rais ametuagiza sasa kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme ili tuwe na umeme wa uhakika, alisema Mhe. Dkt. Biteko.

Ameongeza kwa kusema kuwa Wizara ya Nishati imekusudia kuhakikisha kila Mtanzania anapata kipande cha keki ya Nishati hasa Nishati ya umeme.

“Nilipoteuliwa niliwaambia, TANESCO hamtalala usingizi, na wote mnashuhudia kuwa hali ya umeme imebadilika sio kama miaka kumi nyuma, na TANESCO kwa kweli hawalali wanafanya kazi nzuri” alisema Mhe. Dkt. Biteko.

Kukamilika kwa Kituo hicho kutaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo Mkoa wa Arusha na kuifungua kiuchumi kwa kukuza Sekta za Utalii, Viwanda na Biashara.

MKUU WA MKOA SINGIDA HALIMA DEDENDEGO AIPONGEZA TASAC KWA UTEKELEZAJI WAKE WA MAJUKUMU YA SEKTA HIYO.

 

NA MWANDISHI WETU, SINGIDA

MKUU wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa utekelezaji wa majukumu yake ya kuhakikisha Sekta ya usafiri majini inachangia kukuza Uchumi wa Taifa.


Ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea Banda la TASAC, Jana tarehe 26 Aprili,2025 katika Maonesho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mandewa mkoani Singida.


“Sekta ya usafiri majini inakua kwa kasi sana, hivyo natoa rai kwa TASAC kuendelea kusimamia sekta hii ili iweze kuleta mabadiliko katika nchi,” amesema Mhe. Dendego.


Akiwa katika banda hilo Dendego alipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi, Bi. Mariam Mwayela kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAC ikiwemo kudhibiti na kusimamia usalama, ulinzi wa vyombo vya usafiri na utunzaji wa mazingira majini; udhibiti wa huduma za usafiri majini pamoja na kutoa huduma ya uwakala wa forodha kwa bidhaa mahsusi kwa mujibu wa Sheria.  


“Sisi kama TASAC tumekasimiwa majukumu ya kudhibiti na kusimamia usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira ya vyombo vya usafiri majini na kuhakikisha vyombo, abiria na mizigo vinakua salama lakini pia kwa kuzingatia miongozo ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi kuhakikisha watumishi wote wanakuwa katika hali ya usalama katika mazingira wanayofanyia kazi,” amesema Bi. Mwayela.


Katika maonesho hayo, wadau mbalimbali wametembelea Banda la TASAC akiwemo Mwenyekiti wa TUICO Taifa Bw. Paul Sangeze.


TASAC ni moja ya taasisi zinazoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya OSHA yenye kauli mbiu “ Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidijitali katika kuimarisha Usalama na Afya Mahali Pa Kazi". 


Maonesho haya yanatarajiwa kufikia kilele mnamo tarehe 30 Aprili, 2025.

HABARI KUBWA ZILIZO PEWA NAFASI KWENYE KURASA ZA MBELE YA MAGAZETI LEO TAREHE 27.04.2025

 Good morning, Habari gani popote ulipo mdau wetu kupitia Mkisi Digital, Nikukaribishe kupitia vichwa vya habari magazetini leo Jumapili 27.04.2025




Inafahamika kwamba mpira wa nimchezo wa makosa, Je, unadhani ni wapi simba akikosea basi ataondoshwa kwenye mashindano, Unadhani Simba atatoboa?









Baada ya kumaliza kupitia vichwa vya MAGAZETI basi tunajali sana maoni yako, tupe maoni yako kwa kile kicha habari ambacho kimekubamba.

Saturday, April 26, 2025

DKT. NATU MWAMBA ATETA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MFUKO WA CIF, JIJINI WASHINGTON MAREKANI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Uwekezaji katika Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Investment Funds (CIF), Bi. Tariye Gbadegesin, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe, ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia ya mwaka 2025, inayofanyika jijini Washington D.C nchini Marekani.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Jijini Washington, Dkt. Mwamba na mgeni wake, wamejadiliana masuala kadhaa kuhusu jinsi Mfuko wa CIF unavyoweza kusaidia juhudi za Tanzania katika kutekeleza Mpango wa Nishati (Energy Compact) na kuendeleza vipaumbele vya matumizi ya Nishati safi.