JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Gospel. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Gospel. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 23 Mei 2025

SERIKALI IMETOA RUZUKU YA ASILIMIA 20 HADI 50 KWENYE MITUNGI YA GESI LAKI 4.4 – KAPINGA


📌 *Asema lengo ni kupunguza gharama na kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia*


*📌  REA kusambaza majiko banifu 200,000 kwa punguzo la hadi asilimia 75*


📌 *Baada ya umeme kufika kwenye vijiji vyote; Serikali kuendelea kuhamasisha matumizi ya majiko ya umeme*



Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali imetoa ruzuku ya asilimia 20 hadi 50 kwenye mitungi ya gesi ya LPG takribani 452,445 kwa watumiaji wa mwisho ikiwa ni jjtihada za kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.


Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 23, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Grace Tendega aliyetaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa muda mfupi wa kuhakikisha Wananchi wa Vijijini wanatumia Nishati Safi ya kupikia badala ya Kuni na Mkaa.

 

"Mheshimiwa Mwenyekiti Serikali kupitia REA pia  itasambaza majiko banifu 200,000 yenye bei ya punguzo la hadi asilimia 75 pamoja na kuwezesha ufungaji wa mifumo ya nishati safi ya kupikia katika Taasisi za Umma zinazohudumia watu zaidi ya 100."  Amesema  Kapinga


Aidha, amesema Serikali imekamilisha kazi ya usambazaji umeme katika vijiji vyote hivyo kwa sasa inaendelea kuhimiza matumizi ya majiko ya kupikia yanayotumia umeme ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa vijijini badala ya kutumia kuni na mkaa.


Mhe. Kapinga ametanabaisha  kuwa, Mkakati wa Taifa wa  Nishati Safi ya Kupikia ni wa miaka kumi lakini Serikali inao mkakati wa matumizi bora ya nishati ambao unahusisha pia sekta binafsi kwa ajili ya kusaidia kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.


Akijibu swali la Mbunge wa Mbulu, Mhe. Zacharia Isaay aliyeuliza Serikali imejipangaje kuhakikisha Vitongoji vyote vilivyokusudiwa katika mwaka huu wa bajeti kufikiwa  na umeme katika kipindi cha mwezi mmoja uliobaki, Mhe. Kapinga amesema Serikali inayo mikakati na miradi mbalimbali ya kupeleka umeme katika Vitongoji. 


Amesema kuwa, moja ya mikakati hiyo ni kupeleka umeme katika Vitongoji 15 kwa kila Jimbo, na pia  Serikali imekuja na mkakati wa kupeleka umeme katika Vitongoji 20,000 ambapo   awamu ya kwanza inaanza kupeleka umeme katika Vitongoji 9000 na hatua iliyopo ni utafutajj wa wakandarasi.


Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Anatropia Theonest aliyeuliza bei ya Serikali ya ruzuku imeanza kutumika lini kutokana na mitungi ya gesi kuendelea kuuzwa kati ya 22,000/- na 25,000 na kwa mitungi mikubwa ya kilo 15 shilingi 50,000/- na 60,000/-,  Mhe. Kapinga ameeleza kuwa kwa maeneo ya mjini Serikali imepeleka ruzuku hadi asilimia 25 na maeneo ya Vijijini ni kati ya asilimia 50 hadi 75 na kutolea mfano iwapo mtungi ulikuwa unauzwa shilingi 45,000/- kwa bei ya ruzuku inapatikana kwa shilingi 17,000/- hadi 21,000/- na kusema ni zaidi ya nusu ya bei yake.


Ameongeza kuwa, katika kila Wilaya kuna takribani mitungi 3,255 inayopatikana kwa ruzuku na kuongeza kuwa ndio kwanza mkakati umeanza.


Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Yustina Rahhi alieuliza mpango wa Serikali kuwapelekea jamii ya wafugaji teknolojia ya biogas au kuwajengea majiko yanayotumia samadi ya gesi ambayo ni rahisi, Mhe. Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi huo kupitia umoja wa Ulaya (mfuko wa UNCDF) ambao unateknolojia alizozitaja Mhe. Mbunge.


Akijibu swali la Mbunge wa Nyang’wale, Mhe. Hussein Amar aliyeuliza kuhusu mpango wa Serikali kuzipelekea nishati safi ya kupikia  Shule za Sekondari 19 na Sekondari 12 za bweni zilizo Wilaya ya Nyang’wale ili kulinda mazingira,  Mhe. Kapinga amesema Wizara ya Nishati inaompango wa kuzipelekea nishati safi ya kupikia Taasisi za umma kwa kushirikiana na TAMISEMI.


Katika hatua nyingine Mhe. Kapinga amezishauri Halmashauri  kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia  katika Taasisi zilizopo katika Halmashauri wanazoziongoza kwa kutumia mapato ya ndani.

Jumanne, 13 Mei 2025

KIJANA KABLA YA KUOA SOMA HII

 

Kijana wangu njoo  usikie maneno yangu

 Usioe mwanamke ambaye kwa kumtazama tu unajua ana matunzo ,anaweza kuwa anajitunza mwenyewe anapendeza ,au ana matunzo nyuma usiyoyajua ..endapo unajua maisha Yako ni ya kuungaunga usisogee Kaa pembeni. 


Chukuaaliye pauka au wa kawaida ili angalau wewe unatakapokuwa unampa mafuta ya 3000 anafurahi na kuona anathaminiwa ,, lakini ukichukua mtu anapaka mafuta ya 140000, sabuni ya 40000

Wakati wewe laki na40 unaipigia hesabu za mwezi mzima 😃😃 utaenda pasuka kichwa huko ....


Mwanamke anapiga pamba za 700k 

Wewe unawaza kumzawadia kitenge cha morogo utaenda kuumia

OA mwanamke anayefanana na kiwango chako Cha maisha utaishi kwa furaha ..OA mwanamke anayezidi kiwango chako Cha maisha ukapate presha ...


Usije sema sikusiki ..umesikia Leo


#PASTORLEAH 

.

Ijumaa, 9 Mei 2025

Robert Prevost ni nani? Mfahamu kwa undani Papa mpya Leo XIV

 

Hata kabla jina lake halijatangazwa kutoka kwenye roshani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, umati wa watu uliokuwa chini ulikuwa ukiimba "Viva il Papa" kwa maana ya Ishi milele Papa.

Robert Prevost, mwenye umri wa miaka 69, atakuwa kiongozi wa 267 kwenye kiti cha enzi cha Mtakatifu Petro na atajulikana kama Leo XIV.

Atakuwa Mmarekani wa kwanza kushika wadhifa wa Papa, ingawa anachukuliwa kuwa Kardinali kutoka Amerika ya Kusini kwa sababu ya miaka mingi aliyotumikia kama mmisionari nchini Peru, kabla ya kuwa askofu mkuu huko.

Ana uraia wa Peru na anakumbukwa kwa upendo kama mtu aliyefanya kazi na jamii zilizotengwa na kusaidia kuungfanisha jamii katika Kanisa la eneo hilo.

Alizaliwa Chicago mwaka 1955, Prevost alihudumu kama kijana wa altare na aliwekwa wakfu kuwa padri mwaka 1982.

Katika maneno yake ya kwanza kama Papa, Leo XIV alizungumza kwa upendo kuhusu mtangulizi wake Francis.

"Bado tunasikia masikioni mwetu sauti dhaifu lakini daima yenye ujasiri ya Papa Francis ambaye alitubariki," alisema.

"Tukiungana na kushikana mikono na Mungu, tusonge mbele pamoja," aliwaambia umati wa watu waliokuwa wakishangilia.

Aliwaambia umati uliokuwa ukisikiliza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwamba alikuwa mwanachama wa Shirika la Augustino. Alikuwa na umri wa miaka 30 alipohamia Peru kama sehemu ya misheni ya Augustino.

Francis alimteua kuwa Askofu wa Chiclayo nchini Peru mwaka mmoja baada ya kuwa Papa.

Anawajua vizuri Makadinali kote ulimwenguni kwa sababu ya nafasi yake muhimu kama mkuu wa Baraza la Maaskofu.

Kwa kuwa asilimia 80 ya makadinali walioshiriki mkutano mkuu waliteuliwa na Francis, haishangazi sana kwamba mtu kama Prevost alichaguliwa.

Ataonekana kama mtu aliyeunga mkono kuendelea kwa mageuzi ya Francis katika Kanisa Katoliki.

Ingawa ni Mmarekani, na atakuwa anafahamu kikamilifu mgawanyiko ndani ya Kanisa Katoliki, historia yake ya Amerika ya Kusini pia inawakilisha mwendelezo baada ya Papa aliyetoka Argentina.

Ingawa wakati wake kama askofu mkuu nchini Peru hakuepuka kashfa za unyanyasaji wa kijinsia ambazo zimegubika Kanisa, jimbo lake lilikanusha vikali kwamba alihusika na jaribio lolote la kuficha ukweli.

Kabla ya mkutano mkuu, msemaji wa Vatican Matteo Bruni alisema kuwa wakati wa mikutano ya Baraza la Makadinali katika siku zilizotangulia mkutano mkuu walisisitiza umuhimu wa kuwa na Papa mwenye "roho ya kinabii inayoweza kuliongoza Kanisa ambalo halijifungi ndani bali linajua jinsi ya kwenda nje na kuleta mwanga kwa ulimwengu uliojaa kukata tamaa".

Kutoka BBC Swahili.

2004, Papa Leo XIV alifika nchini Tanzania

Mwaka 2004, Papa Leo XIV alifika nchini Tanzania na kufanya ziara kama Mkuu wa Shirika la Waagustiniani Ulimwenguni. 

Katika.ziara hiyo Papa Leo anayetoka katika Shirika la Order of Saint Augustine (OSA), alifika jijini Dar es Salaam kisha akaenda mkoani Njombe.

Ziara hiyo pia ilihusisha maeneo ya Mahanje hadi mkoani Songea.

 

Alhamisi, 8 Mei 2025

MRITHI WA PAPA FRANCISCO APATIKANA LEO MEI 8 2025

HUYU HAPA PAPA MPYA, KIONGOZI MKUU WA DHEHEDU LA KANISA KATORIKI DUNIANI.

Robert Francis Prevost, aliyezaliwa tarehe 14 Septemba 1955 mjini Chicago, Marekani, ni Papa mpya wa Kanisa Katoliki, akichukua jina la Papa Leo wa XIV.  Kuchaguliwa kwake mnamo Mei 8, 2025, kunamfanya kuwa Mmarekani wa kwanza kushika wadhifa huu katika historia ya miaka 2,000 ya Kanisa Katoliki.

ELIMU NA MAISHA YAKE YA AWALI

Prevost alihitimu Shahada ya Sayansi katika Hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Villanova mwaka 1977.  Baadaye, alijiunga na Shirika la Mtakatifu Augustino (OSA) mwaka huo huo, na akaweka nadhiri zake za milele mnamo Agosti 1981.  Alipata Shahada ya Uzamili katika Theolojia kutoka Catholic Theological Union mjini Chicago, na kisha Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas (Angelicum) mjini Roma  .


HUDUMA YA KICHUNGAJI NA UONGOZI 

Baada ya kupewa daraja la upadre mwaka 1982, Prevost alitumwa Peru mwaka 1985 kama mmisionari.  Alitumikia katika maeneo mbalimbali ya Peru, ikiwa ni pamoja

Jumamosi, 26 Aprili 2025

TANZANIA GOSPEL MUSIC AWARDS KUFANYIKA MEI 23, 2025

 

 Walioingia kwenye kinyang'anyiro wawekwa hadharani.


NA MWANDISHI WETU 

TUZO za Muziki wa Injili Tanzania (Tanzania Gospel Music Awards (TGMA)) zinatarajia kufikia kilele Mei 23, 2025 kwa utoaji wa Tuzo na fedha kwa washindi katia hafla itakayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa jana Aprili 25, 2025 na  Msemaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo hizo Mchungaji Haris Kapiga akizungumza na waandishi wa habari wakati akibainisha watu walioingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hizo zenye vipemgele 20.

Mchungaji Kapiga amesema kuwa mchakato wa Tuzo hizo ulianza tangu Novemba Mwaka jana kwa kufungua dirisha la kila Msanii wa Muziki wa Injili kuwasilisha kwa hiari yake nyimbo zake anazotaka ziingie kwenye kinyang'anyiro hicho huku sharti likiwa ni lazima nyimbo hizo ziwe ni za Mwaka Jana.

"Tuliwaomba watu wawasilishe kazi zao wenyewe kwa vipemgele wanavyoona vinawafaa wao, kazi ya TGMA ni kuwatia moyo watu wenye vipawa ambavyo Mungu amewapatia," amesema Mchungaji Kapiga.

Mchungaji Kapiga ameeleza kuwa jumla ya kazi 529 zilipokelewa ambapo wahusika walipigiwa kura na kupatikana watu watano kwa kila kipemgele na kwamba hatua inayofuata wataendelea kupigiwa kura na kubakia watu watatu kwa kila kipengelea ambapo washindi watapatikana siku ya kilele cha tuzo hizo.

Ametaja vipemgele vya tuzo hizo kuwa ni pamoja na wimbo Bora wa kuabudu wa Mwanamuziki wa Injili wa Mwaka, wimbo Bora wa Muziki wa Sifa, Wimbo Bora wa Muziki wa Injili wa Mwaka na Wimbo Bora wa Injili wa Mwaka kwa wanamuziki wa nje ya Nchi.

Vipengele vingine ni Msanii Bora wa Muziki wa Injili wa Mwaka, Msanii Chipukizi wa Muziki wa Injili, Mwimbaji Bora wa kiume wa Muziki wa Injili wa Mwaka, na Mwimbaji Bora wa Kike wa Muziki wa Injili wa Mwaka.

Akiendelea kutaja vipengele vingine Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo hizo Nina Mbura, amesema ni Kwaya/bendi bora ya Muziki wa Injili ya Mwaka, Video Bora ya Muziki wa Injili, Mtayarishaji Bora wa Video ya Muziki wa Injili wa Nota na mtunzi Bora wa Muziki wa Injili wa Mwaka.

Vingine ni Mwandaaji Bora wa Muziki wa Injili wa Mwaka, Mtayarishaji wa bora wa Muziki wa Injili wa Mwaka, Kiongozi wa Miziki wa Injila wa Mwaka, ushirikiano wa bora wa Muziki wa Mwaka na tuzo ya heshima Kwa mtu mwenye mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Tasnia ya Muziki wa Injili nchini.

Baadhi ya wasanii wanaowania tuzo hizo ni Paul Clement, Water Chilambo, Japheth Zabron wa Zabron Singers, Joel Lwaga, Rehema Simfukwe, Zabron Singers na kadhalika. 

Hata hivyo Mchungaji Kapiga amebainisha kuwa hadi sasa maandalizi ya hafla hiyo yamefikia asilimia 80.

Jumapili, 1 Desemba 2024

NILIMUITA YESU MARA TATU AKANIOKOA

 

Kunti Abdallah ambaye ni miongoni wa manusura wa poromoko la jengo la Kariakoo ambalo limesababisha vifo vya watu 31 na wengine 88 kujeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo limetokea Jumamosi ya Novemba 16 ametoa ushuhuda juzi kwenye mkesha wa maombi uliofanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT) ushirika wa Kinondoni Dar Es Salaam.

"Niliita Yesu mara tatu, nikaanza kusikia maporomoko ya kifusi yakianguka juu ya mwili wangu. Nikasikia uzito na kila kitu kikanielemea."

Alisema aliendelea kuomba akiwa ndani ya kifusi ilhali amebanwa mwili mzima na baada ya muda alipata ujasiri wa kufungua macho na kuona nafasi ndogo iliyojitengeneza na kusaidia kumwingizia hewa.

"Nilianza kupata hewa nikaanza kumshukuru Mungu na kuimba nikiomba Yesu asinipite, Namshukuru Mungu walikuja vijana wabeba mizigo ambao waliniambia walikuta mguu wangu unacheza na walisikia sauti kwa mbali nikiimba.

"Kama si kumwita Yesu nisingepona, mimi nilikuwa mwisho kabisa wa jengo" alisema Kunti aliyeokoka miaka mitatu iliyopita.

Jumamosi, 10 Agosti 2024

Maandamano ya Watanzania Nchini Kenya Kuombea Amani

 

Mamia ya waumini kutoka Tanzania wa Kanisa la Newlife and Player Center lililopo Mombasa nchini Kenya wamefanya maandamano ya amani kanisani hapo Kilifi leo Agosti 10,2024 kuiombea amani nchi yao (Tanzania) kufuatia uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.

Nabii wa kanisa hilo kutoka Tanzania, Utukufu kwa bwana Peter, amesema kusanyiko hilo linatokana na imani waliyonayo waumini hao kwa kanisa hilo ambalo limekuwa likiwapatia huduma ya pamoja na mambo mengine, kuwaponya maradhi mbalimbali na kuimarisha familia zao.

"Kwahiyo tunaamini silaha hutengenezwa wakati wa amani na kutumika wakati wa vita. Hivyo leo hii tunaomba amani itakayoendelea kutuunganisha watanzania sasa na wakati huo wa uchaguzi.

"Tunaunga mkono juhudi za Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuimarisha amani,umoja,upendo na mshikamano katika nchi yetu," amesema Nabii na kusisitiza kwamba:
Imekuwa ikishuhudiwa katika baadhi ya mataifa kwamba baada ya uchaguzi amani inakua imetoweka, hali ambayo waumini hao wamechukua hatua ya kuizuia kupitia ibada.

Kwa niaba ya wenzake, mtanzania kutoka Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro Rose Godfrey ambaye kupitia maombi ya kiongozi mkuu wa Kanisa hilo, Ezekiel Odero alipona saratani ya kizazi, amesema waumini hao wanaamini nguvu ya maombi, Tanzania itaendelea kuwa na amani.



Muinjilisti wa Kanisa la Newlife and Player Center Ezekiel Odero, akiendesha maombi yaliyohudhuriwa na watanzania ili kuiombea nchi amani katika chaguzi zijazo.






Waumini wa Kanisa la Newlife and Player Center wakiomba maombi mbalimbali ikiwemo kuiombea Tanzania amani kwenye chaguzi zijazo.

Alhamisi, 8 Agosti 2024

USIKUBALI KURUDI NYUMA WEWE, TAFUTA MBINU MBADALA.

Bwana Yesu Asifiwe.
Ni watu wanne ambao waliokuwa wamembeba mgonjwa wa kupooza walimwendea Yesu wakitarajia uponyaji wa mgonjwa wao lakini bahati mbaya walipofika walikutana na umati wa watu ukiwa umemzunguka na haikuwezekana kumfikia kabisa.
Badala ya kurudi nyumbani na kukata tamaa watu hawa walitafuta mpango wa pili ili kufanikisha, walipoona ameingia ndani ya nyumba walimbeba na kumpitisha Darini na baadaye akapata kuponywa.

Marko 2:3-5
[3]Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
[4]Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
[5]Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

HATA WEWE LEO HII HUNA SABABU YA KUKATA TAMAA KWA SABABU YA MPANGO WA KWANZA KUTOKWENDA SAWA, UNAHITAJI KUTOBOA DARI YAKO UPATE KUIPATA HAJA YAKO.
Usione gharama kubwa kupangua matofali kwa ajili ya kuifuata haja yako kwani wale wanne wangerejea nyumbani wangebaki na mgonjwa wao hata wewe usikubali kurudi nyuma bila ushindi.
Umefeli kwenye maombi wewe mwenyewe fanya mpango kazi wa pili nenda kaombe na wapendwa usikubali kuacha maombi, umefeli kwenye maombi binafsi nenda kafunge na kuomba usikubali kutopata matokeo.

Kama Eliya aliomba mara saba ndipo wingu la mvua likaonekana hata wewe usiache kujaribu haijalishi haujaona matokeo bado, usikubali kukaa kimya bila mpango wa kando.
Kila unalolifanya linapofeli usikate tamaa na kurudi nyuma ila simama utafute namna tofauti ya kulifanya, ukiona halifanikiwi nenda kafanye jambo jingine hadi upate matokeo.
Umati uliowazuia wale wanne wasione matokeo , unaweza kuwa ni hofu ya kufanya, maneno mabaya na ya kukatisha tamaa, vita unavyokutana navyo, upinzani binafsi, historia za nyuma, na mambo mengine mengi lakini simama ubadili mpango na utafanikiwa.
UNAPOFELI SIO WAKATI WA KURUDI NYUMA ILA NDIO WAKATI WA KUTAFUTA MPANGO MPYA WA KUFAULU.
@MsemajiwaInjili nikutakie siku njema.

Jumatatu, 29 Julai 2024

9 WAFARIKI DUNIA KWA MSONGAMANO KWENYE TAMASHA LA INJILI

 



Mamlaka za afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimesema takriban watu tisa wamefariki kufuatia msongamano uliokumba tamasha lililohudhuriwa na watu wengi kupita kiasi.

Tamasha hilo la mwanamuziki wa nyimbo za Injili Mike Galambay lilikuwa likifanyika katika uwanja wa Martyr katika mji mkuu, Kinshasa, Jumamosi.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, watoto kadhaa wanaripotiwa kuwa miongoni mwa watu waliofariki, huku watu wengine wakilazwa katika wodi za wagonjwa mahututi baada ya ajali hiyo.

Gavana wa Kinshasa, Daniel Bumba, ametoa taarifa kulaumu kitendo cha kuwepo kwa watu wengi kupita kiasi.

Waandaaji wa tamasha hilo, Maajabu Gospel, wamesema maafisa wa usalama walijaribu kuwatuliza watu waliokuwa wanaleta vurugu, kitendo ambacho kimesabisha watu kupoteza maisha yao.

Waandaji wameongezea kusema kuwa uwanja wa Martyr, ambao unachukua watu 80,000, ulikuwa na watu 30,000 katika tanasha hilo lililofanyika siku ya Jumamosi.

Ajali sawia na hili lilitokea mwaka 2022 kwenye tamasha la mwanamuziki Fally Ipupa ambapo watu 11 walipoteza maisha.

chanzo :BBC 

Jumapili, 28 Julai 2024

"UENDELEE KULIOMBEA TAIFA" DR TUMAIN MSOWOYA




Mwimbaji wa
 nyimbo za Injili maarufu Dkt Tumain Msowoya akiomba leo jumapili KKKT Muwimbi 

Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili nchini  Dkt Tumaini Msowoya amewaomba waumini wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT,)Muwimbi, Usharika wa Ifunda kuendelea kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu, mwakani.

Dr Msowoya ametoa Rai hiyo Leo aliposhiriki ibada ya Harambee ya ujenzi wa kanisa la Kisasa Leo katika kanisaa  la KKKT Muwimbi .

Alisema kuwa Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani hivyo jukumu kubwa la Kila mtanzania kwa Imani yake kuendelea kuombea zoezi hilo.

Pamoja na kuliombea Taifa, amewakumbusha kujiandikisha kwenye daftari la Kudumu la mpiga kura na kuendelea kuiunga mkono Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Msowoya ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa amesema kuwa Chama tawala kimefanya mambo mengi mazuri chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa awamu ya sita Dr Samia Suluhu Hassan hivyo zawadi Pekee kwa serikali na Chama ni kuendelea Kuiunga mkono kwa Kuchangua viongozi wanaotokana na CCM .

 




Baadhi ya waumini KKKT Muwimbi wakiwa ibadani 


Kanisa jipya linlo jengwa

VIDEO: TAZAMA VIONGOZI WA DINI KAGERA WAMUOMBEA RAIS DKT. SAMIA, BASHUNGWA AWAS...










Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kagera wameungana kwa pamoja kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa Kitaifa na Serikali kwa kuendelea kudumisha Amani, Utulivu, Upendano na Maelewano.

Ibada hiyo iliyowakutanisha viongozi wa Dini ya Kikristo na Kiislamu imefanyika leo Julai 28, 2024 katika Kanisa Anglikana Mt. Yohana Kimbugu - Muleba, Kagera iliyoambatana na Ibada ya Shukrani ya Miaka 12 ya Uchungaji wa Askofu Grayson Mutegeki Katunzi pamoja na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa.

Jumamosi, 27 Julai 2024

KANISA LA KIBOKO YA WACHAWI LAFUNGWA LINADHALILISHA KWA MAHUBIRI YA OVYO

 


SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeagiza kufungwa Kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe maarufu Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza Kwa Lulenge, Temeke - Dar es Salaam baada ya kanisa hilo kwenda kinyume cha taratibu za usajili.


Barua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ya Julai 25, 2024 imewaelekeza Mwenyekiti wa Kanisa la Christian Life Church na Mchungaji Dominique Kashoix Dibwe kufunga tawi la Kanisa hilo linaloendeshwa na mchungaji huyo.


 Miongoni mwa sababu zilizotajwa za kufungwa kwake ni kutoa mafundisho yenye kuleta taharuki katika jamii na mahubiri ambayo ni kinyume na maadili, mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania. 


Madai mengine ni kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni, kutoa mahubiri chonganishi na kuhamasisha waumini wa kanisa lake kuua watu kwa dhana au tuhuma za uchawi au ushirikina.


Baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali imeagiza kufungwa Kanisa hilo, baadhi ya vitu kanisani hapo vimeondolewa.


Jumapili, 14 Julai 2024

UKIWA KWENYE NDOA TEMBEA KIFUA MBELE

 


Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza Julai 14, 2024 limesema kuwa kila Mkristo mwenye Ndoa Takatifu anawajibu wa kutembea kifua mbele, huku baba, mama na watoto wakiishi kwa Upendo wa Bwana wetu Yesu Kristo.


Haya yamesemwa katika dominika ya 15 ya mwaka B wa Kanisa na Padri Andrea Massawe katika Kanisa la Bikira Maria Malikia wa Wamisionari-Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza ambapo Padri Massawe aliongoza misa ya Kipaimara kwa niaba ya Askofu Mkuu Renatus Nkwande ambapo walei kadhaa walipata sakrameti hiyo.



Akitoa kipaimara hicho katika Parokia ya Malya yenye vigango 18 Padri Massawe alisema, Parokia ya Malya ni kubwa,yenye waamini wakarimu hivyo wajibu kueneza Injili ni kila mmoja wetu na hata hao wanaopata Kipaimara.


Akiweka msisitizo wa maisha ya ndoa Padri Massawe alisema,


“Wengine wana ndoa lakini kila mmoja anatoka nyumbani kivyake, kwanini unakuja kusali kivyako? Mnatakiwa hata kukaa pamoja mke na mume hapa kanisani, kama mumeo amesahau kukupa sadaka unamkumbusha, Padri akihubiri suala la baba na mama kuheshimu ndoa uko jirani na mke/mume wako hapo hapo u nachomekea kwa kumfinya na kumkanyaga miguun kukumbusha wajibu wake.”


Akiendelea kuhubiri Padri Massawe aliuliza maswali kadhaa kwa waamini wake.


Wangapi hapa hamna ndoa lakini mnaishi pamoja? Hapo alijitokeza muumini mmoja tu.Huku akielekezwa afunge ndoa mara moja. Likaulizwa swali lingine, wenye n doa hapa kanisani ambao mume na mke wapo, wanyooshe mikono, mikono mitatu ilinyanyuka , miwili katika kwaya na mmoja kutoka kwa waamini.



“Nyinyi wenye ndoa ambao mnaimba kwaya siwezi kusema leo hii mkae benchi moja maana kila mmoja anaimba sauti yake, lakini wanakwaya mbona mnaoana wenyewe kwa wenyewe?Wewe mzee na mama kutoka kwa waamini ebu kaeni pamoja sasa hivi.”


Mama aliyependeza Kanisa alimfuata mumewe na kukaa naye pamoja, huku waamini wakifurahia kitendo hicho

.

WAZIRI MKUU ALIPONGEZA KANISA LA TAG KWA KUKUZA WATOTO KIIMANI



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 85 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Julai 14, 2024. (Picha





 Baadhi ya waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) wakiimba wimbo wa kuabudu katika Maadhimisho ya miaka 85 ya TAG kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Julai 14, 2024. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho hayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dkt. Barnabas Mtokambali wakisikiliza wimbo maalum katika Maadhimisho ya Miaka 85 ya TAG kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Julai 14, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho hayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dkt. Barnabas Mtokambali (kushoto) na Rais Mstaafu wa Benin, Thomas Boni Yayi katika Maadhimisho ya Miaka 85 ya Kanisa la TAG kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Julai 14, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza wimbo wa kuabudu wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 85 ya Kanisa la Tanzania Assemblie of God (TAG) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam,Julai 14, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza wimbo wa kuabudu wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 85 ya Kanisa la Tanzania Assemblie of God (TAG) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam,Julai 14, 2024. Kushoto ni Askofu Mkuu wa TAG, Dkt. Barnabas Mtokambali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dkt. Barnabas Mtokambali katika Maadhimisho ya Miaka 85 ya TAG kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Julai 14, 2024. Waziri Mkuu, alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho hayo. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelipongeza Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa mkakati wake wa kukuza watoto kiimani huku wakilijua na kulishika neno la Mungu.


“Pamoja na shughuli ya uinjilishaji, leo nimeshuhudia watoto wadogo wakisema maneno ya Mungu bila kusoma mahali popote na mwingine akiielezea Misingi ya Kanisa la TAG bila kusoma popote. Hii ni kazi kubwa, mnasathili pongezi.”


Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 14, 2024) wakati akizungumza na viongozi na waumini wa Kanisa la TAG ambako alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 85 yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.


Amesema kanisa hilo linawafanya watu kuwa wamoja, kuwa na uhusiano wa kiimani na kijamii na kutoa mafundisho ya umuhimu wa kushiriki katika huduma kutoa misaada, elimu, huduma za afya na maendeleo ya jamii.


“Kanisa hili ni mfano katika kukuza umoja na ushirikiano kati ya Wakristo wa madhehebu mbalimbali na waamini wa dini nyingine nchini, kitendo ambacho kinatuwezesha kama jamii kuwa na mshikamano na kuimarisha amani na usalama.


Waziri Mkuu amesema Serikali ina kila sababu ya kuwashukuru Wachungaji na Maaskofu kwa kazi yao kubwa ambayo inaimarisha amani, utulivu na maendeleo katika nchi.


“Serikali inathamini mchango wa taasisi za dini katika kuimarisha maadili mema, kukemea maovu na mmomonyoko wa maadili. Wakati wote Serikali imekuwa ikifanya kazi kwa pamoja na taasisi za dini hususani katika kampeni za kijamii za kuelimisha na kuhamasisha maadili mema na mwenendo mwema kwa wanajamii.”


Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Tanzania, Dkt. Barnabas Mtokambali amewataka waumini wa TAG hilo wawe na maono makubwa ya kuweza kulivusha kanisa hilo kwa miaka mingine 85 huku akiweka msisitizo kwa vijana kuyabeba maono hayo.


“Wana TAG ninawasihi tuwe na maono makubwa, tufikiri na kufanya mambo makubwa kwa miaka mingine 85 ijayo. Tuwe na umoja, upendo na mshikamano na tuendelee kujituma na kujidhabihu kwa hali na mali ili mambo makubwa yaweze kutokea,” amesisitiza.


Ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita kwa kazi kubwa anayoifanya Bara na visiwani ya kuiletea nchi maendeleo na hasa kuboresha miundombinu.

Amesema kuanzishwa kwa safari za treni ya mwendokasi kutoka Dar es Saalam hadi Morogoro ni hatua kubwa kwa Serikali katika kurahisisha huduma za usafiri pamoja kuchochea ukuaji wa uchumi.


“Binafsi, ninapoongelea maendeleo, naguswa na hii sekta ya usafiri kwa sababu kwa miaka zaidi ya 10, nimekuwa nikisafiri kati ya saa nne hadi tano kuja Dar es Salaam yalipokuwa Makao Makuu ya TAG. Na sasa sasa hivi ofisi zimehamia Dodoma, nimekuwa nikienda huko. Itakapoanza safari za mwendokasi mwezi huu kwenda Dodoma, nitakuwa nimeokoa muda wa saa sita, tatu kwenda Dar es Salaam na tatu kwenda Dodoma,” alisema.


Aidha ameipongeza Serikali kwa kudumisha amani, umoja, utulivu na uhuru wa kuabudu nchini. “Kutokana na kudumisha haya, imekuwa ni tunu ya kipekee ambayo imeliwezesha kanisa la TAG na madhehebu mengine nchini kupiga hatua kubwa sana za maendeleo.”


Mapema, Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Mchg. Joseph Marwa alisema mbali na majukumu ya kutangaza injili, Kanisa hilo linatoa huduma za kijamii pamoja na kukukuza maadili mema miongoni mwa waumini wake.


“Idadi ya wachungaji imeongezeka, makanisa yameongezeka na kufikia 5,918; wainjilisti wamefikia 2,008; majimbo kwa sasa yako 71 na wilaya ziko 860 kutoka 557 za awali, sawa na wilaya mpya 303.”


Alisema TAG inatoa huduma za jamii kwa kujenga shule za msingi, sekondari, ina vyuo viwili vya ualimu, vituo vya watoto yatima 21, vituo vya kulea watoto 89 na vyuo vya ufundi vitano ambapo kwa sasa chuo kipya kinajengwa Manyara. “Kwa nchi nzima, tumeshachimba visima 293 ikilinganishwa na 153 vilivyo kuwepo zamani,” amesema.


Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Benin, Thomas Boni Yayi, Wabunge, wamishenari, viongozi wa makanisa kutoka nchi 13 za Afrika na Asia, viongozi 60 kutoka makanisa ya Kipentekoste, wazee wa imani 10, waangalizi, wachungaji kutoka mikoa mbalimbali na washirika wa TAG.








Listen Mkisi Radio