Tuesday, May 6, 2025
WAZIRI MAVUNDE ATANGAZA KIAMA KWA KAMPUNI 95 ZA UCHIMBAJI MADINI
RAIS MWINYI AKUTANA NA KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Zanzibar kujadili Mustakabali wa Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba Mwaka Huu.
Rais Dkt,Mwinyi ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Serikali inafanya kila Juhudi Kuhakikisha Mifumo yote ya Uchaguzi inafanya Kazi kwa Uhuru ,Amani na Uwazi wakati wa Kampeni, Upigaji kura na Matokeo ya Uchaguzi kwa dhamira ya kudumisha Amani Iliopo kwa Maslahi ya Nchi.
Rais Dkt, Mwinyi ameishauri Kamati hiyo kuwakutanisha Wanasiasa kufanya Mjadala wa pamoja Kuzungumzia Umuhimu wa Amani ya Nchi pamoja na kudhibiti Viashiria vya Uvunjifu wa Amani kabla na Baada ya Uchaguzi .
Aidha ameahidi Serikali Kuendelea kushirikiana na Kamati hiyo ambayo imekuwa ikifanya Kazi Muhimu ya Kuhubiri Amani tangu ilipoasisiwa Mwaka 2005.
Rais Dkt, Mwinyi amesema Mshikamano wa Wananchi na Amani ni Tunu Muhimu kwa Mustakabali wa Maendeleo ya Nchi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati Hiyo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab amesema Mkakati Wa Kamati Hiyo ni Kuhakikisha Mazingira ya Uchaguzi yanakuwa ya Amani wakati wa Uchaguzi, na baada ya Uchaguzi na Wananchi waingie katika Uchaguzi kwa Uwazi, Upendo na Furaha.
Kamati hiyo imemkabidhi Rais Dkt, Mwinyi Kitabu Maalum cha Muongozo wa Viongozi wa Dini Kuhusu Uchaguzi.
DAY CARE ZATAKIWA KUSAJILIWA AMA TAFUTENI BIASHARA NYINGINE YA KUFANYA.
Mratibu wa Familia na Watoto kutoka Halmashauri ya Jiji la hilo,Christon Cletus, akizungumza na wamiliki na walezi wa watoto katika vituo vilivypo Ilala jijini Dar es Salaam leo wakati wa semina ya namna ya kupambana na ukatili kwa watoto.
NA MWANDISHI WETU
WAMILIKI wa vituo vinavyotoa huduma ya kulea watoto na masomo ya awali ‘Day Care’ wametakiwa kusajili vituo vyao la si sivyo watafute shughuli nyingine za kufanya.
Wito huo umetolewa leo Mei 5, 2025 jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Familia na Watoto kutoka Halmashauri ya Jiji la hilo,Christon Cletus, wakati akifungua semina ya siku tatu kwa wamiliki na walezi wa watoto wa vituo vya Wilaya ya Ilala.
Semina hiyo yenye lengo la kuwaelimisha watoa huduma hao wa malezi kwa watoto kukabilana na changamoto ya ukatili, imeratibiwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stad, Furahika kilichopo Buguruni Malapa, Ilala jijini Dar es Salaam.
“Nikiangalia mmejitokeza kwa wingi lakini kwa uzoefu wangu nikiwaangalia hapa, nagundua waliosajili vituo vyao hawazidi wawili na sijajua kuna ugumu gani, hivyo natoa wito kwa wale ambao bado hawajasajili kuwasaliana na Ofisa Ustawi husika ili kupata utaratibu na kusajili.
“Mnaposajili inakuwa rahisi kuwafikia inapotokea miradi mbalimbali ya maendeleo na hata inapotokea unyanyasaji kwa kituo furani inakuwa rahisi pia kufika na kuchukua hatua stahiki, naamini wasio sajiliwa baada ya mafunzo hayo watafuata utaratibu na kukamilisha mchakato huo,” amesema.
Pia alimpongeza Mkuu wa Chuo hicho kwa jitihada za kupambana na ukatili wa watoto na kumtaka hasiishie kwa Wilaya ya Ilala pekee bali afanye semina kama hiyo kwa mkoa wote wa Dar es Salaam ili kuwafikia walimiki na walezi wengi.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Furahika, Dkt David Msuya amewasistiza washiriki wa semina hiyo kuhakikisha baada ya mafunzo hayo wanakwenda kuwa mabalozi wazuri watakaosaidia kuwajenga watoto katika misingi bora na kuwa na kizazi imara kitakachojenga taifa imara siku za usoni.
Kuna baadhi ya vituo kuna mambo mengi mengi mabaya ya unyanyasaji watoto ambayo yanafanywa wakati mwingine kwa kutojua misingi ya malezi na hiyo inakuja kutokana na kuajiri baadhi ya watumishi wasiokuwa na elimu.
Naamini baada ya mafunzo hayo mambo yatabadilika unyanyasaji utapungua kama si kuundosha kabisa na hapo tutakuwa tumeunga mkono Serikali kwa vitendo katika kupambana na ukatili wa watoto hususan katika baadhi ya vituo vya ‘Day Care’, amesema.
Joyce Mndima mshiriki kutoka, Mish Day Care, kilichopo Kata ya Buguruni, amesema anaamini baada ya mafunzo hayo ya siku tatu watatoka na uelewa wa kutosha namna ya kulea watoto toafuti na awali.
“Nashukuru kwa mafunzo hayo kwa maana yatatusaidia kuwalea watoto vizuri na tunakwenda kuwa mabalozi wazuri,” amesema.
ASEMA MBETO "CCM ITAHESHIMU NA KUFUATA USHAURI BILA KUVUNJA KATIBA NA SHERIA "
Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimesema kwa miaka yote kimepokea , kusikiliza na kutekeleza Ushauri wa Wazee, watu mbalimbali , Viongozi wa Dini na Kijamii bila kukiuka matakwa ya Katiba na Sheria.
CCM na serilali zake huendesha utawala bila kuingilia mipaka ya Sheria huku kikiheshimu madaraka ya Serikali, Bunge na Mahakama.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis , ameeleza hayo alipotakiwa kutoa maoni yake kufuatia ushauri uliotolewa na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba.
Mbeto alisema Serikali haziwezi kuzuia Uhuru wa mawazo ya watu na ushauri wa Wazee, lakini akawataka wanaoshauri , watambue kuna mahali unapoishia ushauri wao.
Alisema kupokea ushauri si kosa ila kosa huweza kuwa makosa zaidi aidha katika utekelezaji wa Ushauri huo usiokiuka na kuvunja Sheria, Katiba au kuingilia madaraka ya mihimili mingine.
'Ushauri wa Wazee utabaki kuwa sehemu ya utamaduni wa Serikali za CCM. Kama Taifa tumefika mahali tulipo kwa kuthamini michango na ushauri wa Wazee . Kila jambo lina kipimo na mipaka ya utekelezaji wake " Alisema Mbeto .
Katibu huyo Mwenezi aliongeza kusema , kupokea ushauri wowote , lazima anaeshauri na anayeshauriwa wote walitazame suala husika kama lipo kisheria , lina ugumu na wepesi upi , kwakuwa kila hatua, inahitaji kutekelezwa kwa umakini na tahadhari.
"Mwalimu Julius Nyerere alitoa msamaha kwa Wafungwa wa Kesi ya uhaini baada ya Mahakama kuhukumu kisheria. Rais hakuingilia kesi wakati ikiwa Mahakamani. Alifanya hivyo kwa kuheshimu dhana ya mgawanyo wa Madaraka "Alieleza
Mbeto alisema katika Kesi ya kina Michael Kamaliza na wenzake , alikuwemo Mpigania Uhuru Mstari wa mbele wa TANU , Titi Mohamed lakini Rais kwanza aliheshimu Sheria na Mhimili wa Mahakama.
Aliongeza kusema ikiwa leo Viongozi aidha wa CCM, ACT , Chadema , Chauma na vingine, ikitokea kuvunja sheria, kisha yaanze mazungumzo ya usuluhishi, itakuwa kila anayevunja sheria lazima iwepo meza ya mazungumzo , huko si katika kuheshimu dhana ya Utawala wa Sheria.
"Meli, Jahazi au Ngarawa zinapita majini .Ukiona vyombo hivyo vinasafiri Nchi Kavu au Angani huo ni uchuro. Sheria lazima ifuate mkondo wake. Iwe kwa Wazee , Wanasiasa au Viongozi wote tutumie hekima kila tunaposhauri" Alieleza.
Kadhalika Mbeto alisema katika Awamu ya Tano ya Utawala kulikuwa na baadhi ya mambo kadhaa yalioonekana kuwa magumu lakini hawakutokea
Wazee waliokuwa na ujasiri na kushauri lolote .
NYAMGUMA MAHAMUD AIBUKA MSHINDI HABARI ZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
๐Ni kupitia Tuzo za Uandishi wa Habari za Samia Kalamu Awards
๐Wizara ya Nishati yatambua mchango wake
๐ Yamzawadia fedha taslimu, jiko linalotumia umeme kidogo, kompyuta mpakato na uniti za umeme za mwaka mmoja
๐ Mhandisi Mramba asema Tuzo ni kielelezo cha kuunga mkono juhudi za Rais Samia uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia.
Nyamguma Mahamud, Mwandishi wa Habari kutoka Mlimani FM ameibuka kidedea katika Tuzo za Uandishi wa Habari za Samia Kalamu Awards 2025 kupitia kipengele cha habari za Nishati Safi ya Kupikia ambapo Wizara ya Nishati imetambua mchango wake kwa kumpa zawadi mbalimbali ili kuendelea kuhamasisha utoaji wa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia.
Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo imefanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mohamud amekabidhiwa zawadi zake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.
Mshindi huyo amekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni tano, kompyuta mpakato, jiko linalotumia umeme kidogo na uniti za umeme za mwaka mzima.
"Tunatambua masuala aliyoyaandika katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia, kwahiyo tumemzawadia pia jiko la umeme la kisasa linalotumia umeme mdogo pamoja na umeme wa kutumia nyumbani kwake kwa mwaka mmoja," amesema Mha. Mramba
Amesema Tuzo ya Nishati Safi ya Kupikia ni kielelezo cha kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Samia Kalamu Awards imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa na kaulimbiu ya "Uzalendo Ndio Ujanja'
Monday, May 5, 2025
BASHUNGWA APONGEZA JESHI LA POLISI, KWA KUMKAMATA MTUHUMIWA WA VITISHO DHIDI YA PADRI KITIMA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake katika kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya matukio mbalimbali ya kihalifu, ikiwemo tukio la kukamatwa na kuhojiwa kwa mtu anayetuhumiwa kutoa ujumbe wa vitisho kabla ya shambulio dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima.
Bashungwa alitoa pongezi hizo leo, Mei 5, 2025, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jumanne Muliro, kuhusu hatua zinazochukuliwa na Jeshi hilo kufuatia matukio mbalimbali ya kihalifu.
“Nimepata taarifa za kukamatwa na kuhojiwa kwa aliyetoa vitisho kabla ya tukio la kushambiliwa la Padri Kitima. Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada mbalimbali zinazoendelea za ufutiliaji wa matukio mbalimbali yaliyotokea” amesema Waziri Bashungwa.
Aidha, Waziri Bashungwa amelielekeza Jeshi la Polisi kuendelea na msako dhidi ya washukiwa wa matukio yote ya kihalifu na kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria kwa haraka.
BALOZI KAGANDA AHIMIZA USHIRIKIANO KWA WATUMISHI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ZIMBABWE
Mwandishi Wetu Harare Zimbabwe.
Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe Mheshimiwa Suzan Kaganda, amewasili Nchini humo tayari kuanza majukumu yake katika Balozi hiyo huku akiwaomba watumishi kushirikiana ili kutimiza azima ya viongozi wa Nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali.
Ametoa kauli hiyo leo Mei 05, 2025, Jijini Harare wakati alipowasili kwa mara ya kwanza na alipofanya kikao na maafisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe ambapo amesisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi na tija kwa mataifa hayo.
Balozi Kaganda ameongeza kuwa, matarajio ya viongozi wakuu wa Tanzania na Zimbabwe wanategemea kuona Balozi hizo zinaleta matokeo chanya na kutangaza fursa zilizopo katika nchi hizo.
Vilevile amesisitiza kuwa, ni vyema kudumisha umoja uliopo baina ya maafisa katika kutekeleza sera ya Mambo ya Nje.
Friday, May 2, 2025
UJENZI WA DARAJA LA JPM UMEFIKIA 99% KUKAMILIKA MWANZA
Mradi mkubwa wa ujenzi wa Daraja la JPM linalounganisha wilaya ya Misungwi na wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza umefikia asilimia 99 ili kuweza kukamilika .
Hayo yamesemwa na msemaji mkuu wa Serikali Greyson Msigwa mara baada ya kufanya ziara katika Daraja hilo na kujionea hatua ya ujenzi iliyofikiwa ambapo kwasasa yamebakia marekebisho madogo ili kukamilika
Msigwa pia amesema kuwa daraja hilo litakuwa na uhai wa miaka mia moja ambapo siku nyingi litaanza kufanya kazi ili kuondoa changamoto ya wananchi kusubiri kivuko kwa muda mrefu
Aidha kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa ujenzi huo Mhandi Wiliam Sanga kutoka Tanroad amesema kuwa tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi huo jumla ya ajira 33505 ambapo wazawa ni asilimia 91.9 ambapo mpaka sasa wamemlipa mkandarasi shilingi Bilioni 539 .
Katika ziara hiyo ya Msemaji mkuu wa serikali ametembelea na kukagua pia mradi wa ujenzi wa vivuko 5 vinavyojengwa na Songoro Marine pamoja ujenzi wa meli ya Mv Mwanza.