JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumanne, 13 Mei 2025

RC CHALAMILA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA CHARLES HILARY-DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila  leo Mei 13, 2025 ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu  na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Charles Hilary Jijini Dar es Salaam.


RC Chalamila wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Charles Hilary  katika Kanisa la mtakatifu Batholomayo Anglikan, Dayosisi ya Ubungo ameongoza harambee maalum kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa Kanisa hilo ikiwa ni Sadaka lakini pia kumuenzi marehemu kwa kuwa wakati wa uhai wake alikuwa mtu wa kujitoa sana katika kanisa.


Aidha mwili wa Charles Hilary umeagwa na Viongozi wa Serikali, Mabalozi, Taasisi mbalimbali, wawakishi kutoka vyombo vya habari na watu wengine mashuhuri.


Mwisho mwili wa Charles Hilary unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea Zanzibar kwa ajili ya maziko.

 

Mwili wa Charles Hilary, umewasili leo Visiwani Zanzibar


 Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Charles Hilary, umewasili leo Visiwani Zanzibar na kupokelewa katika Bandari ya Malindi na umati wa watu wakiwemo ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wa Serikali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mheshimiwa Idrisa Kitwana Mustafa.


Baada ya mapokezi hayo ya heshima, mwili wa marehemu ulipelekwa nyumbani kwao eneo la Makadara, ambako ulifanyiwa ibada ya sala fupi na maombi ya kumuombea marehemu apumzike kwa amani.


Itakumbukwa kuwa marehemu Charles Hilary alifariki dunia alfajiri ya tarehe 11 Mei 2025 katika Hospitali ya Lugalo, jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi. 


Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali na kuwa daraja kati ya Serikali na wananchi kupitia nafasi yake ya Uongozi Ikulu.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia viongozi wake wakuu, imetoa pole kwa familia, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mkubwa, na imesisitiza kuwa Taifa limepoteza mmoja wa watumishi wake mahiri, mwadilifu na mzalendo.

WATAALAMU WA UJENZI WA MFUMO WA NeST WANOLEWA USALAMA WA MIFUMO



Na Mwandishi wetu
ARUSHA

Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) inaendelea kuboresha na kuongeza kasi ya matumizi ya teknolojia  ili kuimarisha utendaji kazi katika maendeleo ya sekta ya Ununuzi wa Umma Nchini. 

Akizungumza Leo Mei 13, 2025 wakati akifungua mafunzo ya Usalama wa Mifumo ya TEHAMA Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Bw. Dennis Simba amesema, eneo la Ununuzi wa Umma ni eneo nyeti ambapo usalama wa taarifa zake zinazohifadhiwa ni kipaumbele cha Serikali hivyo ni muhimu Mifumo hiyo kuwa na Usalama wa kiwango cha juu.
“kutokana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na watu wenye nia ovu kutaka kupata taarifa zinazowanufaisha ni muhimu Usalama wa Mfumo tunaoujenga uwe wa kiwango cha juu na mafunzo haya yawafanye wataalam wetu waweze kuulinda Mfumo dhidi ya wale wote wenye nia Ovu. “Alisema Mkurugenzi Simba.

Aidha Mkurugenzi Simba ameongeza kuwa Mamlaka itaendelea kutekeleza maelekeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wataalamu wanohusika na ujenzi na usimamizi wa mifumo, wanaendelea kujengewa uwezo ili kuweza kuendana na mabadiliko ya teknolojia yanayotokea siku hadi siku, ingawa wataalamu hao wana uwezo mkubwa wa kuendesha na kulinda usalama wa mifumo hiyo.


“Mamlaka tunaendelea kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, hivyo niwatake washiriki wote wa mafunzo haya, kuhakikisha katika kipindi hiki cha wiki mbili munazingatia maelekezo ya wakufunzi na kuhakikisha munafanya mazoezi kwa vitendo ili kuweza kuongeza taaluma itakayowasaidia vilevile mumepata fursa ya kujifunza kwa nadharia na vitendo na Mamlaka itaendelea kuweka mazingira ya kuendelea kujifunza na kufanya mazoezi mara kwa mara.” Alisisitiza Mkurugenzi Simba 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ujenzi wa Mfumo wa NeST Bw. Michael Moshiro amesema Mamlaka itahakikisha wataalamu hawa wanaopata mafunzo wanakuwa na ujuzi madhubuti wa Usalama wa mifumo ili  kulinda taarifa za Serikali kwa manufaa ya Taifa.
“Kama munavyofahamu PPRA kwa kushirikiana na taasisi zingine za Serikali yetu tunajenga na kusimamia mfumo, na mfumo huu umejengwa na wataalamu wetu wa kitanzania, Aidha, tunafahamu kuwa teknolojia inakuwa kwa kasi nchini hivyo PPRA tumepokea maelekezo ya kuhakikisha wataalamu tunaowatumia wanapata mafunzo stahiki ambayo yataweza kuwasaidia kujenga mfumo lakini pia mfumo kuwa salama.”Alisema Bw. Moshiro.


Mafunzo hayo yanayohusisha Wataaalamu wa Ujenzi wa Mfumo wa ndani ya Mamlaka pamoja na Mtaalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu yanafanyika Jijini Arusha  kwa muda wa siku siku 12 kabla ya kutamatika ifikapo tarehe 24 Mei, 2025.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

 

Iringa


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi-Tamisemi anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu zoezi la usafi wa barabara, akisisitiza kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu.


Mhandisi Mativila amesema hayo mkoani  Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Wenda–Mgama Km.19 inayojengwa na TARURA kupitia mradi wa RISE kwa gharama ya shilingi bilioni 29.7 ambayo imefikia asilimia 99 ya utekelezaji.

Mhandisi Mativila amesema usimamizi mzuri wa barabara unahitajika ili kuhakikisha barabara hizo zinadumu na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.


"Ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa barabara hizi zinatunzwa, hasa kwa kuhakikisha zinaendelea kuwa safi na salama kwa matumizi. Hili ni jukumu la pamoja,” amesema Mativila.


Ameongeza kuwa uwepo wa barabara bora unachochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kuwawezesha wananchi kusafirisha bidhaa na huduma kwa urahisi, hali inayosaidia kuongeza mapato ya halmashauri kupitia ushuru na tozo mbalimbali.

Aidha, Mhandisi Mativila ametoa onyo kwa wakandarasi wazembe wanaoshindwa kutekeleza miradi kwa viwango vilivyokusudiwa au kuchelewesha kazi, akisema serikali haitasita kuwachukulia hatua kali.


“Serikali inataka kuona thamani ya fedha inaonekana katika kila mradi na hatutavumilia uzembe unaokwamisha juhudi hizi za maendeleo,” amesisitiza.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Wenda–Mgama ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha miundombinu ya vijijini kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi.

ZAIDI YA NYUMBA 800 MTWARA KUUNGANISHWA NA MFUMO WA GESI YA KUPIKIA – KAPINGA


*📌 Awasisitiza TPDC na REA kushirikiana ili kuongeza kasi ya kuunganisha gesi majumbani*


*📌 Asema Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia  ni endelevu.*


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) inatarajia kuunganisha mfumo wa gesi ya kupikia katika nyumba takribani 865 mkoani Mtwara kwenye maeneo ambayo yana miundombinu ya bomba la gesi.


Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 13, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Tunza Malipo aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali katika kuunganisha gesi kwa Taasisi na Nyumba za Wananchi mkoani Mtwara kwa ajili ya kupikia.

 

"Katika Mkoa wa Mtwara, Serikali imeshapeleka miundombinu ya usambazaji gesi asilia katika baadhi ya maeneo ambapo jumla ya nyumba 425 na Taasisi nne (4) zimeunganishwa na mtandao wa matumizi ya gesi asilia katika maeneo ya Mtwara mjini."  Amesema  Kapinga


Ameongeza kuwa,  katika nyumba hizo 865 zitakazounganishwa na mfumo,  Serikali imeshafanya usanifu wa kihandisi kwa ajili ya kwenda hatua ya kuunganisha.


Ameweka bayana kuwa,  tayari Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshauagiza  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na TPDC  kushirikiana ili  kuongeza kasi ya kuunganisha gesi asilia kwa wananchi wa Mtwara na Lindi. 


Akijibu swali la Mbunge wa Temeke, Mhe. Dorothy Kilave aliyeuliza kuhusu Serikali kuona umuhimu wa kuharakisha kuunganisha gesi kwenye masoko kama vile Sterio, Temeke, Keko na Mtoni kwa ajili ya Mama Lishe na Baba Lishe, Mhe. Kapinga amesema  Serikali inao mkakati kupitia TPDC kuunganisha gesi asilia katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. 


Ameeleza kuwa, kwa masoko ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja Serikali imeyachukua na itaenda kuyafanyia tathmini.


 Mbunge wa Momba, Mhe. Mhe. Kondesta Sichwale kwa upande wake aliuliza kuhusu suala la  mitungi ya ruzuku kufikia idadi ndogo ya wananchi na kuishauri Serikali kupeleka mitungi ya ruzuku kwa watendaji wa Kata ili kila mwananchi achukukulie hapo kwa kitambulisho cha NIDA.


 Kuhusu suala hilo Kapinga amesema Serikali inaanza kugawa mitungi ya ruzuku takribani  420,000 ambapo utaratibu ni kila mwananchi kuchukua mtungi wa gesi kwa kutumia namba yake ya NIDA ama kitambulisho cha NIDA  ili kumuwezesha mwananchi mmoja kupata mtungi mmoja.


Ameongeza kuwa,  Serikali pia ilitenga mitungi  3,255 kwa kila Wilaya ikiwa ni hatua ya kuanza kwa mkakati wa nishati safi ya kupikia ambapo amewahakikishia Wabunge kuwa mkakati huo ni wa miaka kumi na endelevu.


Mhe. Kapinga ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka kumi asilimia 80 ya watanzania watakuwa wanatumia nishati safi ya kupikia ambayo ndio maono ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

KIJANA KABLA YA KUOA SOMA HII

 

Kijana wangu njoo  usikie maneno yangu

 Usioe mwanamke ambaye kwa kumtazama tu unajua ana matunzo ,anaweza kuwa anajitunza mwenyewe anapendeza ,au ana matunzo nyuma usiyoyajua ..endapo unajua maisha Yako ni ya kuungaunga usisogee Kaa pembeni. 


Chukuaaliye pauka au wa kawaida ili angalau wewe unatakapokuwa unampa mafuta ya 3000 anafurahi na kuona anathaminiwa ,, lakini ukichukua mtu anapaka mafuta ya 140000, sabuni ya 40000

Wakati wewe laki na40 unaipigia hesabu za mwezi mzima 😃😃 utaenda pasuka kichwa huko ....


Mwanamke anapiga pamba za 700k 

Wewe unawaza kumzawadia kitenge cha morogo utaenda kuumia

OA mwanamke anayefanana na kiwango chako Cha maisha utaishi kwa furaha ..OA mwanamke anayezidi kiwango chako Cha maisha ukapate presha ...


Usije sema sikusiki ..umesikia Leo


#PASTORLEAH 

.

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MDAHALO WA MAWAZIRI WAKUU KWENYE JUKWAA LA MAAFISA WATENDAJI WAKUU


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika mdahalo wa Mawaziri Wakuu kuhusu namna Sekta ya Umma inavyoweza kushirikiana sekta binafsi ili kuchochea maendeleo, mjadala huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Sofitel Mei 12, 2025 jijini Abidjan, Ivory Coast. Mawaziri Wakuu walioshiriki mjadala huo ni Waziri Mkuu wa Cameroon, Joseph Dion Ngute,Waziri Mkuu wa Ivory Coast Robert Beugré Mambé pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Guinea Amadou Oury Bah

MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UJENZI WA SOKO LA KISASA

 

▪️Ni soko kubwa la kipekee la Machinga Complex


▪️Machinga Wanawake Dodoma wazindua Umoja wao


▪️RC Senyamule ataka Jiji kuongeza maeneo ya kufanyia biashara 


▪️Mbunge Mavunde awataka Machinga Dodoma kuchangamkia Mkopo wa Bilioni 7 za Jiji


*Dodoma*


Umoja wa Wanawake Machinga Dodoma(UWAMADO) wamempongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa ujenzi wa soko la kisasa la Machinga Complex na miundombinu ya kisasa ya soko hilo ambalo ni la kipekee nchini.


Hayo yamesemwa jana wakati wa uzinduzi wa chama cha UWAMADO uliofanyika kwenye eneo la soko la Machinga Complex kwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule

Akisoma Risala Katibu wa UWAMADO Bi. Mariam Kajembe amesema umoja huo umelenga kuwaleta wanawake Machinga pamoja ili kujijenga na kujiimarisha uchumi.


Aidha pia UWAMADO umempongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa ujenzi wa Soko la Machinga Complex ambalo limesaidia kuwaleta pamoja wafanyabiashara wengi wadogo pamoja ambao awali hawakuwa katika maeneo rasmi na hivyo kuwafanya kutokuwa rasmi.


Akitoa hotuba yake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule amewapongeza UWAMADO kwa kuamua kuanzisha umoja wao ambao utawasaidia kujiendeleza zaidi na kujiimarisha kiuchumi.

“Jambo hili la kuanzisha umoja ni jambo jema,hakikisheni umoja unafikia malengo mliyokusudia.


Mh. Rais kawajengea soko kubwa na zuri,soko hili liwe kichocheo cha ukuaji wenu kimtaji na kibiashara.


Niwatake Uongozi wa Jiji la Dodoma kuendelea kubuni na kuanzisha maeneo mapya ya kuwapanga vizuri wafanyabiashara wadogo wa Dodoma”Alisema Senyamule

 

Akitoa salamu zake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewapongeza UWAMADO kwa kuona umuhimu wa kukaa pamoja kujiinua kiuchumi na kuwataka kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Jiji ambayo kiasi cha Shilingi Bilioni 7 kimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu.

Listen Mkisi Radio